Hivi tungekodi kampuni ya Uingereza kuchunguza makinikia tungejua tulichojua?

Kwa nini anahimizwa afuate taratibu, lakini hataki kuzifuata...! ? Anaruka huyo Chief.?
 
Tusinge kodi kampuni za nje tungeweza kujua hata tuna Gesi kiasi gani?.
Si lazima waseme wamegundua ndio muingie mkataba wa kuchimba? Hata hivyo tuna hakika kama kiasi walichosema kipo ni kweli au ipo gesi zaidi?
Kwa upande wa madini si tumewahi gundua kampuni za kigeni wakichimba na kuuza madini huku wanatueleza bado wanafanya uchunguzi kama madini yapo au hayapo?
 
Kama ni kweli, vip ulilipwa pesa zako?.
Zile ripoti zilikuwa hovyo sana, technical ripoti huwezi kuandika kishabiki vile. Watanzania wengi uwelewa wetu ni mdogo sana hivyo ni rahisi kudanganywa. Mwendazake alikuwa muongo sana.
Nadhani ungesema welewa wako ni mdogo... acha kufikiri kila mtu SOB kama wewe. Sijua mlizaliwa porini... rubbish
 

Stuxnet kama Dkt Magufuli alitudanganya kwenye makinikia acha ahukumiwe huko aliko ila kama watanzania alituambia ukweli basi wewe Stuxnet upate ajali uvunjike miguu yote ila ubaki na mikono ya kuja kushuhudia hapa. Ukiomba msamaha utapona.
 
Mimi nawasifu sana nyinyi wakuu msiokata tamaa kubishana na hawa watu ambao ni “complete illiterates” kwenye uelewa wa mambo ya nchi hii. Mnayoandika yamewazidi sana kiwango chao. Lissu alifafanua masuala ya MIGA vizuri sana lakini wakaishia kumkashifu tu.

Magufuli alijaza team za illiterates mitandaoni, makanisani, misikitini na kwenye vikundi mbali mbali ambazo kazi zake kubwa ilikuwa kupotosha, kuzomea, kuvuruga na kukatisha tamaa mijadala yote ya maana yenye kutafuta na kuonyesha (reveal) ukweli wa mambo yanayofanywa na serikali yake.

Inahitaji moyo yana kujadiliana na watu wa aina hiyo with all the facts bila kuchoka.
 
Mwandiko sasa!
 
Serikali ina mkono mrefu ila ikaingia mikataba ya kifisadi kwa miaka 20? Huo mkono ulikua wapi miaka yote hiyo? Kwamba Mwanyika ni TISS? Mboma JPM alimtaja informant siku ile ile ila akasema Mwanyika ndio msaliti? Unaweza mchafua mtu vile then umpe ubunge alafu expect watu watakuelewa kweli?

Hakuna cha mkono mrefu wala nini ila siasa tu za kilaghai kwamba unafurahisha watu kwenye majukwaa ila nyuma ya pazia hakuna hatua inayochukuliwa. No wonder hakuna hata mmoja aliyewekwa ndani kwa ufisadi Tanzanite na dhahabu kwa miaka yote 20
 
Si lazima waseme wamegundua ndio muingie mkataba wa kuchimba? Hata hivyo tuna hakika kama kiasi walichosema kipo ni kweli au ipo gesi zaidi?
Hivi kwa akili yako watu wanaweza kuwekeza almost TZS 70 TRILLION bila kuwa na uhakika kuna gas kiwango gani?! Hivi unajua hata bajeti ya nchi yako ni kiasi gani ili hatimae uwe na picha TZS 70 Trillion ni nini hasa?
Kwa upande wa madini si tumewahi gundua kampuni za kigeni wakichimba na kuuza madini huku wanatueleza bado wanafanya uchunguzi kama madini yapo au hayapo?
Sasa kinachokushangaza hapo kipi?! Au ufahamu kwamba madini, na hata gesi ni non-renewable resources?


Angalia hiyo timeline iliyotolewa na Shell Tanzania! Kwa kiwango kilichopo kinatarajiwa kuchimbwa kwa muda wa miaka 30-40! Na wanakuambia operations zake zitafungwa ndani ya miaka 2 hadi 3.

Hebu jiulize kwanini wasingendika tu 30, au 35, au 40? Au kufunga miaka 2, au 3?

Usipo-monitor kujua umebakiwa na kiasi gani si unaweza kuwekeza kwa mfano $50M wakati mzigo uliopo huwezi kukupa mapato hata ya $10M!
 
Watanzania hawapendi kulipa kodi wana subiri wafanya kazi wa uma wawalipie kodi, hawataki kukata bima ya matibabu ila wana taka wafanye starehe zao wajifungue bure alafu wapewe uhuru wa kuongea ili wakutukane mitandaoni na kufuatilia umbea.
 
Na ws Na wale waliyo chunguza makenikia, ma Phd holders na maprofesa wakaonyesha aina ya metals zilizoko na viwango ni illiterates?
Mjinga tu,..when it comes to interest of the nation kuna watu wanafikiti ku fend interest binafsi na familia zao tu ndio kua umeelimika.
 
Tatizo ni kukurupuka , wapo watu hawachukui muda kusoma content, wanafuata headlines tu.
Lakini wakati wa Mjomba Magu nani angethubutu kumyoshea kidole?
 

Kwanini sifa za lami usimpe Kikwete umpe Magufuli, lakini za flyover umpe Magufuli usimpe Mbarawa? Ukielewa hapo utakuwa umetoka kwenye lindi la uongo tuliolishwa.
 
Kwanini sifa za lami usimpe Kikwete umpe Magufuli, lakini za flyover umpe Magufuli usimpe Mbarawa? Ukielewa hapo utakuwa umetoka kwenye lindi la uongo tuliolishwa.
Kikwete mwenyewe na awamu ya mkapa walimpa sifa magufuli kwa uadilifu na ubunifu kwenye ujenzi barabara. Kumbuka mkapa alimsifu magufuli kwa kupendekeza kwake na kuanzisha ujenzi wa barabara za lami bila kutegemea mikopo ya nje.
Jk pamoja na kumuondoa kwa muda jpm kwenye ujenzi wa barabara muda mfupi alimrejesha. Mkapa na jk wanastahili sifa kwa kumretain mtu resourceful kama magufuli licha ya fitna nyingi toka wapigaji.
 
na wapuuzi kama nyie eti tutashitakiwa Miga, mbona accecia walifutiliwa mbali na hawakwenda mahakamani Kudai fidia,Kama walikuwa halali na hawaibi?
Kwanza mpuuzi ni wewe unayeshindwa hata kuandika kwa Kiswahili fasaha, kenge wewe!!

Pili, ni mpumbavu tu ndie anaweza kusema mbona hao Acacia hawakwenda huko MIGA manake kila mwenye akili timamu anafahamu Acacia hawakuwa na sababu ya kwenda kwa sababu Serikali ya Mtukufu ilishaingizwa chaka, ama kwa kutofahamu au watu walishakula chao!!

Hivi ungekuwa wewe ndo Acacia, ungeenda MIGA kufanya nini wakati:-

1. Mliambiwa mnadaiwa kodi TSZ Trilioni 450 lakini mnatoa kishika uchumba cha Sh 700 Billion, ambayo haifiki hata 0.5%, tena unakubaliwa kulipa kwa mafungu halafu mnapigiwa makofi!

2. Mmefanya share transfer au mmeuza 34% ya share wakati Sheria inasema unapouza share unatakiwa kulipa 30% kama Capital Gains Tax, lakini hamkulipa!


3. Mmeambiwa itabidi mjenge kiwanda cha kuchenjua hayo makinikia hapa hapa, nanyi mnasema haitalipi, na kwahiyo mnaruhusiwa muendelee kupeleka makinikia Japan!

Sasa kama unatumia kichwa chako sawasawa, na wewe ndie Acacia mwenyewe, hapo ungeenda MiGA kufanya nini?! Soma ile framework uone kilichoandikwa!!

Hivi kwa akili yako pamoja na favors zote hizo bado ulitarajia Acacia waende MIGA ambako kesi zinachukua zaidi ya miaka 5 wakati pale bandarini kulikuwa na makinikia yanayochangia 30% ya mapato yake!!

Lakini kama msingefanya ujinga wa kutoa favors zote hizo, Acacia wangeenda tu kwa sababu wasingekubali kulipa anything like trillions ambazo mlikuwa mnafurahia kwamba mnawadai!

Soma thread hii hapa kuhusu nini alisema Tundu Lissu na ujue ni kwanini jamaa walikuwa wanajidai sana! In short Lissu aliwaambia kama kweli tupo serious na hizi kampuni za madini, basi tujiondoe kwanza MIGA kwa sababu ukishajitoa kule, wanakuwa hawana pa kukimbilia zaidi ya kwenye mahakama zetu wenyewe!!

Lakini kwavile bado tulikuwa MIGA, Acacia na Barrick bado waliendelea na danadana zao, na serikali ilikuwa inahofia ku-press hard kwa sababu, ingawaje wewe mpiga makofi hujui lolote, wenyewe ( serikali) walifahamu hawa ukiwakandamiza hadi wakose pumzi, watakachofanya ni kukimbilia MIGA ambako TUSINGETOKA kwa sababu hata ukaguzi wenyewe ulikuwa wa upande mmoja, na usingekuwa na nguvu zozote kisheria!

Halafu ndugu yangui TUJITEGEMEE, Serikali ya Mzalendo Magu ilipeleka wapi 30% yetu ya Capital Gains Tax?
 
Look at you! Kama ni JPM ndie anastahili sifa za hizo barabara, kwanini sifa za SGR hapewi Waziri wa Ujenzi?! Kwanini hizo makinikia unazosema, sifa usimpe Waziri wa Madini?! Au ndo ile "chako ni changu na changu ni changu"!
 
Mkuu, ile hela ilikokotolewa kuanzia wameanza uchimbaji mpaka leo tokea awamu ya tatu mpaka sasa, na ilionesha ni kiasi gani wamekwepa kwa muda wote huo na je lilikiwa kosa la nani kurihusu upigajiwa dizaini hiyo???
jibu ni tawala za awamu zilizopita, na ndio maana baada ya mazungumzo ikabidi ziwekwe terms mpya kuwa yaliyopita sio ndwele ni kweli makosa yalifanyika ila sasa yasijirudie thats why kikatolewa kishika uchumba cha dola mil 300 na mkataba ukasainiwa upya huku TZ ikipewa umiliki wa asilimia kadhaa, kitu ambacho kitaongeza kiasi ambacho kilikuwa kinapata kutoka kwenye madini maradufu ya awali

je pasipo na uthubutu wa kuzuia yale makontena, tungepata yote hayo?????

ni miaka mingapi makontena yalikuwa yakisafirishwa tu bila kujua kilichomo ndani???
 
Yes ili kuweka good terms, na ndio maana wakatoa Dola milioni 300 na mkataba ulisainiwa upya ili kuinufaisha TZ kitu ambacho hakijawahi kufanyika tokea TZ imeanza kujihusisha na masuala ya madini
Yaani mnadai Trillion 450,000 mnapewa dollar mil.300,000 tu alafu mnashukuru kuwa haijawahi kutokea?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…