Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

KWANZA NTAUA NA KUSAMABARATISHA MIFUMO YA WAZEE WA”REMOTE” HADHARANI ILI NITAKALOFANYA LISIPINGWE AU MIMI KUONDOLEWA PAMOJA NA KUFUMUA UPYA USALAMA WA TAIFA NA KUWAFUKUZA NA KUWAWEKA JELA UVSISIEM WALIOKO HUKO WOTE.


1.TUME MPYA YA UCHAGUZI

2.KATIBA MPYA

3.CAG KUWA NA MENO

4.TAKUKURU KUFUMULIWA NA KUSUKWA UPYA

5. DED KUTOKA KWENYE IDARA NA SI TEUZI

6.WAZIRI ASIWE MBUNGE

7.CHOMBO CHA KUDUMU CHA KUCHUNGUZA MIENENDO YA POLISI

8.MAHAKAMA NA BUNGE KUWA NA MENO

9.UKIKUTWA UNASIFISIFIA SEREKALI KIFUNGO JELA MIEZI 6

10.MKUU WA WILAYA FUTA,KUWE NA MKUU WA MKOA NA MA-DED.

11.NANUNUA GARI AINA YA PROBOX NEW MODEL SAMBAZIA RC NA MA-DED.

12.UFISADI KIFUNGO CHA MAISHA JELA.

13.URAIA PACHA RUKSA

14.WAZIRI WA MAMBO YA NJE NAWEKA MZUNGU

15.MABALOZI NATEUA WENYE UZOEFU NA SI KUJUANA

16.KUONDOA KINGA YA MASHTAKA KWA RAISI NA VIONGOZI WA JUU.

17.FUTA CHEO CHA MAKAMU WA RAISI. ABAKI PM KAMA MTENDAJI MKUU.

18.RAISI AKIFA UCHAGUZI KUIITISHWA

19.SHERIA YA KUZUIA MWANAMKE KUWA RAISI( Hili tunajuta)

20.RC ANACHAGULIWA NA WANANCHI



Mwisho kabisa keki ya taifa ni ya wote na si baadhi ya koo
 
Mimi nitamtaka tu anipe ufafanuzi wa kwa nini miaka nenda sura ni zilezile kwenye Baraza la Mawaziri.
Hivi hakuna sura nyingine zenye sifa? Nchi ina watu zaidi ya milioni 60!

Lakini kila siku wateule ni walewale. Yaani mtu akivurunda Wizara hii, anahamishiwa Wizara nyingine! Ikitokea Mbunge ni mtoto wa Kigogo wa juu, basi lazima apewe unaibu uwaziri! Hii nchi imekuwa ni ya Kisultani!
Linashangaza sana hilo jambo.
 
Viongozi Wa Kiafrica Ndo Wanasababisha Waafrica Wote tuonekane Hatuna Akili Kabisa Na hapo Ndo kunasababisha Tulichukie Bara hili la Giza Tatizo Kubwa ni UONGOZI MBOVU
Tatizo ni viongozi wetu kuwa vibaraka wa wazungu. Hapo ndio shida inapoanziaga.

Ukiwa Patriotic leader lazma wazungu wakutaftie namna wakuhujumu na kukumaliza.
 
Sitamani kuwa kiongozi lakini ingetokea kuwa rais wa nchi hii kwa haraka haraka, ningepunguza gharama zisizo za msingi za serikali, mav8 v8 haya weka kando, gari za hybrid ama umeme ni safi zaidi kuna haja gani mkuu wa wilaya kutembelea gari ya milioni 200 tuna wilaya ngapi?

Gharama za mafuta na umeme ningefanya kila namna zishuke... hivi vitu ni mihimu na athari yake inamgusa mtu wa chiiini kabisa, mfano mafuta mpaka kufika bandari yetu ni 1200+ hayajavuka 1500 iweje yaje kuuzwa 3000? Hapo unashusha mafuta katila kila lita unaweka tu maxmum ya serikali ni buku.. hawa mawakala sijui ewura sijui nani nani, wanaotoza vikodi kiasi inafika 3000 wote watapata bajeti yao kutoka serikalini kupitia hiyo hiyo buku ya serikali... mafuta yatashuka kwa asilimia kubwa.


Mafisadi fisadi woote wataipata fresh ya unga, mtu ukifanya ubadhirifu ukibainika unatema mali zetu ulizomeza,
Katiba mpya hapa lazima ihusike
Mawaziri hawatakuwa wabunge.
Wakuu wa wilaya wawe ni waajiriwa kabisa.

Siasa za kusifiana sifiana ili mtu apate cheo tupilia kule.

Elimu yetu lazima tuipandishe hadhi mtu anatoka engineer ni injinia kweli.. maviwanda ya kuzalisha vifaa vidogo vidogo, sijui chaja chaja, vifeni na takataka nyingine nitahakikisha vinazalishwa hapa, sisi ndio tunauza nje.

Kilimo lazima niwafanyie wepesi wakulima, kiwe kilimo cha kisasa na chenye mantiki, mashamba ya serikali(watu wataajiriwa huko kuzalisha)

Sheria kali saana kwa wabadhirifu.. nahakikisha uzalendo unarudi mtu anaipenda tanzania yake upyaaa.


Mambo ya kurekebisha ni mengi mnooo kwa jinsi nchi yetu ilivyooza.
Utanipa u IGP ikikupendeza
 
Kusali, kufunga, kuomba , kutubu ....kila mtu kwà dini yake kwà siku sita. Baada yapo ni Kazi Kazi, ya kusafisha Nchi.

Nitakua zaidi ya Magufuli mara 6.

Nitakua navaa different masks...popote ulipo nipo. Wakati mwingine nitakua naonekana sehemu nikiwa pekeyangu bila hata ya walinzi.

Nitakua nawafanyia surprise wale wote wasiopenda maendeleo na Mafanikio ya Nchi hii.
 
Kusali, kufunga, kuomba , kutubu ....kila mtu kwà dini yake kwà siku sita. Baada yapo ni Kazi Kazi, ya kusafisha Nchi.

Nitakua zaidi ya Magufuli mara 6.

Nitakua navaa different masks...popote ulipo nipo. Wakati mwingine nitakua naonekana sehemu nikiwa pekeyangu bila hata ya walinzi.

Nitakua nawafanyia surprise wale wote wasiopenda maendeleo na Mafanikio ya Nchi hii.
Kaka ikikupendeza uniweke hata kwenye misafara yako
 
Tanzania kuwa na mikoa 15tu yenye wilaya 45 tu,cabinet wizara 15 tu;All CEOs wa serikali kama IGP,TAKUKURU, TISS etc etc kuomba kwenye hizo nafasi, hakuna uteuzi, ;JUDICIARY kujitegemea kwa kila kitu kuanzia bajeti yao na all judges wote wataomba nafasi hizo;Police nitalifumua jeshi hili na kutengeneza special units within jeshi hili na nitabadili jina ,iwe service na sio Force, wazee wote above 40yrs kwenye jeshi hili nitawapumzisha na kuingiza young guy's wenye fresh mind
 
Nitapanga safu ya wasaidizi wangu wenye Elimu yakutosha; wapenda nchi yao [ patriots] na HONEST individuals yaani waaminifu. Kwa vigezo hivyo definately nitawatoa wengi kwenye uongozi wakiwemo makamu wa Rais Phillip Mpango, waziri mkuu Kassim Majaliwa na waziri wa fedha Mwigullu Nchemba kwani they don't pass the three tests!!
Na wengine wote watakaoteuliwa ni lazima wafaulu vigezo vifuatavyo;

MERITOCRACY
PATRIOTISM
HONESTRY

Na hakutakuwa na longo longo ya ujomba!
MERITOCRACY
PATRIOTISM
HONESTRY

Ukiona mtu anapenda tumia hayo maneno ujue ni laghai au tapeli kama carl peters
 
Picha linaanza nitajenga Jela kubwa sana za kubeba watu kuanzia 5000. Then ghafla bin vuuu nafanya teuzi ya mahakama maalumu ya Mafisadi na wahujumu uchumi.

Ninauhakika 90% ya CCM wataishia jela. Na hilo ndilo litakuwa lengo langu kuzika CCM na mifumo yake ili kukomboa kizazi kijacho kisipatwe na laana zao wajaalaana hawa.

Halafu nitapitisha mchakato wa katiba mpya na kuondoa elements zozote za muingiliano wa mihimili mikuu ya nchi yaani mahakama, bunge na serikali kuu.

Halafu nitabadilisha structure ya uwakilishi kwa maana nitaunda mfumo wa uwakilishi wa moja kwa moja wa raia kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa ili raia wawe na maamuzi ya moja kwa moja na sio kuwa na vikorido korido vya maamuzi kiasi kwamba raia wanajikuta wanawakilishwa badala ya kuwasilishiwa maoni yao.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nahisi Wabunge wangenitoa. Maana ningeanza nao.

1. No V8
2. Kata Posho za Vikao.
3. Sio lazima wabunge wote waudhurie vikao. Zamu zamu kutegemea na muswada unaoongelewa.
4. Vikao vya Virtual vingekua vingi.
5. Katiba mpya.
6. Uchaguzi kila baada ya miaka 4 hafu ahadi za jukwaani wakati wa campaign kama haujafikisha 75% una kesi ya kujibu.
7. Hamna viti maalimu.
 
Kusali, kufunga, kuomba , kutubu ....kila mtu kwà dini yake kwà siku sita. Baada yapo ni Kazi Kazi, ya kusafisha Nchi.

Nitakua zaidi ya Magufuli mara 6.

Nitakua navaa different masks...popote ulipo nipo. Wakati mwingine nitakua naonekana sehemu nikiwa pekeyangu bila hata ya walinzi.

Nitakua nawafanyia surprise wale wote wasiopenda maendeleo na Mafanikio ya Nchi hii.

[emoji3]
 
Hapa mnaotaman kuwa viongozi tuone experience
Watumishi wote wa serikali wakiwemo wa kisiasa wanakuwa na kazi za mikataba renewable baada ya miaka miwili na ukomo ni miaka kumi na tano unaachia wengine nafasi na wewe urudi mtaani kujitegemea. Itasadia sana nchi kwenda mbele sababu viongozi na watumishi wataanza kuweka mazingira mazuri ya biashara wakijua watarudi mtaani muda wowote.
 
Back
Top Bottom