Sitamani kuwa kiongozi lakini ingetokea kuwa rais wa nchi hii kwa haraka haraka, ningepunguza gharama zisizo za msingi za serikali, mav8 v8 haya weka kando, gari za hybrid ama umeme ni safi zaidi kuna haja gani mkuu wa wilaya kutembelea gari ya milioni 200 tuna wilaya ngapi?
Gharama za mafuta na umeme ningefanya kila namna zishuke... hivi vitu ni mihimu na athari yake inamgusa mtu wa chiiini kabisa, mfano mafuta mpaka kufika bandari yetu ni 1200+ hayajavuka 1500 iweje yaje kuuzwa 3000? Hapo unashusha mafuta katila kila lita unaweka tu maxmum ya serikali ni buku.. hawa mawakala sijui ewura sijui nani nani, wanaotoza vikodi kiasi inafika 3000 wote watapata bajeti yao kutoka serikalini kupitia hiyo hiyo buku ya serikali... mafuta yatashuka kwa asilimia kubwa.
Mafisadi fisadi woote wataipata fresh ya unga, mtu ukifanya ubadhirifu ukibainika unatema mali zetu ulizomeza,
Katiba mpya hapa lazima ihusike
Mawaziri hawatakuwa wabunge.
Wakuu wa wilaya wawe ni waajiriwa kabisa.
Siasa za kusifiana sifiana ili mtu apate cheo tupilia kule.
Elimu yetu lazima tuipandishe hadhi mtu anatoka engineer ni injinia kweli.. maviwanda ya kuzalisha vifaa vidogo vidogo, sijui chaja chaja, vifeni na takataka nyingine nitahakikisha vinazalishwa hapa, sisi ndio tunauza nje.
Kilimo lazima niwafanyie wepesi wakulima, kiwe kilimo cha kisasa na chenye mantiki, mashamba ya serikali(watu wataajiriwa huko kuzalisha)
Sheria kali saana kwa wabadhirifu.. nahakikisha uzalendo unarudi mtu anaipenda tanzania yake upyaaa.
Mambo ya kurekebisha ni mengi mnooo kwa jinsi nchi yetu ilivyooza.