Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Punguzo mavyeo ya kipuuzi Mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya, mkurugenzi,katibu tawala yani hadi wananyang'anyana kazi what for!! Uongozi wa mkoa na wilaya watachaguliwa na wananchi wao sio kuteua teua ovyo kunakowafanya wananchi wawe wanafiki nafiki kutaka vyote badala ya kuwa na uzalendo
 
Picha linaanza nitajenga Jela kubwa sana za kubeba watu kuanzia 5000. Then ghafla bin vuuu nafanya teuzi ya mahakama maalumu ya Mafisadi na wahujumu uchumi.

Ninauhakika 90% ya CCM wataishia jela. Na hilo ndilo litakuwa lengo langu kuzika CCM na mifumo yake ili kukomboa kizazi kijacho kisipatwe na laana zao wajaalaana hawa.

Halafu nitapitisha mchakato wa katiba mpya na kuondoa elements zozote za muingiliano wa mihimili mikuu ya nchi yaani mahakama, bunge na serikali kuu.

Halafu nitabadilisha structure ya uwakilishi kwa maana nitaunda mfumo wa uwakilishi wa moja kwa moja wa raia kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa ili raia wawe na maamuzi ya moja kwa moja na sio kuwa na vikorido korido vya maamuzi kiasi kwamba raia wanajikuta wanawakilishwa badala ya kuwasilishiwa maoni yao.
 
sera nzuri kwenye kilimo na viwanda vitaboost maeneo mengine ya nchi kama,elimu,afya na ajira.

Ntaanza kwa kuweka mazingira mazuri kwenye kilimo na uwekezaji wa viwanda kwa kupunguza utitiri wa kodi na kudhibiti urasimu.

sambamba na hilo miaka miwili ya bajet 40% ya bajet ntaipeleka kwenye sekta ya kilimo ili kuweka miundombinu ya umwagiliaji kama mabwawa,mashine na vifaa vya kisasa kwaajili ya kilimo kikubwa na cha kisasa.

tz zaidi ya 80% ya mbolea tunaagiza kutoka nje ya nchi,mimi kama Rais ntahakikisha bwawa la JNHPP linazalisha umeme wa uhakika na wa gharama nafuu bila kuhujumiwa na mafisadi wa nchi sanjari na kupunguza utitiri wa kodi ili kuwavutia wawekezaji waanzishe viwanda vikubwa vya mbolea,nguo,mafuta ya kula,korosho n,k.

ili kuhakikisha dhamira yangu ya dhati kuinua kilimo na kuchochea uwekezaji inafanikiwa vizuri na kwa wakati mimi kama Rais sekta ya viwanda na kilimo vitakua chini ya ofisi ya Rais
 
Nitaondoa mifumo ya kijinga ya kuteuana bila.
Nafas zote za uteuzi unafanywa leo zitakuwa wazi kwa Watanzania WOTE kulingana na sifa zilizoainishwa lakini ni lazima ujaze fomu maalumu na kujieleza kuwa ni Kwa nini unatamani kuwa katika NAFASI Fulani SERIKALINI. .Mfano waziri Wa Viwanda Wa Mambo Wa mifugo . Ni lazima useme kuwa ni Kwa nini unatamani kuwa waziri Wa mifugo. Waziri Wa Elimu unatakiwa useme maono Yako kabla ya kuapishwa Ili niyapime Kama yanatija Kwa Jamii au ni uvundo uliozieleka kukopi na kupest Kila mwaka Toka Kwa watangulizi.

NAFASI za Ukuu Wa Idara zote lazima ueleze unafaa vipi kwenye hizo NAFASI. Na Maoni ya wananchi yatazingatiwa mana Mfano unamteua MTU kuwa Mkuu Wa Polisi halafu ni MTU asiye na maono zaidi ya KUFANYA KAZI Kwa Maslahi yake muda WOTE. Ukimpa NAFASI KAZI yake ni kutengeneza mtandao Wa kukusanya pesa Kwa Wahalifu na kujilimbikizia Mali au Kupiga madili ya kuiba pesa za wale Wa chini ambazo ni stahiki zao halali. Utatumia vipi NAFASI Yako Kwa manufaa ya Umma.

Kwa Nini utoke kwenye familia maskini isiyowahi kumiliki Hata Pikipiki lakini ukiwa Wazuri unataka kutembelea gari ya Milioni 460 kutumia Kodi za Watanzania ? Je, Jamii itanifaikaje na uteuzi WAKO katika kupunguza Umaskini?

MTU kama Prof. Nalichako ,alitokea familia ya kawaida inayojua matatizo wanayopata wafanyakazi hasa wale Wa chini Kama Walimu,Mapolisi,n.k ambao mara nyingine wanahakishwa hamishwa au kupangiwa Maeneo ambayo hawawezi kujitafutia maendeleo kirahisi Wakiwa KAZINI kutokana na mazingira ya KAZI lakini anashabikia Kikokotoo kinachowafanya wafanyakazi Wa chini kuendelea kuwa chini na kuwa na maisha Duni Hata basada ya kustaafu. MTU anapangwa KAZI Mfano Mwanajeshi au polisi kule Pemba akiwa ni mzaliwa Wa Musoma ambapo Kuna ardhi ya asili heka ishirini na wakali huo huo MTU Wa Bara Hana fursa ya kupata ardhi Pemba au Zanzibar , Sasa anastasfu Badala ya kupewa pesa ZAKE zote Ili akaanzisha maisha yake kule anakotaka kutokana na KUFANYA KAZI Kwa muda Mrefu kwenye eneo lisiloruhusu kuwekeza kikamilifu na pia kubanwa na muda na majukumu na kuhamishwa hamishwa!
Cha ajabu unamteua tu MTU kama Mama ndalichako na wengine Wa ajabu ajabu bila kujua maono na mtizamo wake juu ya Jamii iliyojaa maskini 80% ikiwa imegubikwa na wafanyakazi wenye Mishahara midogo , Riba kubwa kwenye mabenki, Kodi kubwa kwenye biashara na familia tegemezi yenye Vijana wengi wasio na Ajira rasmi na fursa zinazofichwa na wale walioteuliwa Kwa manufaa Yao.

Mkurugenzi anateuliwa bila kujua Nini atakachokeenda kukifanya kwenye Jamii iliyojaa WAKULIMA na wafugaji kwenye ardhi Moja Badala yake anatumia muda Mwingi KUFANYA vikao na semina elekezi Kupiga pesa. Wanahangaika na miradi isiyokamilika.Madaraja ya matope ,yanayojengea Kila mwaka . Tumbavu kabhisa!!

Hakuna MTU atapata NAFASI ya uongozi Kama Fadhila . Hapana !!
Utachunguzwa ukiwa na historia Hata ya kimazingira ya kujihusisha na ubadhirifu,rushwa au kuhamasisha rushwa utakaa pembeni.
Sitataka viongozi Wa maigizo na KUFANYA KAZI Kwa kukurupuka.

Kama tunataka kuzuia WEZI kwenye Halmashauri hatuwezi kuchaguana Kwa kujuana. Unataka kuzuia ubadhirifu kwenye wizara ni lazima tuweke watu wenye Nia njema na waliopanda ngazi kutokea chini Kwa uadilifu na uaminifu SIO kumtoa tu MTU Sijui kutoka jalala Gani na kumpa NAFASI kubwa kwenye idara inayohusika na fedha au mipango.

Elimu itakua ya Maana tu Kwa MTU muadilifu.
Msomi anapoitumia elimu yake vibaya na kuihujumu nchi anakua mbaya mara Saba kuliko yule asiyesoma.

Nikiwa Rais Wa nchi hii nitafuta kabisa Riba kwenye mabenki Yote na kufuta mabenki ya Kizungu. Tutaanzisha Benki yenye mifumo ya Kiafrika. MTU atakatwa gharama ya mifumo ya kibenki mwanzoni tu wakati Wa kuchukua mkopo. Baada ya Hapo tutakachoangalia ni kujenga mifumo ya kurejesha fedha Kwa uaminifu Ili wengine wapate na dhamana itaambatana na wadhamini ambao ni Wanachama kwenye mabenki popote Ndani ya nchi.

MTU yeyote atakayezembea kurejesha fedha za mkopo Wa Benki Atakua na hatia ya kifungo gerezani na kufilisiwa Mali ZAKE zote. Masharti yatakua ni makali sana Kwa ajili ya kuhakikisha watanzania wanakopeshwa fedha na kujiajiri Hasa wale wanaomaliza vyuo na kujiunga kwenye vikundi na kupata wadhamini na dhamana. Lakini Riba itakua ni 0% . Miradi watakayoanzisha au kuboresha Italipa Kodi na Hazina itakua na fedha za kuwalipa wafanyakazi Wa mabenki Yote kama zilivyo huduma nyingine za Jamii. Mifumo ya Sasa ya kibenki ni mifumo ya kishetani ya kuzifanya nchi za Afrika na waafrika wanaofanya KAZI za Halili kuendelea kuwa maskini na wanaokaa kwenye viyoyozi kuwaibia pesa zao na Jasho lao kama watumwa Wa mabenki.

Pakitokea Mzungu akataka kuanzisha Benki Basi hataruhusiwa kuwa na Riba inayozidi 5%.

Kilimo na ufugaji:
Kilimo na ufugaji vitaimarishwa sana Kwa kuwekwa mitaala ya kilimo kuanzia Shule ya Msingi SIO kusubiri mpaka watu waingie Sokoine Wakiwa Tayari wamejengeka dhana kichwani ya kuwa WAKULIMA ni wale watu maskini wasiosoma na waliokosa kazi ya kuajiriwa na kukaa Ofisini.

Kila Shule itatakiwa iwe na Bustani za mboga mboga Badala ya Maua na watalima wanafunzi wenyewe Tena kitaalam . Kila Darasa kitakua na aina ya mboga ya kulima na Maji ya mvua itakua ni lazima yavunwe kwenye mashule Yote na kuhifadhiwa kwenye matenki Kwa ajili ya umwagiliaji.
Ni marufuku Shule Kununua nyanya na mchicha NJE ya Shule.
Shule zote za sekondari na msingi kuanzia Darasa la Tano wataanza kujifunza masomo ya kilimo na ufugaji. Watakaokuwa wamevuna mazao Vizuri watayauza na kununuliwa Madafatari na kalamu na vifaa vifaa vingine Ili kuwaonyesha wengine kuwa kilimo ni Ajira ya uhakika na isiyo na masharti magumu zaidi ya kutumia Akili,Maji,Mbolea ,mbegu na ardhi.

Nitaimarisha sana Tume ya watumishi Wa umma Ili Kila atakayepata fursa ya kupewa uongozi basi aweke wazi Mali ZAKE . Na akificha halafu akatokea MTU anazijua mali zilizofichwa na mtumishi Wa umma basi Yule mtoa Taarifa atazawadiwa fedha taslimu Sh. Milioni Kumi au robo ya Mali zilizofichwa . Na Mali hizo zitataifishwa.

Kiujumla nitahakikisha Elimu inaendena na mazingira ya kitanzania na fursa zilizopo kabla ya kunifundisha Mtanzania masuala ya Uingereza na Ureno ni lazima kwanza awe ameshajua kuwa dhahabu inapatikanaje na rubi ikoje na inapatikana Mikoa Gani .

Nitahakikisha Kila MAHALI panapandwa miti ya kijani Badala ya miti ya asili yenye isiyo na kijani. Miti ya asili mingi ni miti yenye Hali ya ujangwa mana Haina rangi ya kijani.
Tutapanda Miti inayoota Kwa haraka na migumu Kama miarobaini, maembe , kachungwa , Minazi n.k.

Madaraja Yote ya vijijini yatajengwe Kwa haraka na Kwa kushirikiana na wafanyabiashara na wanakijiji wenyewe.
Haiwezekani watu wakajenga kanisa au msikiti Wa bil. Moja wanashindwa kushirikiana na Serikali kujenga Daraja la kupitisha mazao Yao na wao kupita. Hiii itasaidia kuharakisha maendeleo na kiwabana watakaohujumu miradi ya umma.

Nitarudisha masomo ya Dini mashuleni Kwa Ajili ya kutengeneza kizazi chenye ujuzi Sahihi Wa Dini wanazoabudu.Hivyo watakaosoma masomo ya Dini watapata fursa ya kuingia Chuo kikuu kama wanaosoma Historia na lugha n.k.
Ni ajabu kumnyima fursa MTU anayejua Islamic knowledge au Divinity kweda chuo kikuu wakati amesoma vitabu vyenye historia ya Sheria na hukumu ZAKE na namna ya kutengeneza ushahidi.

Masomo ya Dini kuwa miongoni Mwa sifa za kujiunga na vyuo vikuu yalifutwa wakati Wa Mkapa na kutoa Mwanya Wa kujenga kizazi kisichojua Umuhimu Wa maadili na ndicho kinachotusumbua Kwa Sasa.

Itakua ni mwiko kabisa Kununua magari ya kifahari Kwa watendaji WOTE Wa Serikali isipokuwa Kwa Rais ,Makamu Wa Rais na waziri mkuu ,Spika Wa Bunge na Jaji mkuu.
Wengine WOTE ni watendaji watakua na magari ya KAZI na ya Bei ya kawaida kama Land cruizer Hard top na asiyetaka atakua amejiondoa mwenyewe mana kuna wanaotamani NAFASI ya kuwatumikia watanzania Hata Kwa kutumia Rav 4
 
Namfungulia mashitaka Ridhiwani Kikwete na baba yake kwa kulitia hili taifa hasara kusaini mikataba ya kijinga ili kumuokoa muuza unga. Nitavunja mikataba yote na serikali ya Kichina iliyosainiwa ili kumuokoa Ridhiwani na kumkamata (Ridhiwani) ili arudishe China kunyongwa. Mtu mmoja hawezi kulitia hasara taifa la watu zaidi milioni 60.
[emoji1787][emoji1787]Sio lazima umfunge Mzee Wa watu . ,,,
Unataifisha Mali zote za huyo muuza unga na kuhakikisha hapati kamwe NAFASI ya kisiasa katika nchi hii.
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi tamani kuwa kiongozi, uongozi ni mzigo uongozi ni mateso
 
Ukiangalia Sanaa Nchi za Kiafrica Kama Kuna Laana Flani hivi haiwezekani Mnakuwa Na Jirani yenu amepiga hatua Kubwa Kimaendeleo Mnashindwa Hata Kwenda kwa Basi tuu kuiga Alichofanya Mpaka Amefanikiwa Mf South Africa Ndo ulitakiwa Uwe mfano Kwetu kuiga Walichofanya Kwenye kila Kitu Lakini Sijui Viongozi wanatembeaga kufanya Nini huko zaidi ya Kulala Five Star Hotel na Malaya
Viongozi hawana mipango kwa ajili ya tanzania, viongozi ni wabinafsi mipango ni kuinyonya tanzania kwa faida ya familia zao, unategemea nini kaka?
 
Sitamani kuwa kiongozi lakini ingetokea kuwa rais wa nchi hii kwa haraka haraka, ningepunguza gharama zisizo za msingi za serikali, mav8 v8 haya weka kando, gari za hybrid ama umeme ni safi zaidi kuna haja gani mkuu wa wilaya kutembelea gari ya milioni 200 tuna wilaya ngapi?

Gharama za mafuta na umeme ningefanya kila namna zishuke... hivi vitu ni mihimu na athari yake inamgusa mtu wa chiiini kabisa, mfano mafuta mpaka kufika bandari yetu ni 1200+ hayajavuka 1500 iweje yaje kuuzwa 3000? Hapo unashusha mafuta katila kila lita unaweka tu maxmum ya serikali ni buku.. hawa mawakala sijui ewura sijui nani nani, wanaotoza vikodi kiasi inafika 3000 wote watapata bajeti yao kutoka serikalini kupitia hiyo hiyo buku ya serikali... mafuta yatashuka kwa asilimia kubwa.


Mafisadi fisadi woote wataipata fresh ya unga, mtu ukifanya ubadhirifu ukibainika unatema mali zetu ulizomeza,
Katiba mpya hapa lazima ihusike
Mawaziri hawatakuwa wabunge.
Wakuu wa wilaya wawe ni waajiriwa kabisa.

Siasa za kusifiana sifiana ili mtu apate cheo tupilia kule.

Elimu yetu lazima tuipandishe hadhi mtu anatoka engineer ni injinia kweli.. maviwanda ya kuzalisha vifaa vidogo vidogo, sijui chaja chaja, vifeni na takataka nyingine nitahakikisha vinazalishwa hapa, sisi ndio tunauza nje.

Kilimo lazima niwafanyie wepesi wakulima, kiwe kilimo cha kisasa na chenye mantiki, mashamba ya serikali(watu wataajiriwa huko kuzalisha)

Sheria kali saana kwa wabadhirifu.. nahakikisha uzalendo unarudi mtu anaipenda tanzania yake upyaaa.


Mambo ya kurekebisha ni mengi mnooo kwa jinsi nchi yetu ilivyooza.
Kura yangu umepata
 
Sitamani kuwa kiongozi lakini ingetokea kuwa rais wa nchi hii kwa haraka haraka, ningepunguza gharama zisizo za msingi za serikali, mav8 v8 haya weka kando, gari za hybrid ama umeme ni safi zaidi kuna haja gani mkuu wa wilaya kutembelea gari ya milioni 200 tuna wilaya ngapi?

Gharama za mafuta na umeme ningefanya kila namna zishuke... hivi vitu ni mihimu na athari yake inamgusa mtu wa chiiini kabisa, mfano mafuta mpaka kufika bandari yetu ni 1200+ hayajavuka 1500 iweje yaje kuuzwa 3000? Hapo unashusha mafuta katila kila lita unaweka tu maxmum ya serikali ni buku.. hawa mawakala sijui ewura sijui nani nani, wanaotoza vikodi kiasi inafika 3000 wote watapata bajeti yao kutoka serikalini kupitia hiyo hiyo buku ya serikali... mafuta yatashuka kwa asilimia kubwa.


Mafisadi fisadi woote wataipata fresh ya unga, mtu ukifanya ubadhirifu ukibainika unatema mali zetu ulizomeza,
Katiba mpya hapa lazima ihusike
Mawaziri hawatakuwa wabunge.
Wakuu wa wilaya wawe ni waajiriwa kabisa.

Siasa za kusifiana sifiana ili mtu apate cheo tupilia kule.

Elimu yetu lazima tuipandishe hadhi mtu anatoka engineer ni injinia kweli.. maviwanda ya kuzalisha vifaa vidogo vidogo, sijui chaja chaja, vifeni na takataka nyingine nitahakikisha vinazalishwa hapa, sisi ndio tunauza nje.

Kilimo lazima niwafanyie wepesi wakulima, kiwe kilimo cha kisasa na chenye mantiki, mashamba ya serikali(watu wataajiriwa huko kuzalisha)

Sheria kali saana kwa wabadhirifu.. nahakikisha uzalendo unarudi mtu anaipenda tanzania yake upyaaa.


Mambo ya kurekebisha ni mengi mnooo kwa jinsi nchi yetu ilivyooza.
Watakuua
 
1. Magereza yote ya mjini navunja naenda kujenga mengine kwenye maeneo ya kilimo km huko mbarali, ifakara, njombe vijijini. Haiwezekani wahalifu waishi mjini
2. Nitabadili Katiba na Sheria za nchi kwenye Mambo mengi sana mf hakutakuwa na wabunge wa viti maalumu, Kinga za viongozi FUTA,
3. Nitatunga Sheria Kali sana kuhusu ukopaji fedha za maendeleo . Hapa ndipo wakoloni walikuja kututawala upya coz mswahili akishasikia mkopo upo yupo tayar kukopata hata km Hana nao mpango/ kipato cha kurejesha
4. Nitatekeleza adhabu ya kifo. Hususani kwa mtu yeyote atayeua kwa makusudi, wauza dawa za kulevya, mafisadi wakuu. nk
5.
 
Back
Top Bottom