Hivi ukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo utafanya nini kwa Taifa lako?

Hapa mnaotaman kuwa viongozi tuone experience
Ningefutilia mbali serikali ya baraza la mapinduzi na kuunganisha Tanzania kuwa nchi moja isiyo na mkoa nyonyaji kama visiwani na kuwafungilia mbali wale wote wanaotuhumiwa na CAG mbali na kuanzisha lifestyle audit kwa kila mwenye madaraka au njuluku
 
Hatua ya kwanza ni kufumua uozo wote kila kona. Nitatumia style ya Magufuli ya kutocheka na nyani.

Kikubwa wafanyakazi wa umma ukomo ni 5 years ofisini unaachia. Ukitaka kwenda senior position unaomba upya na proof kabisa kwamba umeonesha ufanisi wa hali ya juu. Utakula miaka mingine mitano kisha unaachia ngazi kwa kustaafu ukapige mishe zako. Hakuna biashara ya kuzeekea ofisini ila ntaboresha sana maslahi kuhakikisha baada ya hio miaka 5 unaweza kujiajiri maana malipo ya mshahara ntalipa hela ndefu. Ukibainika umefanya rushwa au ufisadi ni miaka 30 jela pamoja na kufilisiwa na kizazi chako hakitaruhusiwa kukanyaga kwenye ajira za umma. Watu wakaendeleze sekta binafsi.

Mahakama ijitegemee kwa kila kitu anzia budget hadi matumizi ila wembe ni ule ule. Sifugi uozo sheria ni miaka mitano mtu asepe. Judge ni miaka 10. Kila mtu akajiajiri waache wengine wapatiemo mtaji humo.

Bunge sio picnic, wabunge mshahara Million 5 ila posho ipungue hadi elfu 70 bila mkopo. Wajitegemee na mapato yao yatategemea na wanaleta maendeleo gani kwa wananchi. Wananchi ndio watafanya harambee ya kumchangia mbunge anunue gari ila kama mbunge ni mzigo basi halambi kitu. Speaker nae asimamie miongozo ya bunge ikibainika kwa namna yeyote anaegemea serikalini na kutetea maslahi ya serikali basi wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani nae apigwe chini mara moja. Hii itaondosha uchawa. Ikibainika kuna dalili za rushwa tu mahali wote ni 30 years jela.

Takukuru nawawekea organ ya kuwabana pumbu kuhakikisha majukumu yao wanayafanya effectively. Wakizingua ni jela tu haina msalia mtume. Aidha ni kufilisiwa jumla jumla na jela tu. Hamna room ya plea bargain
 
Number 11 ... Hahaha
 
Haitatokea mimi kupata nafas hy bora nife na mawazo yangu mazur yenye kupendeza pengine hata lissu au kiongoz yoyote aliopo madarakan kwa sasa hakuna na hatokuja kuwaza, kama niwazavyo mimi mr bann na ninafikiri nafasi ya urais hainitoshi ni kinafas kidogo sana kwangu hiko kinafas nakiona kama kuongoza ngombe malishoni kwakwel hakinitoshi ndio mana bora nife tu na mawazo yangu kwanza moja ya sifa zangu ninauwezo wa kuwaingia watu kwenye akili zao na kuwa amrisha wafanye ninachotaka na hili naliweza hata wakiwa watu milion 30 kingine ninauwezo wa kusafiri ndani ya sekunde kumi kwenye nchi 10 vuta picha kwa uwezo huu nilionao wananchi wangapi nitawafikia ndan ya siku moja so sizan kama kinafasi cha urais kitanifaa mnaweza sema ni utani ila ndio nilivyo asanten kwa kunisoma
 
Hapa mnaotaman kuwa viongozi tuone experience
1.Wabunge wangeomba nafasi za kazi kutokana na uhitaji na sio kuchaguliwa. Kama bunge linatunga sheria basi kigezo sio kujua na kusoma tu, wawepo wajuzi wa mambo pia.
2. Ningegawa maendeleo kutokana upatikanaji wa vitega uchumi na rasilimali kwa kikanda
 
Nafuta kiswahili mambo gani ya kusoma kwa lugha ya kiswahili darasa la kwanza hadi la saba huku nasoma kiingeleza kama somo na bado kinatutoa knock out alafu mara paah form one masomo yote nasoma kwa lugha ya kiingeleza kutesana tuu huko
 
Ati Magufuli alikuwa katili? Bora yeye alimaliza miaka mitano mimi sina uakika kama naweza maliza mitatu, ila hiyo mitatu moto nitakao uwasha lazima izimwe na petrol yenyewe.

Hivi hili baraza la mawaziri lililopo nani anaweza salimika? Anyway..........hawawezi zidi watatu.

Hako ka nchi kadogo ka zanzibar hakawezi kuwa na raisi na jeshi la kujitegemea.huko naweza kuweka gavana awe ana report kwangu.
Which means katiba inabadirishwa ndani ya miezi 3 naana ninakuwa nina muda mchache wa kuishi so kila kitu nafanya fasta.
Aiiiiiiiiiii wakandarasi mlio. Lipwa na jpm miradi yote imesimama mko mnakula bata hamjamaliza nikiaposhwa tu jiondowe wenyewe.

Baba mwenye tamko kutoka mawinguni aiiiiiiiiiiiiiii unatakiwa kuhama mwenyewe kabla sijaapishwa.

Ili kutaka mizizi, naua vyama vyote kwanza nchi naiendesha kwanza bila chama chocolate cha siasa kumbuka hii clause nakuwa nishaiweka kwenye katiba ya kuondoa vyama vyote pale inapo itajika.

Wafanyankazi naomba niishie hapa naona mmejisahau deko limezidi nyodo kazini.

Vigogo nawapunguzia mishahara naajili watoto wote walioko mitaani na vyeti.

Kama ulijenga jengo hifadhi ya barabara na uliambiwa ukagoma ukajenga kwa kiburi sitowi hata notice greda linapita chwaaa.

Ahaaaaa sector ya madini sijuhi nawafanyaje wacha niishie hapa na hii ndo inaweza niondoa haraka.

Napunguza sana nafasi za kuteua watu waombe kazi wapitie kwenye interview hapa namaanisha teuzi zinakuwa chache sana.

Umeme mchi nzina ndani ya miezi 3.

Miaka mitatu mafisadi mnaweza iona mika 1000.
Hii vita si lazima iniondowe? So lazima niache ninetengeneza katiba iliyonyooka bila chenga haya mambo ati raisi kafa mtu yuko kwake hana ili wala lile anaambiwa eti yeye ni raisi hii mistake haiwezi jirudia.

Aisee kila kitu ni katiba so nitahakikisha ndo kitu chankwanza nafanya ndani ya miezi 3.
 
[mention]JamiiForums [/mention] naomba hii heading ipostiwe kwenye mitandao ya kijamii mingine ili kama kuna wezi na wabadhilifu waweze kuuona na waje waone wananchi wanavyotamani wanyongwe na wafungwe jela.

[mention]Maxence Melo [/mention] Huu uzi ni mzuri utawafanya viongozi waupitie na waone maoni ya wadau.Upostini Kwingine .

Ila mimi nahisi kama ngekuwa raisi wa nchii hii ningeuendesha kijeshi kabsaaa magufuli asingefikia mkono wangu wa chuma hata kidgo.
 
Viongozi Wa Kiafrica Ndo Wanasababisha Waafrica Wote tuonekane Hatuna Akili Kabisa Na hapo Ndo kunasababisha Tulichukie Bara hili la Giza Tatizo Kubwa ni UONGOZI MBOVU
Huo Uongozi mzuri utaukodi wapi ikiwa mliopo ndio nyie kutoka corrupt society?
 
Kwani saizi kinashindikana nini kufanya hayo? Harafu swala la Watalii linategemea factor nyingi na zinazotegemeana.
 
Ningehamishia makao makuu ya nchi kijijini kwetu
Pia ningeifanya kanda ya kaskazin kam nchi inayojitegemea
 
Makamba wazir na baba yake ndani au kunyongwa kabisa
Nchemba kunyongwa kabisa

Makam mpango anakuwa wazir wa fedha
Rais

Majaliwa anakuwa makamu wangu wangu

Wazir mkuu namuweka bashiru

Utumishi namrudisha jafo
Mambo ya ndani polepole

Waliotajwa na cag wote jela bila mahakama
Au kunyongwa

Na nataman kuwapa nafasi wataalamu kutoka mzumbe na sua

Ud na udom wakae pembeni kwanza
 
Hizo sera nzuri mbona huzitaji? Kuondosha hizo Kodi unazoita utitiri kwanza zitapunguza Bajeti ya Serikali na hujasema utafidia wapi,pili kufuta aunkupunguza haikupi guarantee ya kupata investors Kwa mda huo huo maana inaweza chukua miaka 2 au zaidi kupata wachache..

Mpaka hapo utaendeshaje Serikali wakati mahitaji yanaongezeka?

Kwani tatizo la Kilimo Cha Tanzania ni uzalishaji au soko? Umeshafeli Hadi dakika hii 🤣🤣

Mwisho Kufuta urasimu Haijawahi kuwa rahisi maana wanaleta urasimu ni staff ambao huwezi kuwepo Kila sehemu kuwa track.
 
Sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba ambazo hazilimwi natengeneza mfumo inakuwa ni vijiji vya ujamaa vinakuwa chini ya Suma JKT vijana wa mjini mabishoo, wavivu, wapiga debe, wakatisha tiketi na wanaokula kwao wanasubiria ajira za serikali nawapeleka huko wakalime na kusindika mazao nchi ipate hela.
 
Hizi ni sera za Kijamaa ambazo zilishashindwa kitambo Sasa ukifanya tuu hivyo haitachukua round Uchumi utaporomoka na ukiporomoka ndio hapo Sasa sijui utapata wapi pesa za Kuendesha Nchi..

Hayo ukiyoyaeleza yanawezekana kama yatafanywa gradually ila wafanyabiashara/investors wakihisi hatari yeyote umekwisha broo maana watasitisha au kupunguza uwekezaji wao matokeo yake utaanza ku struggle Kuendesha Uchumi,waulize Wachina na Cuba..

Mwisho mambo hayo ya kupanda miti,mbogamboga yatakuwa na maana kama Watoto watakuwa wanakula wao shule Sasa sijui maji ya kufanya hayo everywhere yatatoka wapi na kama ni mvua itahitaji ujenzi wa miundombinu kitu ambayo ni pesa na hizo pesa unatoa wapi Kwa Sasa upeleke maji Kwa watu na zingine ujengee Water harvesting infrastructures huko kwenye mataasisi..

Eti Madaraja ya Vijijini yatajengwa na Wanavijiji,Kwa hiari au Kwa lazima? Na kama utaleta force account labda pesa ilipwe Kwa wanavijiji ila ikirudishwa Serikalini Kwa minajiri kwamba unaokoa gharama utaishia kuua sekta ya ujenzi kama Jiwe alivyofanya..

Mpaka hapa nimeona watu wanaweza kujifunza kwamba kumbe kuongea na kupayuka Kila mtu anaweza ila kwenye vitendo Sasa ni vitu viwili tofauti,Ruto na Yule Rais wa Zambia wanalijua hili vizuri Kwa Sasa.
 
Hapa mnaotaman kuwa viongozi tuone experience
Binafsi ningekuwa na Vipaombele vifuatavyo
1.Biashara na uwekezaji,hapa ningepunguza utitiri wa Kodi,tozo nk,
2.Utawala Bora,hapa ningeifanya ugatuaji wa madaraka kwenye Mikoa na ningebadili namna ya kuwapata hao viongozi Ili mambo mengine wafanye huko huko,
3.miundombinu hasa Barabara na Bandari ndio ningefungua Kila Kona,
4.Maji,
5.Elimu yenye mkazo kwenye Uvumbuzi,ufundi na Biashara
6.Maliasili eg Madini na Utalii
7.Kilimo na viwanda,hapa Ili kukupa incentives nikikupa leseni,nakupa grace period ya Kodi miaka 2 au zaidi Ili tuu niwe na uhakika wa Soko la mazao ya Kilimo na mifugo na hasa for exports
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…