Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
- Thread starter
- #41
Halafu nikipata Hela ninunue nisichopenda? Mbona picha nimepiga kwenye room ya wageni na hicho ndo choo Chao au hiki nilinunua kwatumia mchanga mkuu?Usha
Ushamba ni ujinga. Tafuta hela kijana kila kitu utaona rahisi.
Mkuu una uhakika mbuzi ukimpeleka ulaya utageuka kuwa farasi?Umewahi kubahatika kutoka walau nje ya Tanzania? Bila shaka hujawahi ndiyo maana unaanzisha thread kama hii. Nasema hivi kwa sababu Bongo watu wanadhani choo ni lazima kiwe kichafu sana na inzi kwa wingi. Kwa taarifa yako Ulaya hakuna vyo vya kuchuchumaa. Infact ni kuanzia hapo airpot, ukishaingia kwenye ule ukumbi wa kuondokea, kwenye ndege, na unakokwenda kote ni vyoo vya kukaa. Uzuri ni kuwa majuu watu ni wastaarabu na wanajua maana ya hygyne. Na kwa Tanzania kuna watu wengi tu nyumbani wana vyoo vya kukaa. Kama umezaliwa mbugani huko mnakokata magogo vichakani hili linaweza kuwa jambo la ajabu kwako.
Hapa sijazungumzia uchafu kama unavyodai wewe. Pia nipo nafanya kazi na watu Toka mataifa mbalimbali hasa Canada, Australia nk tuna tumia vyoo vya kukaa na visafi masaa 24!
Lakini Bado sijawahi vutiwa na choo Cha namna hii na sio kwamba situmii kuna muda hunibidi tu mfano umeenda semina kwenye maukumbi makubwa ya kisasa nk vyoo ni aina tu ya kukaa hapo hunibidi kutumia.
Narudi hata kama kingekuwa Cha dhahabu au Almasi Bado nisingevutiwa nacho (kukaa) napenda kuchuchumaa mkuu. Ova.
Sio kwamba kwangu Sina ninacho ila ilinibidi niweke Kwa wageni maana sipendi.