Hivi unajisikiaje unapotumia choo cha kukalia?

Usha



Ushamba ni ujinga. Tafuta hela kijana kila kitu utaona rahisi.
Halafu nikipata Hela ninunue nisichopenda? Mbona picha nimepiga kwenye room ya wageni na hicho ndo choo Chao au hiki nilinunua kwatumia mchanga mkuu?
Mkuu una uhakika mbuzi ukimpeleka ulaya utageuka kuwa farasi?

Hapa sijazungumzia uchafu kama unavyodai wewe. Pia nipo nafanya kazi na watu Toka mataifa mbalimbali hasa Canada, Australia nk tuna tumia vyoo vya kukaa na visafi masaa 24!

Lakini Bado sijawahi vutiwa na choo Cha namna hii na sio kwamba situmii kuna muda hunibidi tu mfano umeenda semina kwenye maukumbi makubwa ya kisasa nk vyoo ni aina tu ya kukaa hapo hunibidi kutumia.


Narudi hata kama kingekuwa Cha dhahabu au Almasi Bado nisingevutiwa nacho (kukaa) napenda kuchuchumaa mkuu. Ova.

Sio kwamba kwangu Sina ninacho ila ilinibidi niweke Kwa wageni maana sipendi.
 
Mtu akiwa na maupele, au fungus, gono, UTI na wewe unazoa vilevile, uchafu mkubwa sana hivi vyoo
 
Wasukuma wenzangu ndio tunapinga hivi vyoo, tumezoea kumaliza haja mashambani, hakuna namna tuzoee ndio dunia inakoenda huko.
 
Inategemea choo kinatunzwaje,vingine vinakua visafi,muda wote wahudumu wa usafi wanafisafisha na dawa na kupulizia perfume,aisee yaani kuna wakati usingizi ukinibana ofsin nakimbilia hapo na kukaa na kusinzia au nachat kabisaa.
Kama kwenu kuna vyoo visvyo na matunzo naomba uvikwepe.
 
Labda niweke sawa mim,i hata kikiwa cha pekee yangu ile style ya kukaa ndo huninyima raha hayo ya usafi wala sijaongelea.
 
Mkuu unajipunja maisha ujue!

Choo cha chumbani mwako unaogopa kupachika cha kukaa!

Yaani mimi bila hicho sinyi najibana hadi nirudi nyumbani kwangu.

Kabla ya sifa zingine, choo hicho ni 'sound proof'.

Hata kama unaendesha zako, unapoanza kupiga piano taatratatata, hata ukiwa karibu na 'wasoni', hupati aibu maana sauti yote inamezwa unapokuwa umekaa juu ya sinki la choo, makalio na mapaja huzuia sauti isitoke nje.

Kingine, ukaaji wa kuning'inia unapojisaidia juu ya sinki, kinyesi chote hukamuliwa na kuisha kabisa katika rectum, si rahisi kupata bawasili.

Kuogopa kutumia choo cha kukaa ndani ya chumba chako ni sawa na kuogopa kivuli chako mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…