Hivi unamchukuliaje mtu wa namna hii?

Hivi unamchukuliaje mtu wa namna hii?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
HIVI UNAMCHUKULIAJE MTU WA NAMNA HII?

Anaandika, Robert Heriel

Hivi unamchukuliaje mtu ambaye kazaliwa mjini lakini hajasoma? Yaani kuna shule na vyuo vya kutosha lakini yeye hajasoma, yaani Hana hata elimu ya diploma wakati vyuo hivyo amezaliwa amevikuta. Hivi mtu wa namna hiyo unamchukuliaje?

Unamchukuliaje mtu ambaye anajiita Muislam safi lakini haijui Quran na yupo comfortable 😂😂, au Mtu kujiita Mkristo Safi alafu hajui hata Biblia na wala hajui abc za Ukristo na yupo Comfortable kabisa. Hivi watu wanamna hii wewe unawachukuliaje?

Hivi unamchukuliaje mtu anayejifanya anajua Sana kingereza na kujivunia nacho alafu wakati huohuo ukimuambie azungumze lugha mama yake hajui. Mtu WA namna hiyo unamchukuliaje?

Hivi unamchukuliaje mtu anayeishi kijijini lakini Hana Shamba analolimiliki, mtu wa namna hiyo unamchukuliaje?

Hivi unamchukuliaje mtu ambaye kavaa vizuri na yupo smart Kwa nje lakini mahali anapoishi ukiingia ndani utabaki mdomo wazi. Mtu wa hivyo unamchukuliaje?

Hivi unamchukuliaje mtu kasoma mpaka degree na kahitimu vizuri lakini anakuambia Hana kazi. Na yupo comfortable kabisa. Unamchukuliaje? Je utaungana naye au utamuona katika jicho jingine?

Unamchukuliaje mtu anayeishabikia CCM alafu maisha yake ni dhoofu ilhali, yakifukara na yasiyo na matumaini. Unamchukuliaje mtu huyo?

Unamchukuliaje mtu anayekuona huna kazi ya maana lakini umemzidi kipato/maisha😂😂.
Yaani yeye anahangaika kila siku lakini maisha yake ni yaleyale.

Unamchukuliaje mtu ambaye anakuona mshamba, ananyuka viwalo na kujipenda lakini anakuja kukukopa kila iitwapo leo, au unamdai yeye au mke wake. Unamchukuliaje?

Unamchukuliaje mtu anayejivunia kuishi mjini wakati huko mjini Hana la maana analolifanya zaidi ya kugeuzwa MSUKULE au mtumwa wa wenye navyo. Unamchukuliaje?

Unamchukuliaje mtu unayemheshimu na kumuona anaakili lakini analishwa na mkewe. Au anaendeshwa endeshwa na mkewe?

Unamchukuliaje mtu anayeshauri watu namna ya kuwa Tajiri wakati huohuo yeye mlo mmoja tuu unamshinda. Mtu wa namna hiyo unamchukuliaje?

Unamchukuliaje mtu ambaye anadharau makabila ya watu wengine au kudharau watu wengine ambao Wana sifa za ndugu zake au wazazi wake?
Mfano, mtu anadharau watu wasio na vipato au wenye kazi za kuvuja jasho ilhali mama yake mzazi au Baba au dada au Kaka zake wanafanya kazi hizohizo, mtu wa hivyo unamchukuliaje?

Mwisho, tuache kudharau wengine Kwa sababu za kijinga.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
We Taikon unatuchukuliaje sisi kutuletea story ya ukweni lakin safari ya itaendelea kwa chamdeko hujatuletea?
 
Unamchukuliaje Waziri ambaye yupo busy kupandisha Tozo,bando,kukata maji, Umeme?
 
Kuna wale wanamjua kila tajiri aliye mjini anamiliki nini na ukubwa wa utajiri wake na wameupatehe wakikaa ni story za matajiri tu halafu wao kutwa kucha wapo vijiweni wanaganga njaa hawafanyi hata kazi zaidi ya story za nani yupo wapi na anamiliki nini.Siwaelewagi hawa watu kabisa.
 
Back
Top Bottom