Hivi unapofumba macho bila kusinzia huwa unaona?

Hivi unapofumba macho bila kusinzia huwa unaona?

Ubongo bado huendelea kuchakata yale uliyokuwa unaona kabla ya kufumba macho.

Inategemea mazingira uliyopo. Kwa mfano kama ni mchana na kunamwanga utaona mwanga hafifu au kama ulikuwa unauelekeo wa miali ya jua basi utaona wekundu fulani ambao kiukweli ni rangi ya damu yako inayopita kwenye blood vessels za jichoni. Kama ni gizani hutaona chochote bali ubongo itaendelea kutoa tafsiri ya unachofikiria au ulichokuwa unatizama kabla ya kufumba macho.

Macho yapo kazini lakini hakuna kinacchoingia kwenda kwenye ubongo kwa kupitia macho yako.
Asante sana kaka
Hakika nimejifunza vitu vingi sana
Karibu tena
 
Asante sana ubongo ni kitu muhimu mnoo ndio maana ukisikia mtu damu imevilia kwenye ubongo ndio baasi anaondoka
Sio lazima sana. Damu ikivilia kwenye ubongo inategemea ni sehemu gani ya ubongo imeathirika. Ubongo una pande mbili (Lobes).Kama damu imevilia upande wa kulia basi upande wote wa kulia wa muathirika utaparalyse. Kama ni upande wa kusho ni vivyo hivyo Upande wa kushoto utaparalyse.
Kwa mantiki hiyo Utasikia fulani amepatwa na kiharusi upande wa kulia/kushoto kutoka juu hadi chini. Lakini tena kuna wale wanaopata athari za kiungo/viungo fulani kutegemea ni Nerves gani zinazohudumia kiungo hicho zimeathirika labda kwa kukosa damu kutokana na mshipa unaopeleka damu huko kubinywa e.g. ugonjwa wa sciatica, hewa(oksijeni) e.g. Degedege au nerve kushambuliwa na virusi/bacteria e.g. Polio n.k.
 
Hapana, siwezi kuona vitu vilivyo mbele yangu kwa macho yaliyofungwa, lakini naweza kuona picha au mawazo katika akili yangu
 
Back
Top Bottom