Kuna kitu kinaitwa Blindsight yani kuona bila kujua kama unaona. Kuna watu ambao wana matatizo kwenye ubongo wao kiasi kwamba hawawezi kuona kitu chochote kile lakini ukiweka kitu mbele yao kama kuwatega na ukawaambia watembee, huwa wanajikuta wanakikwepa bila wao wenyewe kujua kwa nini wamekiwepa! Hii maana yake nini? Ubongo wa binadamu una mifumo miwili tofauti ya kupokea picha mfumo wa kwanza unakupa picha unayoiona sasa hivi, na mfumo wa pili ni subconscious radar inayolinda usalama wako bila wewe mwenyewe kujitambua.
Unapofumba macho yako na kuhisi kama bado unaona au unajua kabati lilipo ujue ni ule mfumo wako wa ndani wa usalama unaoendelea kufanya kazi kimya kimya hata unapokuwa umefumba macho.
Fikiria ukiwa umekaa kwenye chumba chenye ukuta mweupe usio na kitu chochote na kukiwa na ukimya kwa masaa mengi, baada ya muda lazima utaanza kusikia sauti au kuona vitu visivyokuwepo. Iko hivi Ubongo wa binadamu umezoea kupokea maelfu ya data kila sekunde kutoka kwenye milango ya fahamu, unapofumba macho bila kusinzia, unakuwa umekata ghafla usambazaji wa picha kwenda kwenye ubongo, ubongo una tabia ya kuchukia sana kukaa bure bila kazi! Ili kujaza lile giza na nafasi iliyo wazi lazima utaanza kutengeneza picha zake wenyewe. Kwa hiyo, zile rangi unazoziona ni hali ya ubongo kujiliwaza pale unapokaa bila kuwa na kazi yoyote ile ya kuichakata.
Hebu fanya hili jaribio sasa hivi nikiwa nakuambia. Fumba macho yako alafu ufikirie umetengewa nyama laini ya mbuzi iliyotoka kuchomwa sasa hivi ina ndimu ya kutosha na pilipili ya kuwasha pembeni. Je, hauoni picha yake kabisa kichwani kwako? Na sasa hivi pengine mate yameanza kukujaa mdomoni, sivyo? Sasa swali la kujiuliza hapa hiyo picha ya nyama umeiona wapi wakati macho yako yamefumba na mbele yako kuna giza?
Hapo ndio utajua kuwa binadamu ana the mind's eye. Ubongo una uwezo wa kuchora picha yenye rangi, moshi, na maumbo bila kutumia mwanga wa jua hata kidogo. Ukifumba macho sasa hivi na kuhisi bado unaona, hiyo inakuwa ni kwa sababu hiyo programu ya ndani ya uchakataji picha inakuwa bado ipo na inafanya kazi.