Hivi uzuri wa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ni upi ?

Waliowika sana na kuipa yanga mafanikio ni Shungu,Mkwasa na Mziray huyo Zahera ni Failure.
Usimsahau Tambwe Leya. Naona Yanga wanafikiri Zahera ana uwezo kama Tambwe Leya, wameuachia klabu, huku akifanya atakavyo!! Sijawahi kuona, wananchi wanamkadhi timu mkongongomani!! Hapo sio bure, ipo namna.
 
?????--------- Wee ni Nani? Kama ni mwanachama au shabiki wa yanga? Ok weee ni Simba siyo? NI kweli Mwalimu wa Yanga sio mwl. Wewe ndiye Mwl tosha. Kuwa kocha msaidizi wa nchi iliyo izidi nchi yako kisoka eti ajui. CHADEMA Kweli NI sawa na CCM
 
Hahahah mkuu muache apumzike! Ila umetembea nae kisawasawa,mana Zahera huwa anajidai kafundisha ulaya ila ukifatilia hivyo vitimu alivyofundisha ni vya ajabuajabu tu. Na kibaya zaidi anaowadanganya wameridhika kudanganywa hawahitaji kutafuta taarifa zaidi.
Ni kweli Zahera ni kocha mzuri na ana upekee wake,lakini unakuzwa kupita kawaida.
 
Uzuri wake ni upi ikiwa habebi makombe ?
 
Reactions: Tui
Kwanza acha upotoshaji Zahera hajafundisha Timu ya Dision 5 , Nilicho kufahanisha ni kwamba Zahera amefundisha Belgium na France tena kama kocha mkuu. Sasa kama izo timu hazipo katika izo nchi ningekua mpotoshaji kama wewe. Uka zungumzia amefundisha timu za amature nika kuuliza Afrika kunaligi ngapi za kulipwa? Wewe binafsi unamchukia Zahera ila bila kupepesa maneno CV na Utendaji wa Zahera ni wa kiwango chajuu kwa apa nchini hasakwa maendeleo ys Soka letu.
Yanga imepata kocha wa kiwango cha Uefa hakuna mpenzi wa Yanga ambaye alijua hafahamu mapungu ya timu lakin Zahera aliweza ku balance nakama si fitina za bongo Yanga ingekuwa bingwa.
Unajua nini kingetokea kwa Simba!! Uchebe angefukuzwa, Manara angefukuzwa, Mwekezaji ange kimbia, Wanachama wa Msimbazi wasinge elewa lolote kwa timu ya Bilion tatu na nusu kukosa ubingwa.
Sasa tusubiri tuone msimu huu tayari mmeshaingia mchecheto kwakua mnajua Zahera atafanya yake.
 
 
Huyu zaidi ya ukocha pia ni dalali na alimuuza Makambo kwa mafanikio mkubwa.
 
Reactions: Tui
Mikia fc washukuru sana tifua na ratiba zao kuwabeba ubingwa wangeusikia tu
 
Msingepangiwa kucheza mechi 12 nyumbani hata nafasi ya pili mngeisikia kwenye redio.Ushiriki wa viti maalum umewezekana kwa ufanisi wa Simba.
Timu ifikie robo fainali ya CAF ishindwe kushinda ligi rahisi kama ya Tanzania!!!. Simba wamewazidi pointi 7 na goal difference 62 ambazo ukichanganya 33 za Azam na 29 za Yanga ndio mnakuwa sawa.Tafuteni visingizio vingine hivi vya sasa ni fedheha.
 
Robo fainali matokeo mabaya..nyie mpira mmeanza kufuatilia lini
 
SIMBA wananunua timu pinzani mpaka wakina Kambuzi...unashinda CAF nyumbani "kimipango"nje maweee
 
Ligi ambayo Mavugo anashinda golden boot..kwa magoli kumi..be serious
 
Huu ndo msimu wa pili tumwache aanze ligi.pochetino ni kocha borana kuna makocha wengi bora ambao hawana vikombe.kuna wachezaji bora ambao hawana vikombe.ubora wa kocha ni namna ambayo anapanga kikosi chake na kudhibiti
Benchi la ufundi.
Kocha yeyote mzuri analeta vikombe , huyu wenu ameleta nini ? timu inacheza hovyo kabisa ! huwezi hata kudhani wanatumia fomesheni yoyote ila !
 
Kwa Tanzania zahera ni kocha bora,na kuhusu vikombe ni msimu huu ambapo inabidi tumjudge kwa hilo kulingana na hali aliyoikuta na ubora wa kikosi.
Mara nyingi makocha wanapenda kufanya kazi na aina fulani ya wachezaji ambao wanaingia kwenye mifumo yao,hata Pep hakupata kikombe msimu wa kwanza alivyofika uingereza kama nna kumbukumbu vizuri,ila kilichofatia baada ya kusajili wachezaji anaowataka kila mtu wa mpira anakijua.Tumpe muda tu Zahera,msimu huu ambao kapata anavyotaka tuone.
 
Halafu hata Zesco mwaka huu watafungwa sana maana wamewauza wachezaji wao wazuri akina Kambole na Winston Kalengo. Juzi kati wamefungwa na Zanaco FC. Walicheza chini ya kiwango sana. Zesco wamekuwa na mpira wa ovyo sana sasa hivi. Hivyo, siku za Lwandamina ndani ya Zesco FC zinahesabika.
 
Anafanya kazi mbili kwa pamoja, kufundisha mpira na kuwa msemaji wa timu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…