Hivi viongozi wa Tanzania wana sheria zao wenyewe zilizo tofauti na sie wengine?

Hivi viongozi wa Tanzania wana sheria zao wenyewe zilizo tofauti na sie wengine?

Tumeona Dodoma Mkurugenzi Mafuru akitunga Sheria ya kuchukuwa asilimia 70 ya Ardhi ya Mwenye hati sembuse hao kuendesha wrong site!!!!!
 
Kimsingi ni kukosekana kwa maadili ya uongozi maana japokuwa sheria ya usalama barabarani ilirekebishwa na kuwataja viongozi wengine kuwa kipaumbele barabarani lakini kiuhalisia ni kujikweza tu maana mtu kama ijp ni mlinzi wa usalama sasa anapowekwa kwenye mazingira ya kutojua kinachoendelea hata anapokuwa barabarani atawezaje ku assess hali ya usalama mitaani? Badala yake anasubiri taarifa za uongo anazoletewa na vijana wa doria na rpcs.
 

Mt 20:25-28 SUV​

Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
-------------------------------
Hii model ya uongozi ya Kristo ndiyo huwa litmus test yangu kwa viongozi aina zote hapa duniani. Kuanzia viongozi wa dini hadi wa siasa hadi wa mataasisi mbalimbali. Kiongozi yeyote kwangu asiyefuata hii model namuona tu lilevi kama walevi wengine. Na inashangaza sana kwamba nchi maskini ndio zinaongozwa na viongozi walevi tu wa madaraka.
 
Ndugu yangu...hivi unajua kuwa hata wewe ukiwa na dharura ya msingi kabisa ambayo ni explainable unaweza kupita njia hiyo...Kwa dharura let's me remind you that barabara Ina watumiaji wakuu wawili nao ni
1. Mtumiaji muhimu...
2. Mtumiaji maalumu....

Katika hayo makundi 2 jiulize wewe upo kwenye kundi Gani...?​
 
Back
Top Bottom