Hivi vitu ndio vilinifanya nigome kutoka Jiji la Dar es Salaam

nimekuja mbio kusoma comment yako nikidhani vijana wenzio wa mikoani watakuwa wamekupa likes nyingi.nimepigwa na butwaa kwa hali niliyoikuta
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nimeipenda paragraph ya mwisho
 
Mimi mwenyewe Niko Arusha lakini akili yangu Iko Dar es Salaam kibiashara #isaluteDaressalaam
 
nadhani vijana wa arusha hawajui kama hapa dar tuna zoo.

acha tuwasambazie taarifa.
View attachment 2370910
Arusha kuzuri ila vijana wa huko wanapoanza kulinganisha na kusema imeizidi dar hapo ndio wanapandisha watu nyongo
Dar yenyewe kwa dunian haijakamilika bado kuitwa jiji ndio ipitwe na ara πŸ˜ƒ
 
Dar imekuwa overrated kinyama

Sijui labda sababu nimezaliwa na kukulia Dar nimepazoea sana lakini sionagi uspesho wake
Mimi life limenipiga hapo dar baada ya kumaliza chuo nimepigiga for 5 consecutive years, ajira hakuna unaambiwa usichague kazi ila izo kazi zenyewe ambazo haupaswi kuchagua hazipo ukijimix kwenye kijiwe cha kuosha magari na wana unatolewa nje, ukisema utafute hata deiwaka tu za saidia fundi napo bila bila kulala njaa ni utaratibu wa kawaida kabisa yaani ule msoto msoto kweli stress, hauna hata hela ya kula, masimango ya watu, kudhalaulika, nilikonda mwili uneisha kabisa hapo hapo unafikiria matarajio waliokua nayo ndugu kwako ukimaliza chuo yaani hata demu aje uchi wa mnyama mashine haidindi ikafika hatua nikawa mpaka naongea peke angu barabarani nikaona sasa naelekea kuwa kichaa ikabidi nije huku kijijini kupata utulivu wa akili kidogo wakati nafikiria my next move sasa hizi shuhuda zinazotelewa hapa ni kama vile ukiwa dar fursa nje nje ndo nabaki kushangaa dar hii hii niliyoikimbia au kuna dar mbili hapa tanzania
 
Ukitaka ona maajabu...
Hadi leo Dodoma ndani ya KM 10 kutoka Kati ya Mji, viwanja bei yake sawa na Chamazi...

Dar huko Bunju hapashikiki na ni zaidi ya KM 35 toka Mjini...

Train ya SGR ikimalizika na nauli iwe fare, watu wengi wataishi Dar na kazi Dodoma, imradi tu Train iwahi fika Dodoma

Kuna watu wataona bora kila Ijumaa waondoke warudi Jtatu asbuhi, na hii itafanya Dodoma ishuke kimapato kwani bata zitaliwa Dsm

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hata Marais wote wanajengews nyumba Dsm

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Miaka mitano ushawahi kujaribu hata biashara ndogo ndogo? Ni kama umefocus zaidi kwenye ajira.

Sijui ni hustle gani unapitia ila kwa jinsi ulivyoandika ni kama umepitia magumu mengi kwa hilo pole sana. Ila turudi nyuma miaka mitano ni mingi lazima ungekuwa ushapata njia ya wapi unaelekea hata kama ungekuwa umeishia darasa la nne. Ngoja nikae kimya yawezekana ningekuwa kwenye position yako ningalikuwa na hali mbaya zaidi
 
Dar imekuwa overrated kinyama

Sijui labda sababu nimezaliwa na kukulia Dar nimepazoea sana lakini sionagi uspesho wake
Ukitaka kujua umuhimu wa dar hamia lindi πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…!

Wewe unaishi mjini kila kitu unapata ukihitaji unapachukulia poa poa, tembea mikoani...ishi!

10 years in Moro,
7 years in Moshi,
3 Months in Mbeya,
1 Week in Lindi,
1 Week in Dodoma,
3 Days in Babati,
3 Days in Arusha,

Hakuna mahali kama DSM
 
Mkuu acha tu niliyopitia nayajua mwenyewe, kipindi nipo mdogo nilikua nasikia watu wanajiua kwa stress, ugumu wa maisha and the likes sikuwahi kuwaelewa mpaka yaliponikuta., i faced really hell yaani nikiangalia nyuma hata sielewi nilisurvival vipi mpaka kufikia leo ingawa bado sina direction yoyote angalao kidogo nina utulivu wa akili.. kuna situation ambazo ni ngumu kuzielewa kama hujazipitia
 
Vijana wenzako wa kahama na njombe uko wanawekeza kwenye kilimo wananunua masemi na kufungua maduka kariakooo we uko busy kuzurula mjini kama una akili dar ni sehemu ya kufanya biashara ila kuaccumulate capital ni ngumu.

Dar ukiwa na million ni ngumu kufanya uwekezaji utakaokutoa kimaisha .

Ila baadhi ya mikoa million inaweza kukuzalia hata million 10 ndani ya mwaka mmoja

Ila yote kwa yote inategemea na akili yako na uwezo wako wa kuziona fursa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kila la kheri mkuu. Ila jaribu kufocus kwenye vitu vingine pia mkuu you never know unaweza pata sehemu ukawa comfortable zaidi huku ukijipatia kipato chako. Ajira zenyewe Masimango kibao
 
Kwa Nini wameenda kufungua maduka kariakoo.? Si wangeyafungulia hukohuko njombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…