Napenda sana kurejea nadharia za Mh Kashimba (mb)Mkuu ukiona hivyo basi ujue kuwa mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana kwakua haumruhusu mtu kuwa mbunifu bali unamfanya apate ajira tu ya kawaida.
Hali ni mbaya zaidi kwa miaka ya karibuni kwani wanafunzi wamekuwa wanakaririshwa tu ili kujibu mitihani na shule zifanye biashara.
Tunapaswa tubadili mitaala yetu ili iwajenge wanafunzi katika kuitumia elimu yao nje ya mfumo wa ajira za kawaida.
Nadhani kipimo tunachotumia kupema uwerevu bado sii sahihi kuna haja ya kufanya rejea na kutengeneza mazingira wezeshi na rafiki ili kuibua vipaji halisi
Tumeona wengi wameishia kwenye fani za uhandisi ,utabibu na maswala ya mawasiliano .. lakini hawana maajabu yeyote...
Huenda mfumo wa elimu hauwaruhusu kukuza/kuibua vipaji vyao.
Pia sifa wazipatazo wakati mwingine huwafanya kuwa malimbukeni ..hivyo hujikuta wamejitengenezea ulimwengu wao tofauti na uhalisia.
Maoni yangu: mitaala ya vyuo vya ufundi imekuwa na tija kuliko huu mfumo rasmi wa elimu ya nadharia ya kukariri madarasa mpaka vyuo vikuu