Hivi wataalam wa kilimo toka SUA wana impact gani! Mbona hawasikiki?

Swali zuri sanaaa!

Utakuta watu wengi waliotoka SUA ndio wanafanya kazi NSSF, PPF, Banks n.k

Sijui Shambani penye mazao na mifugo waende akina nani?

Ila nahisi ni serikali haijatengeneza mazingira wezeshi.
Iulize serikali yako.
 
Sua ime
SUA ilianza kutoa hao wataalamu tangu miaka mingapi iliyopita?
kua university toka 1984 baada ya kujitenga kutoka chuo kikuu cha dar es salaam,
Jiulize serikali imetoa kipaumbele kwa kuasi gani kwa chuo hiki? Kwanini walikuwa wanaoeleja ruzuku ndogo katika chuo hiki , ? Sababu hawakukipa kilimo kipaumbele kwa matendo bali kisiasa
 
Umeongea yote mkuu, wakulima ndio tatizo kuu na sio wataalam wala chuo chetu kikukuu pendwa cha Kilimo Sokoine
 
Swali zuri sanaaa!

Utakuta watu wengi waliotoka SUA ndio wanafanya kazi NSSF, PPF, Banks n.k

Sijui Shambani penye mazao na mifugo waende akina nani?

Ila nahisi ni serikali haijatengeneza mazingira wezeshi.
Sio kila mtu aliyesoma SUA kasoma mambo ya shamba tu so wanafanya kazi sehemu nyingi pia
 
Serikali imewekeza kiasi gani kwenye kilimo!?
Personally nimesoma SUA, kozi ya Animal science, kabla ya 2008 kozi hii ilikua inachukua miaka minne mpaka kuhitimu, lakini kwa sasa kozi hii inachua miaka mitatu lakini syllabus ni ile ile ya miaka minne. Tofauti ni kwamba mazoezi ya vitendo yamepungua.
Je! Ni kwanini serikali iliamua kupunguza mwaka mmoja katika kozi hii!? Possibly itakua ni ubanaji wa matumizi. Hii inaashilia kua Kilimo/ufugaji sio kipaumbele cha serikali.
Hivyo kabla ya kusema SUA hawana impact kwenye kilimo (which is not true), lazima uulize serikali ina commitment gani kwenye kilimo na iko tayari kwenda umbali gani katika kuimarisha sekta ya kilimo.

SUA wamesaidia sana wakulima kwa Ku-disseminate technilojia mbali mbali za kusaidia wakulima. MF.SUA wame-develop mbegu (hybrid) za matunda, SUA wametengeneza Chanjo za magonjwa ya kuku (Google prof. Philemon wambura kutoka Collage of veterinary and medical sciences), ukienda Department ya Animal science, aquaculture and Range science wamefanya kazi kubwa sana kwa wafugaji.
Wataalamu tupo lakini tunahitaji msaada mkubwa kutoka kwa serikali ili tulete impact kwenye sekta ya kilimo. Usipotusaidia ni wazi tutaenda kutafuta mkate katika maeneo mengine ambayo sio ya utaalamu wetu simply b'se Graduate wa SUA ni kiraka.
 
Sasa wataalam hawaajiriwi na serikali wakawatumikie Wakulima, unataka wafanyaje labda, waishije?
Kuna madaktari na mainjinia pia ambao hawafanyi walichosomea
 
Mkuu pitia kwenye hivi vyuo vya kati yaani kusoma ni kidogo sana mda mwingi ni practical tena mashambani tofauti na sua na vyuo vingine vikuu ambavyo wanafunzi wanalima kwenye projector
[emoji1] [emoji1] Hahaha eti wanalima kwenye projector.
Mkuu nimesoma SUA na wale watu wa kozi za kilimo walikuwa shamba kufanya practical. BTW mtu wa degree ni msimamizi/mtawala hivyo theory ni muhimu sana
 
Ukisema kilimo ni nyanja kubwa na haiwez kusimama kizembe na hasa kwa nchi kama Tanzania inayo kua ,na sua hawaboreshi kilimo bali kaz ya kuzalisha wataalam.
 
Mkuu! Nikifungua consultancy ya kilimo na mifugo sidhani kama raia watakuja. Na kama wakija sidhani kama wapo tayari kutoa pesa kwa ushauri pekee.
 
Chaa ajabu wengi unawakuta wanafanya kaZi bank!! Ushahidi ninao
Mkuu maisha popote, Kuna kozi inaitwa Agricultural Economics and Agribusiness ni uchumi kamili, sasa kama hakuna ajira za kuhudumia wakulima, na kuna za benki afanyaje?
 
Fani karibu zote zinaunganishwa na vyama vya wataalam. Lawyers, architects engineers, doctors. Chenu cha wataalamu wa kilimo ni kipi?
Kwanza lazima tutambue kua SUA inatoa taaluma tofauti tofauti ingawa zote zipo katika bracket kubwa la kilimo.
Mfano. Veterinarians wanachama chao pekee(Tanzania veterinarian Association), Animal scientists tupo kwenye taratibu za mwisho za kusajili chama chetu, Wildlife officers pamoja na wanachama (nimesahau jina), Agronomist, Crop production experts (Agriculture general and Horticulturists) na food science sina uhakika kama wanavyama ila wataalamu wa misitu wanacho chama.

Kwa hiyo sio rahisi kukapatia jibu la pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…