old is gold
mimi siwezi kuingia kwenye mkumbo wa kushabikia kisa nionekane najua,nimeangalia series zote mbili na season zake zote.
kila series ina mapungufu yake na kila moja ina ubora wake sema tu PB ilitoka kipindi hakujawahi kuwa na series kama ya aina ile,na MH ipo kwenye kipindi watu washaona kitu cha aina hii wanaigiza.
tunaipenda PB sababu ya memories,ipo kichwani..sababu tunakumbuka na binadamu tuna tabia ya kusifia vya zamani.
ingawa kwa upande wangu pia PB ni favourite kuliko MH....
characters hawawezi fanana,mfano mtu hapo juu anafananisha Rio na Tbeg...Rio kwenye MH kacheza kama dogo tu mtaalamu wa IT so issue za ubabe usitegemee,alichofunzwa ni kutumia tu bunduki na vitu vingine ila kazi yake kubwa mule ndani ni issue za mitambo.
halafu kumbuka pia Michael aliwachagua watu wake kuzingatia mahitaji yake,sawa..pia wale walikua kwenye gereza la watu wahalifu wakubwa so issue za wao kuwa hard lazima sababu ni wahalifu sugu,akina Rio wameokotwa tu mtaani sababu ni watu hawana cha kupoteza ndio maama hata akiua mende anaanza kulia.
lengo la proffesa ni kuteka na kubuy time waprint mzigo kwa kufanya negotiation...
mazingira mengine yameshaandaliwa miaka kadhaa nyuma huko
Sent using
Jamii Forums mobile app