Hivi wenye magari wote tukaamua Mei 4 tupaki magari, itakuwaje?

Hivi wenye magari wote tukaamua Mei 4 tupaki magari, itakuwaje?

Kaka hii nchi kuna watu Wana pesa.
Acha wale walionunua gari kwa mikopo
 
NI vyema wananchi mrudi kiendesha magari yenye ujazo mdogo km vitz IST passo Ractis nk..
Hayo maHarrier na Forester V8 DUALLIS Yafungieni kwa kitambo mpk hali itakapobadilika ya bei ya mafuta
 
utapaki mpaka lini mwamba?,ongeza bidii zaidi uongeze kipato ili ukabiliane na gharama za maisha.
 
Nimeshtuka sana kusikia eti kesho mafuta yanapanda tena bei hadi kufikia 3,400/= kwa lita kwa baadhi ya mikoa.

Hivi itakuwaje kama wenye magari wote watasusa na kupaki magari kesho. Au tuamue hapa hapa?


Wanatubeep, ...., mi nawapigia, nishaamua, napaki, kwani nini bhanaa, napakiii.., siwezi kuendelea ku-fund vita ambayo hainihusu..., Tanzanians should stop funding this WAR!!!, its not our WAR!!

Afrika na hasa Tanzania hii partivulary ni tabu sana na ubinafsi hakuna wanaotetea maslahi mapana ya wote, kila mtu ni individualist
 
Tutatembea kwa miguu. Kilomita 6 za kwenda kazini haziwezi kunishinda. Hii itatusaidia wengine kuanza kufanya mazoezi kwa lazima. Naamka alfajiri naanza kutembea mdogo mdogo ili nisifike kazini nanuka jasho.
Ndugu umoja ni nguvu. Serikali zikikosa mapato yatokanayo na mafuta watawaza vizuri. Sote tubanane kwa usafiri wa umma tuchelewe sote makazini serikali inunue staff bus kama kampuni ya cocacola tupande bure kwa vitambulisho hili litawanufaisha na wanafunzi pia. Tushikamane na mtoa mada.
 
Tatizo tulilonalo ni uongozi mbovu usiyo na maono nashangaa sana watu wanaojiita wachumi kumbe ni wachumia matumbo yao. Jiulize kupandisha dizel kiasi kile ni kuua thamani ya shilling na kuongeza mfumko wa bei mara dufu. Serikali ilitakiwa kuangalia umuhimu wa mafuta ya diesel kwa na madhala yake baada kuipandisha bei. Ukiangalia mazao mengi kutoka mashambani yanatengemea malori yanayotumia diesel mabasi ya abiria mjini mikoani na vijijini aslimia kubwa ni diesel. Je wachumi wetu wameliangalia hilo? Kama week tatu ama nne zilizopita tuliambiwa kuna mafuta ya kutosha kwa miezi saba, je hiyo stock imekwisha kwa week tatu?
 
Baada ya vita ya Uganda, Mwl Nyerere alitutangazia watanzania tufunge mikanda, najaribu kuwaza hivi aliwahi kuja kututangazia tena tufungue ila mikanda?
 
Umekurupuka dunia hii huwezi kukwepa gharama za mafuta hata kama haumiliki chombo cha usafiri
We paki Ila mi sipaki na hiyo hela ya kulipia mafuta unayo ikwepa utailipia kwenye kununua bidhaa na kupanda daladala/bodaboda
 
Inabidi tuwe na magari mengi ya umeme. Tesla ni ya umeme, kuna canter ya umeme, malori ya umeme tayari volvo ya umeme ipo, mabasi ya umeme yaje tayari uganda wanatengeneza kiira motors. Kiufupi magari ya umeme ndio suluhisho
Kabisa....hiyo ndio solution,viwanda vya magari vikianza kuzalisha magari ya umeme kwa wingi na kuuza kwa bei ambazo ni affordable automatic mafuta nayo yatashuka tu bei
 
Monasikia mrusi anauza mafuta kwa bei ya kutupwa shida nn kiagiza hayo mafuta
 
Muhasishaji ya kupandisha vitu hovyo hovyo anasemaje?
 
Watu tunalalamika maisha magumu LKn ukipita kumbi za strehë kila mtanzania ana pesa. Dah unajiona ni wwwe tu umebakia kupta pesa. We paki peke Yako tu.. wenzio wanaendelea kuweka heshima
 
Mimi hata wakauza mafuta 10k kwa lita siwezi kosa pesa ya kulipa, ninachosema ni kwamba, siwezi kufund vita ambayo hainihusu!!!!
Mtoa mada nimekuelewa mfano wako..inasikitisha Sana aisee na hizi bei za mafuta sio Siri inaumiza Sana nakumbuka wiki iliyopita nimepanda zangu private car ili kulinda maisha mengine ya home kwasababu nimepiga hesabu naenda mjini gari yangu alafu narudi na TSH 20,000 kitu ambacho hakuna haja ya kutumia gari yangu...

Bei ya mafuta kwangu imaekuwa changamoto Sana kwasababu nikitoka zangu chamazi Hadi kariakoo natumia Zaid ya TSH 18,000. - 20000 hii ni kwenda na kurud alafu unaenda kupiga Mishe unapata TSH 30,000 huku na parking unadaiwa.
Nitakuwa napaki Tu kama sielewi mchongo WA pesa umekaaje
 
Nimeshtuka sana kusikia eti kesho mafuta yanapanda tena bei hadi kufikia 3,400/= kwa lita kwa baadhi ya mikoa.

Hivi itakuwaje kama wenye magari wote watasusa na kupaki magari kesho. Au tuamue hapa hapa?


Wanatubeep, ...., mi nawapigia, nishaamua, napaki, kwani nini bhanaa, napakiii.., siwezi kuendelea ku-fund vita ambayo hainihusu..., Tanzanians should stop funding this WAR!!!, its not our WAR!!
Kwa umoja upi?
 
Back
Top Bottom