Malori aliyonunua Bakhressa hivi karibuni ni Mercedes-Benz Actros na Volvo FH12. Yote ni 6X4.
Safi kabisa ... niongezee tu bakhressa ananunua gari kabisa , mpya lakini standard version,
Unapotaka kununua malori (tractor units ) kuna vigezo vinazingatiwa ,hasa aina ya matumizi ,uzito utakao beba na njia utakazo pita ukisha jua hilo ndio unakwenda kununua horse kutokana na horse power .
Watu wengi biashara hii inawashinda kwa kuwa wananunua magari bila kudhingatia ugumu au urahisi wa njia au kazi watakazofanya , mf horse power 200-300 hutakiwi kuzidisha tani 18, gari standard kwa sasa ni 400-500hp, ingawa una weza uka opt kwenye extravagants 500-750Hp bands,
Nikirudi kwa mtoa mada ,kusema tu unataka lori kama la bakherssa unakuwa hauko specific ,na nina wasiwasi hata biashara yenyewe hujaijua vizuri, yeye anakwenda njia zozote kwa hiyo ameamua kununua 6x4 hii ni nzito lakini imara ,kwa kulifahamu hiyo anatumia trailer za Serin (Turkey) full air ride . kimsingi lori za bakhresa ni combination ya (horse) tractor unit, nzito na imara6x4 na trailer nyepesi sana ,but a very expensive combo kwa wanaoanza biashara ya lori.
kwa kuwa unaanza ni vema ukatumia 6x2 ambayo kwanza ni rahisi kununua , nyepesi, hivo utabeba mzigo mwingi n.k.. halafu tafuta trailer za imara.