Hiyo fedha unayoihangahikia na kuitolea macho kila ipo siku utagundua kuwa fedha si lolote, si chochote, ni suala la muda tu

Hiyo fedha unayoihangahikia na kuitolea macho kila ipo siku utagundua kuwa fedha si lolote, si chochote, ni suala la muda tu

Nimeona watu wenye fedha waliotumia zaidi ya milioni 100 kujitibu lakini fedha haikufua dafu wakafa.

Nimeona matajiri ambao kila mtu angetamani kuwa kama wao lakini hao Matajiri hawajawahi kupumzika hata wiki moja kuitafuta fedha.

Hii maana yake zile fedha zao mamilioni na mabilioni bado hayajaweza kuwapa jawabu la maisha. Wanaendelea kutafuta pesa na hawatapata jawabu na utulivu mpaka kifo kiwakute
Dalili za mtu aliyekata tamaa na maisha..pole sana!
 
na maskini wanakufa kila siku na kuacha wapendwa wao kwa kukosa pesa za matibabu....
kifo ni kwa kila mtu na kuwa na pesa ya matibabu haimaanishi kuwa utakuwa exempted na kifo.
Bob collymore the late safaricom Ceo , amefariki kwa ugnjwa wa kansa ilhali akiwa na pesa tele pamoja na access ya huduma bora kabisa za afya.
 
Sema kwa namna ulivyo andika hivyo unaonekana ni mtu ambaye:-

1. Umetanguliza sana dini mbele ( umaskini ndo huazia hapa)
2. Maneno ya vijiweni kwa sana( mipango isiyo na vichwa wala miguu)
Mimi nilikuwa napenda pesa haswa overtime maan kazi ya kuajiriwa ,nilikuwa nafanya mpaka jumapili ndani ya miaka miwili nimechoka ,tena niliumwa kabisa kwa kusaka pesa za overtime naforce ila wapi.

Nikaona ujinga bora nipumzike cha kufa bure ,kula bata maisha kuna ange huwezi kufika kama kufika utafika ila sio kwa kutumia nguvu.
 
Nimeona watu wenye fedha waliotumia zaidi ya milioni 100 kujitibu lakini fedha haikufua dafu wakafa.

Nimeona matajiri ambao kila mtu angetamani kuwa kama wao lakini hao Matajiri hawajawahi kupumzika hata wiki moja kuitafuta fedha.

Hii maana yake zile fedha zao mamilioni na mabilioni bado hayajaweza kuwapa jawabu la maisha. Wanaendelea kutafuta pesa na hawatapata jawabu na utulivu mpaka kifo kiwakute
Nmeona depression ndani yako, ukiendekeza utakufa kabla ya mda.
 
Fedha itafutwe ila kula maisha ni muhimu ,wanaopondea ndio kwanzo wapo chini ...Eeh bhana sikia kuna watu wanazichota tu hizo wala hawafanyi kazi zenu.

Tengeneza mirija ya pesa uwe na mda wa kumpuzika .
 
Mimi nilikuwa napenda pesa haswa overtime maan kazi ya kuajiriwa ,nilikuwa nafanya mpaka jumapili ndani ya miaka miwili nimechoka ,tena niliumwa kabisa kwa kusaka pesa za overtime naforce ila wapi.

Nikaona ujinga bora nipumzike cha kufa bure ,kula bata maisha kuna angel huwezi kufika kama kufika utafika ila sio kwa kutumia nguvu.
Ni kweli mkuu, hela zitafutwe wastani siyo kutumia mda mwingi sana, maana mwili, ubongo utachoka haraka hata kupelekea kupata maradhi kama ulivyo sema.

Ila kusema tusitafute hela kabisa, hapa inakua siyo kabisa,
 
Nimeona watu wenye fedha waliotumia zaidi ya milioni 100 kujitibu lakini fedha haikufua dafu wakafa.

Nimeona matajiri ambao kila mtu angetamani kuwa kama wao lakini hao Matajiri hawajawahi kupumzika hata wiki moja kuitafuta fedha.

Hii maana yake zile fedha zao mamilioni na mabilioni bado hayajaweza kuwapa jawabu la maisha. Wanaendelea kutafuta pesa na hawatapata jawabu na utulivu mpaka kifo kiwakute
Umasikini uliwahi kutibu ugonjwa gani? Au umasikini unaleta jawabu gani la maisha?
 
Pesa haizuiii kifo moja kwa moja ila ina uwezo wa kusogeza siku za kuishi mbele kidogo ama kutoa mtu katika hatari ya kufa.

Chukulia vifo vyote vinavyotokana na ukosefu wa madawa, na vifaa maalum vya matibabu na wataalam wabobezi, je yangekuwepo yoye hayo vifo si vingepungua.

Miaka ya nyuma wakina mama wajawazito walikua katika hatari kubwa sana ya kupoteza maisha wao na watoto wao kwasabab ya huduma hafifu lakini miaka hivi karibuni vifo vimepungua, havijapungua kimiujiza vimepungua Kwasababu kuna uwekezaji umefanyika kukabiliana na hizo hali na hapo unazungumzia pesa.

Kwa hiyo hoja yako ni dhaifu.

Wewe ukiumwa ugonjwa sawa na huyo bilionea we utarudishwa ukafie nyumbani baada ya siku 3 wakati bilionea akisogeza miezi kadhaa ndio utofauti wa pesa unapokuja😂

Tafuta pesa kijana.
 
Pesa ni kitu kinachorahisisha maisha, Ili mambo yako yafanyike Kwa urahisi Sasa hivi lazima uwe na pesa lakini siyo kwamba ni chombo cha kudumu cha kujipa furaha muda wote, sometimes ukiwa na pesa nyingi unaweza kukaa na kufikiria kuwa kumbe pesa siyo Kila kitu, hitimisho ni kuwa tutafute pesa Kwa njia nzuri Ili tuishi Kwa wepesi na amani.
 
kifo ni kwa kila mtu na kuwa na peaa ya matibabu haimaanishi kuwa utakuwa exempted na kifo.
Bob collymore the late safaricom Ceo , amefariki kwa ugnjwa wa kansa ilhali akiwa na pesa tele pamoja na access ya huduma bora kabisa za afya.
kansa haina tiba kiujumla, vipi kuhusu wanaokufa kwa marelia? ....na wenyewe tuwaache tu wafe kwasababu kifo ni lazima kwa kila mtu?....
 
kansa haina tiba kiujumla, vipi kuhusu wanaokufa kwa marelia? ....na wenyewe tuwaache tu wafe kwasababu kifo ni lazima kwa kila mtu?....
Kifo ni lazima Hilo kwanza unatakiwa ulijue. Kila ugonjwa una stages zake inategemea bahati ya mgonjwa. Hiyo kansa Kuna watu wanapona kabisa na hiyo maleria unayoiona rahisi kutibu Kuna watu inawaua wakiwa kwenye expensive Icu.
Maisha kiujumla ni kamari tu kama ilivyo betting.
 
Back
Top Bottom