Hizi abaya zinawatia uchizi wake zetu

Hizi abaya zinawatia uchizi wake zetu

Naogopa sana kusema mke wako anaweza akakuchiti kwa mtandio tu wa abaya 😭😭😭
Mwambie kwa kidiplomasia. Kuwa abaya atapewa na mwanaume mwingine asipokuwa na kauli / ubabe bilankutumia akili kwa hawa viumbe
 
Akiendekeza kutumia pesa nje ya uwezo wake kwa kumsikiliza mwanamke hatapata maendeleo kwenyeaisha yake.
Na siku akiyumba zaidi kiuchumi huyo mwanamke atamkimbia au atamsaliti.
Jitahidi uwe unafanya maandalizi ya hizo abaya mapema, mfano wiki, wiki mbili au hata mwezi kabla
 
Mwambie kwa kidiplomasia. Kuwa abaya atapewa na mwanaume mwingine asipokuwa na kauli / ubabe bilankutumia akili kwa hawa viumbe
Bora nilivyomwambia kwa njia hii maana jamaa anaonesha anampenda sana mke wake kwahiyo kuumia ni rahisi sana
 
Daaaahh mi mbona sijaelewa abaya ni fashion ya nguo mpyaa au mbona kama sijaelewa ivii , mwenye tupicha kdgo atufumbue macho kwa kweli......??
 
Abaya zaleta kizaa zaa Mjini, Lol
😂😂😂😂
 
Watu wengi wanapenda kuangalia matokeo, hawapendi kuangalia mchakato ulioleta matokeo.
 
Wakuu...wife wangu leo nimeamini ya kuwa ni kweli bado mtoto sana...asubuhi ya leo amegoma kwenda msikitini,amegoma kupika kisa abaya.

Iko hivi anadai abaya zilizopo ni za mwaka jana na zimepitwa na wakati,,nikamuuliza unataka kuiharibu bajeti niliyoipanga kwa muda mrefu...saivi utoe laki ya abaya ili uwaoneshe majirani kwa ajili ya siku moja tu?

Nikamwambia embu utavaa siku nyingine hii siku ni moja tu acha ipite.,,naona ndio kanuna..isitoshe unamaabaya karibia manne humu ndani acha leo mtoto avae wewe utavaa siku nyingine...lakini pia ushakuwa mtu mzimaa pressure ya nguo ya sikuu kuu unaitoa wapi au unataka tutibuane saizi.

Ikumbukwe leo tumeamka chalii wetu anajiskia vibaya mno...nikamchukua yeye na mtoto hao kwenye boda tukaelekea hospital...pale imekata vipimo,dawa...usafiri kama 50000 hivi.

Wakuu nimempotezea huyu kiumbe ...nimeenda africana nikanunua jogoo nikapika mwenyewe na pilau...nimeona bado kanuna hadi saivi..nimesaidiana na wana tumetoa kitu maisha yameendelea nasubiria usiku sijui atanipa...haya bhana kataa ndoa wanazidi kupata point tatu muhimu.
Ni wajibu wako kumnunulia. We si ndo mme wake!?
 
Naomba picha ya "abaya" nami niijue maana hata siijui ni kitu Gani, ushamba huu jamani🤣
 
Wanawake wangekua wasikivu kama AI maisha yangekua rahisi
 
Back
Top Bottom