#COVID19 Hizi chanjo za Corona zinaenda kuondoa herd immunity tuliyoipata nchini

Nyie ndiyo mlimdanganya dikteta Magufuli kuwa papai lina corona!
Teh teh teh teh...🀣🀣🀣....we jamaa bhana...haaa haaa..πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sasa kwa vipi herd immunity inapungua hapo?......How Vaccine affect infectivity & fatality of infectious disease?
Unaliza swali ambalo majibu yake unayapata kama unajua vizuri herd immunity.
 
K
Kaka samahani ni dhahiri kabisa, kile unacholeta hapa "chanjo" na "herd immunitY" hujaelewa bado misingi yake.

Kila chanjo (tangu mwanzo wa mfumo huo) inaharakisha jibu la mfumo wa kia mwilini. Haina uwezo wa kuubadilisha bali inaharakishi uwezo wake. Hali hiyo ni msingi wa chanjo zote, hata zile ulizopokea tayari ulipokuwa mtoto mdogo.
Je, tuko pamoja au la?

Kila chanjo si ya asilimia 100. Kila chanjo huwa na athiri mbaya kwa sehemu ndogo sana ya hao waliochanjwa. Hata chanjo zote ulizopokea tayari.
Je, tuko pamoja au la?

Kila chanjo, hata hizo ulizopokea, ina asilimia ndogo ambako haizuii ugonjwa husika. Lakini inapunguza SAANAAA idadi ya maambukizi. Bila matokeo hayo jinsi yalivyo watoto wengi zaidi hapa nchini yangekufa mapema.
Je, tuko pamoja au la?

Nimekuuliza maswali matatu. Ukijibu ndiyo, tafadhali ueleze wapi tofauti na chanjo ya COVID.
Usipokubali, tafadhali ujieleze kwa kutaja sababu za kitaalamu na marejeo.
 
mta
mtalaam huyu hapa.mie sijamwelewa kwa kweli

Huyu daktaru Swai ana maelezo mzuri na ushauri mzuri. Tumfuate.
Isipokuwa kuhusu chanjo elimu yake si ya kisasa.
Tekinolojia imebadilika sana.

1. ni kweli chanjo hizo za Covid hazikuchunguliwa jinsi ilivyo kuwa kawaida zamani.

2. Lakini nchi zilizothibitisha na kukubali chanjo hizo zilipima matokeo ziliona matokeo yanafaa ni nzuri yakipunguza maambukizi bila kuleta madhara (mbali na madhara ya kawaida kwa kila chanjo).

3. Chanjo za Covid zinaonekana kuokoa maisha kuliko kuharibu
 
Jaribio la Herd Immunity lilifail, kwani wimbi la tatu limethibitisha hayo, baada ya jambo hilo kuonekana kugonga mwamba, chanjo haikwepeki.
 
Sidhani kwamba tunakubaliana.
Ni kweli kwamba watu wachache waliopata chanjo wanaweza kuambukizwa na virusi (si korona pekee, ni kweli pia kwa magonjwa mengine).
LAKINI wengi wanalindwa.
Menginevyo uliandika pale juu
"Wachunguzi wanasema chimbuko la inayoitwa kwa kiingereza VARIANTS ni matokeo ya chanjo." -
Nilikuomba juu utuonyeshe ukweli wake.
Hebu tuambie: Mchunguzi gani?? Lini?? Wapi??? Taja chanzo!!!
(sidhani utaweza)
 
Pumba tupu
 
Una taaluma yoyote ya Afya au ndio ukishakuwa na bundle, smartphone na vidole, umeshajua kila kitu.

Umeshawahi kujiuliza kwanini daktari mahakamani anahojiwa na watu ambao hawajawahi kushika hata themomita?

Na kwa nini ushahidi wake unachukuliwa kama ushauri tu, sio neno la mwisho?

Tumia akili yako vizuri. Kama huna sema nikuazime.
 
Wewe ni mpotoshaji na siku zote wapotoshaji wanachukua kipande cha taarifa ndiyo wanakitumia kuhadaa watu.

Mbona hujatumia takwimu za Ulaya na Marekani namna wanavyoanza kurudi kwenye maisha ya kawaida baada ya kuchanja 40% tu ya population zao?
Hoja yako ni nini?

Kwanza huwezi kuchukua takwimu za Ulaya kwa sababu wako kwenye lockdown kwa muda mrefu na historia inaonyesha wanapoingia kwenye lockdown hata maambukizo hupungua sana lakini wakiondoka kwenye lockdown, maambukizi huanza kuongezeka.

Ulaya wamepata/wanapata chanjo wakati wako kwenye lockdown na kwa mantiki hii huwezi kutumia takwimu hizo kujua ukweli. Tusubiri mpaka mwezi wa kumi ndipo tutajua kama chanjo imefanya kazi kwa nchi za Ulaya baada ya kuanza kuondoa lockdown.
 
Ninachosikitika ni kuwa hizi chanjo ambazo baadhi ya watu watazipa nchi zitaenda kuua herd immunity ambayo watanzania wengi kama sio wote nchini tulikuwa tumeipata kwa muda wa takribani miaka miwili.
Unafahamu Herd Immunity ni nini?!

Na kama unafahamu, unaweza kueleza hiyo Herd Immunity mliipata kwa mazingira yapi?
 
Umeshawahi kujiuliza kwanini daktari mahakamani anahojiwa na watu ambao hawajawahi kushika hata themomita?

Na kwa nini ushahidi wake unachukuliwa kama ushauri tu, sio neno la mwisho?

Tumia akili yako vizuri. Kama huna sema nikuazime.
JUHA IN THE MAKING...

What a stupid argument....

Ulishawahi kusikia hao watu wasiowahi kushika thermometer waki-argue AGAINST taarifa za wataalamu?!

Ulishajaribu kujiuliza ni kwanini hata huko mahakamani ikionekana mtuhumiwa ana matatizo ya akili kwa mfano, hakimu ataamuru apelekwe hospitali akachunguzwe na watalaamu?!

Sasa majibu ya kitaalamu yakishatoka, unatarajia hakimu atapingana na hayo majibu?!
 
Yaani unaandika utumbo mpana mtupu na unatujazia samadi tu hapa!

Jibu hoja wewe mkemia uchwara!! Acha kuweweseka kama panya magawa!

Je, ukidungwa chanjo huwezi kuambukizwa corona? HAPANA, UNAWEZA KUAMBUKIZWA.

Je, ukidungwa chanjo huwezi kuambukiza wengine? HAPANA, UNAWEZA KUAMBUKIZA WENGINE!

Je, ukidungwa chanjo unaweza kuacha kuvaa mabarakoa? HAPANA, ENDELEA KUVAA MABARAKOA.

Mweeh [emoji23][emoji23][emoji23] sasa hiyo ni chanjo kweli au tunataniana tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…