#COVID19 Hizi dawa za COVID-19 ni siasa au tuna malengo gani? SUA hiki kitu gani?

#COVID19 Hizi dawa za COVID-19 ni siasa au tuna malengo gani? SUA hiki kitu gani?

Kama ukinunua pharmacy peleka pale halafu waambie wakupe form ya TMDA ujaze malalamiko au pakua app yao au website yao TMDA utakuta form ya malalamiko utajaza.

Hii husaidia kufanya follow up ya dawa pia kuzuia madhara zaidi kwa wengine ikiwemo kuzuia hiyo dawa isiingie kwenye mzunguko wa matumizi ya kawaida.
Mbona mnakuwa kama nyumbu jamani. Ujazie utapeli fomu? Hawa wanakula fedha ya wajinga. Mnadhani mambo ni rahisi namna hiyo!
 
Kwa wasiwasi wangu, koo lilipokwaruza tu, nikajua dalili hizo. Hapa nilipo niko hoi kwa kuharisha usiku kucha. Ni uchafu gani tunauziwa na taasisi za serikali? Watu wa SUA bado munacheza na afya zetu kama enzi iliyopita?

Ni kweli hiki ndo kiwango cha utaalamu wa chuo kikuu? Na hapa ni baada ya kupigwa kichupa kingine cha chuo kikuu cha Dar ambacho chenyewe kinanukia mchai-chai. Sijui Muhimbili wana mizizi gani! Mutatuua!

Hili chupa ubora pekee ni kuandikwa kwa kiingereza; High quality. Sijui ni quality ya kitu gani? Labda wanaigiza mambo ya waziri wa afya na nyungu za Muhimbili.
 
Mbona mnakuwa kama nyumbu jamani. Ujazie utapeli fomu? Hawa wanakula fedha ya wajinga. Mnadhani mambo ni rahisi namna hiyo!
Hizo dawa zimekuwa registered na Mamlaka ya udhibiti wa dawa za binadamu, hizo form na TMDA ni kwa ajili ya kutoa feedback ya side effects za dawa.

Kama amenunua sehemu official, apeleke na ajaze malalamiko, sio atarudishwa pesa Ila kwa ajili ya feedback ya kuweza kusaidia wengine wasipate madhara.

I hope next time hautachangia kwa lugha za dharau.
 
Haki mtu ukiwa tapeli Bongo hufi njaa. Wajinga wengi sana. Mtu anauziwa maji tena pengine machafu anaambiwa ni dawa ya COVID!
Bora hata maji, kinyesi cha wanyama pia inawezekana. Utapeli uko kila sehemu. Angalia utapeli bungeni. Utapeli serikalini. Sasa utapeli vyuo vikuu!
 
Hizi dawa huwa zinakuwepo Hospitali au ni madukani? Kama zinatibu mbona madaktari hawawandikii Wagonjwa waliolazwa kwenye wodi?
Za kuambiwa changanya na zako. Jali afya yako. Chukua tahadhari zote za kujikinga na covid 19.
 
Bila Katiba Mpyaa Ujinga kama huu Hauta isha...
Sasa ukinihakikishia kwamba katiba mpya itazuia wajinga hawa, nitaunga mkono, lakini usijekuta ni hawa wajinga ndo watasimamia mchakato wa katiba mpya! Si unajua huko jalalani?
 
SUA ni chuo cha kilimo brother mengine mchanganyage na zenu kabla ya kuyachukulia hatua. Pole sana kwa kupoteza kizibo.😂😂😂
 
Hizo dawa zimekuwa registered na Mamlaka ya udhibiti wa dawa za binadamu, hizo form na TMDA ni kwa ajili ya kutoa feedback ya side effects za dawa.

Kama amenunua sehemu official, apeleke na ajaze malalamiko, sio atarudishwa pesa Ila kwa ajili ya feedback ya kuweza kusaidia wengine wasipate madhara.

I hope next time hautachangia kwa lugha za dharau.
Mkuu samahani kama nimekukwaza. Hili wanalofanya ni utapeli. Hakuna dawa hapo. Ni wajanja wanakula fedha ya watu. Nakuapia niamini, sina nia mbaya. Nasikitika jinsi watu wanavyopigwa kidogo walichonacho bila huruma. Hata huko kwenye mamlaka kama TMDA usikuamini. Ohoo dear desperation makes people do unbelievable things!
 
Haya madude yote unayo dukani au umeyabugia? Mengine kama vile kachumbali! Ni hatari kwa figo zako.
Hayo madude nilikuwa napokea picha mbali mbali kwenye magroup ya whatsapp kutoka kwa wataalamu walioibuka kama uyoga kupambana na kovidi
 
Hivi waziri wa afya ni 'Dr' by profesional au ni PhD ya ustawi wa jamii?
Maana naye kabla alituaminisha kutumia hizi kachumbali na chachandu lakini yuleyule kwa sasa anahamasisha masks na chanjo na social distancing. Sasa najiuliza mtu mmoja anawezaje kuwa na misimamo tofauti kwenye suala moja katika kipindi kisichozidi miezi hata 6?
Nina mashaka kama kweli hawa watu wako serious na maisha yetu
 
Wengine wote hawa tuwaonee huruma kwa ufahamu wao. Tatizo ni hawa wa SUA na UD. Watu kama hawa ni pumbav kabisa! Elimu gani wanayotuonesha nchini kama wanatuletea mizizi na majani ya hovyo hovyo kiasi hiki?
Walikuwa wanaenda na Dira ya Serikali ya awamu ya tano, elimu zetu zimeshamezwa na wanasiasa ndio maana Magufuli aliweza kutoa kauli zenye utata katika vita dhidi ya kovidi na wataalamu waliobobea katika maeneo hayo walikuwa wanaunga mkono na kumpigia makofi bila kuchallenge hata kidogo msimamo wake !
waziri wa afya.jpg
 
Kimeumanaaaaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbona hilo jina kama sumu ya kuulia magugu shambani? ni bora tungetoa fomula tuwaachie watu watengeneze nyungu zao nyumbani......wekeni ingredients watu watengeneze wenyewe.
 
Back
Top Bottom