#COVID19 Hizi dawa za COVID-19 ni siasa au tuna malengo gani? SUA hiki kitu gani?

#COVID19 Hizi dawa za COVID-19 ni siasa au tuna malengo gani? SUA hiki kitu gani?

Kuna magonjwa yanayotusumbua Afrika lakini Ulaya hayapo. Kwa mfano, ugonjwa wa 'sleeping sickness' unaosababishwa na mbung'o hauna chanjo na ukichelewa tiba mara nyingi unaua. Mpaka sasa hivi hauna chanjo na mashirika ya madawa ya nchi za magharibi hawana habari nao kwa sababu hauna tija kwao. Taasisi pekee inalogharamia utafiti wa chanjo za ugonjwa huu ni la Bill na Melinda Gates. Kwa nini hao wakina Nimr hawajikiti kwenye kutafuta chanjo ya ugonjwa huu badala ya kuhangaika na dawa za kimaghumashi? Au na yenyewe tunangoja mabeberu watuonee huruma watutafutie chanjo?
Au chanjo dhidi ya sumu za nyoka ambao wana ua sana ndugu zetu huko vijijini?

Tunasikitisha sana.

Amandla...
 
Kwa wasiwasi wangu, koo lilipokwaruza tu, nikajua dalili hizo. Hapa nilipo niko hoi kwa kuharisha usiku kucha. Ni uchafu gani tunauziwa na taasisi za serikali? Watu wa SUA bado munacheza na afya zetu kama enzi iliyopita?

Ni kweli hiki ndo kiwango cha utaalamu wa chuo kikuu? Na hapa ni baada ya kupigwa kichupa kingine cha chuo kikuu cha Dar ambacho chenyewe kinanukia mchai-chai. Sijui Muhimbili wana mizizi gani! Mutatuua!

Hii dawa ni kama RUNGU, inaua wadudu wanaoruka na wanaotambaa!
 
Kwa wasiwasi wangu, koo lilipokwaruza tu, nikajua dalili hizo. Hapa nilipo niko hoi kwa kuharisha usiku kucha. Ni uchafu gani tunauziwa na taasisi za serikali? Watu wa SUA bado munacheza na afya zetu kama enzi iliyopita?

Ni kweli hiki ndo kiwango cha utaalamu wa chuo kikuu? Na hapa ni baada ya kupigwa kichupa kingine cha chuo kikuu cha Dar ambacho chenyewe kinanukia mchai-chai. Sijui Muhimbili wana mizizi gani! Mutatuua!

Wanataka tufe
 
Mizaha ipi zaidi ya kutukana mamlaka za kisayansi ambazo ni za rufaa..kwa msaada km kweli ungekuwa unataka kujua namna zinazofanya kazi ungehoji juu ya reserch ya mimea iliyotumika km kwelu inauwezo wa kukabiliana na jambo hilo??mfano unapoitaja Sua unazungumzia mmea uliofanyiwa tafiti zaidi ya miaka 12 unaitwa liyungi(syanadenium glaunces pax) ingia google uone kazi zake kisayansi kwa tafiti kushirikiana na hao wazungu...wee unazungusha kanga km mwanamke wa kidigo watu wanatumia elimu zao
Nimekuuliza maswali mawili ambayo ni very basic and fundamental katika sayansi ya madawa na hujayajibu hadi sasa hivi:

1.Hizi dawa zimejaribiwa wapi,lini na mafanikio yake yalikuwa ni asilimia ngapi?

2.Hizi dawa zina specific ingredients gani kwa ajili ya ku-attack antigens gani na katika level gani?

Kushindwa kwako kuyajibu haya maswali inathibitisha kuwa wewe ndiye mwanamke wa kidigo anaezungusha khanga.Halafu hizi unazoziita ni mamlaka za dawa ni mizaa mitupu kama hazina majibu ya hayo maswali yangu mawili hapo juu ambayo ni very basic katika sayansi ya madawa.
 
Mkuu behaviorist naomba nikupinge kidogo. Iko hivi . mimea hutengeneza secondary metabolites kwa Kiwango na composition kinachotofautiana kati ya mmea na mmea. Baadhi ya hizo metabolites ni flavonoids, tarpenoids, phenolics, plant sterols, saponini , alkaloids etc. Kiwango cha hizi metabolites ndizo hufanya mimea fulani kuwa na uwezo wa kutumika kama tiba kwani secondary plant metabolites zimejaribiwa kwenye maabara na kuonyesha uwezo kama antioxidants, some as antiviral, anticancer, antiglycemic ,antibacterial etc. Kwaiyo sio sahihi kubeza hizi anti covid preparation kwani hata zile zitolewazo mahospitalini kutibu kovid hazimuui virus bali ni supportive therapy.
Mkuu nimeuliza maswali mawili ambayo ni very basic and fundamental katika sayansi ya madawa na hayajajibiwa hadi sasa hivi:

1.Hizi dawa zimejaribiwa wapi,lini na mafanikio yake yalikuwa ni asilimia ngapi?

2.Hizi dawa zina specific ingredients gani kwa ajili ya ku-attack antigens gani na katika level ipi?
 
Kama ukinunua pharmacy peleka pale halafu waambie wakupe form ya TMDA ujaze malalamiko au pakua app yao au website yao TMDA utakuta form ya malalamiko utajaza.

Hii husaidia kufanya follow up ya dawa pia kuzuia madhara zaidi kwa wengine ikiwemo kuzuia hiyo dawa isiingie kwenye mzunguko wa matumizi ya kawaida.
Sawa wazo nzuri.maana Kama Ina madhara isiwadhuru wengine
 
Yale machupa ya maji yanayookotwa njiani ndiyo yanatumika kujaza huo urojo Mkuu
 
Nimekuuliza maswali mawili ambayo ni very basic and fundamental katika sayansi ya madawa na hujayajibu hadi sasa hivi:

1.Hizi dawa zimejaribiwa wapi,lini na mafanikio yake yalikuwa ni asilimia ngapi?

2.Hizi dawa zina specific ingredients gani kwa ajili ya ku-attack antigens gani na katika level gani?

Kushindwa kwako kuyajibu haya maswali inathibitisha kuwa wewe ndiye mwanamke wa kidigo anaezungusha khanga.Halafu hizi unazoziita ni mamlaka za dawa ni mizaa mitupu kama hazina majibu ya hayo maswali yangu mawili hapo juu ambayo ni very basic katika sayansi ya madawa.
Kama ungekuwa umenunua hiyo dawa ungeona hizo specific agent zenye kupambana na hilo tatizo tena zimeandikwa kiswahili.pili unasema imefanyiwa majaribio wapi...haa haa hivi hizi chanjo zimefanyiwa majaribio wapi kabla ya kuanza kudungwa watu..walalamishi wa nchi hii wazuri kwenye kupinga vyao na wepesi kushadadia vya kigeni kwa hoja ile ile anayoipinga...
Soma hivyo viambata vilivyoandikwa kisha fanya reserch hata kwa google..kisha uje domo la kupinga sio kulalama tu
 
Dawa zote huwa na side effects ambazo wakati mwingine ni severe kwa baadhi ya watu kama kuganda damu kwenye ubongo. Wewe kuharisha tu imekuwa noma. Jee ungeganda ubongo kwa kutumia dawa za hao wazungu ingalikuwaje? Kwa taarifa yako hiyo dawa ya SUA iliua virusi vyote vya covid 19 kwenye panya 1,000 waliokuwa infected na COVID 19. Haya, na wewe si ulipona hiyo covid 19 baada ya kuhara kama bata? SUA ni miamba ya dunia. Wanatumia panya kufanya diagnosis ya covid 19, tuberculosis na AIDS. Wanatibu covid 19 kwa kutumia dawa ya panya. Si wa mchezo. WHO haitaki kuwatambua kwa sababu ni Waafrika.
Safi kabisa maelezo yameshiba
 
Wengine wote hawa tuwaonee huruma kwa ufahamu wao. Tatizo ni hawa wa SUA na UD. Watu kama hawa ni pumbav kabisa! Elimu gani wanayotuonesha nchini kama wanatuletea mizizi na majani ya hovyo hovyo kiasi hiki?
Majani ya ovyo yametafitiwa zaidi ya miaka 12 ovyo ni majani au wewe kijana unayebalegh muda huu..balance shobo kidogo
 
Kwa mujibu wa sheria ya sheria ya Tiba asili na Tiba mbadala namba 23 ya 2002 maabara inayotumika kupima dawa kabla ya kusajiliwa na Baraza la Tiba asili pale wizara ya afya ni maabara ya mkemia mkuu wa serikali.Na dawa asili hupimwa kwa muongozo wa Who.sasa mnapokosoa vyema pia mkaheshimu hizi jitihada chache za Watanzania wenzenu..Hiyo TFDA unayosema ilishavunjwa toka zama za mwendazake
Mkuu, sawa hizo sheria wengine hatuzijui. Ila kitendo cha kuruhusu hizo concoctions kutambulika kama sawa za Cov 19 ni kuwatapeli wananchi na ni criminals act.
 
Mkuu behaviorist naomba nikupinge kidogo. Iko hivi . mimea hutengeneza secondary metabolites kwa Kiwango na composition kinachotofautiana kati ya mmea na mmea. Baadhi ya hizo metabolites ni flavonoids, tarpenoids, phenolics, plant sterols, saponini , alkaloids etc. Kiwango cha hizi metabolites ndizo hufanya mimea fulani kuwa na uwezo wa kutumika kama tiba kwani secondary plant metabolites zimejaribiwa kwenye maabara na kuonyesha uwezo kama antioxidants, some as antiviral, anticancer, antiglycemic ,antibacterial etc. Kwaiyo sio sahihi kubeza hizi anti covid preparation kwani hata zile zitolewazo mahospitalini kutibu kovid hazimuui virus bali ni supportive therapy.
We unatafuta sifa tu ya kutaja majina hayo. Una maana miezi mitatu ilitosha kufanya majaribio na kujua mumea huu na ule unaweza kupambana na COVID? Tusipende kuzubaisha watu kwa vijineno vya miaka mingi iliyopita kutetea uzembe. Waganga hujitetea kwamba wameoteshwa, hawa wa vyuo vikuu walioteshwa pia? Rubbish!
 
Majani ya ovyo yametafitiwa zaidi ya miaka 12 ovyo ni majani au wewe kijana unayebalegh muda huu..balance shobo kidogo
Rubbish! Miaka 12 corona ilikuwepo? Mbona unapayuka kuendelea kupotosha watu. Elimu gani hii?

Kama unayafahamu sana kuliko sisi, hebu tueleze hizo kachumbali kama kweli zinatibu corona kwa kiasi gani?
 
Ni

Ushamba wenu tu , kama dawa za kawaida tu zina reaction na wameeleza kabisa unaweza kutapika kuhalisha na mengineyo sasa iweje hizo zenu za kiswahili?
Kwa hiyo ukiharisha ndo dawa inakolea? Wewe umeharisha mara ngapi leo?
 
Kama ungekuwa umenunua hiyo dawa ungeona hizo specific agent zenye kupambana na hilo tatizo tena zimeandikwa kiswahili.
Dawa hizi hazina specific ingridients for the specific antigens.
pili unasema imefanyiwa majaribio wapi...haa haa hivi hizi chanjo zimefanyiwa majaribio wapi kabla ya kuanza kudungwa watu..walalamishi wa nchi hii wazuri kwenye kupinga vyao na wepesi kushadadia vya kigeni kwa hoja ile ile anayoipinga...
Soma hivyo viambata vilivyoandikwa kisha fanya reserch hata kwa google..kisha uje domo la kupinga sio kulalama tu
Chanjo zote zimefanyiwa majaribio na kila moja inajulikana efficacy yake kama jedwali linavyoonyesha hapo chini.Ulivyocheka hapo juu ni kwamba umejicheka wewe mwenyewe kwa ujinga wako wa kutokufuatilia haya mambo.
imagee12.png

Souces:Covid: What do we know about China's coronavirus vaccines?
 
Hivi wewe na mkemia nani anayejua sayansi??hizo dawa za vyuo zote zimepita kwake ..unataka sayansi gani??unajua procedure za kupima japo dawa moja tu inavyofanyika au kasuku tu...kubali watu walijitoa kwa ajili ya kusaidia jamii na watu wamenufaika na hizo products punguza wivu wa baleh
Naona kila meseji unang'ang'ania mkemia mkuu. Umeona wapi kwamba aliruhusu? Umeona wapi kwamba TBS aliruhusu? Umeona wapi kwamba TMDA aliruhusu. Au hata hujui mamlaka husika? Rubbish!
Watu kama wewe ndo munalishwa haja kubwa na matapeli kama hawa.
 
Kwa wasiwasi wangu, koo lilipokwaruza tu, nikajua dalili hizo. Hapa nilipo niko hoi kwa kuharisha usiku kucha. Ni uchafu gani tunauziwa na taasisi za serikali? Watu wa SUA bado munacheza na afya zetu kama enzi iliyopita?

Ni kweli hiki ndo kiwango cha utaalamu wa chuo kikuu? Na hapa ni baada ya kupigwa kichupa kingine cha chuo kikuu cha Dar ambacho chenyewe kinanukia mchai-chai. Sijui Muhimbili wana mizizi gani! Mutatuua!

Mkuu hii dawa ya SUA binafsi nimeishuudia imewasaidia wengi sana mimi mwenye ni kiwa na mafua au kikohozi nikitumia mafua yanakata fasta nadhani labda utakuwa na shida nyingine au uliifungua ukaiacha wazi.
 
Back
Top Bottom