#COVID19 Hizi dawa za COVID-19 ni siasa au tuna malengo gani? SUA hiki kitu gani?

Kuna magonjwa yanayotusumbua Afrika lakini Ulaya hayapo. Kwa mfano, ugonjwa wa 'sleeping sickness' unaosababishwa na mbung'o hauna chanjo na ukichelewa tiba mara nyingi unaua. Mpaka sasa hivi hauna chanjo na mashirika ya madawa ya nchi za magharibi hawana habari nao kwa sababu hauna tija kwao. Taasisi pekee inalogharamia utafiti wa chanjo za ugonjwa huu ni la Bill na Melinda Gates. Kwa nini hao wakina Nimr hawajikiti kwenye kutafuta chanjo ya ugonjwa huu badala ya kuhangaika na dawa za kimaghumashi? Au na yenyewe tunangoja mabeberu watuonee huruma watutafutie chanjo?
Au chanjo dhidi ya sumu za nyoka ambao wana ua sana ndugu zetu huko vijijini?

Tunasikitisha sana.

Amandla...
 
Hii dawa ni kama RUNGU, inaua wadudu wanaoruka na wanaotambaa!
 
Wanataka tufe
 
Nimekuuliza maswali mawili ambayo ni very basic and fundamental katika sayansi ya madawa na hujayajibu hadi sasa hivi:

1.Hizi dawa zimejaribiwa wapi,lini na mafanikio yake yalikuwa ni asilimia ngapi?

2.Hizi dawa zina specific ingredients gani kwa ajili ya ku-attack antigens gani na katika level gani?

Kushindwa kwako kuyajibu haya maswali inathibitisha kuwa wewe ndiye mwanamke wa kidigo anaezungusha khanga.Halafu hizi unazoziita ni mamlaka za dawa ni mizaa mitupu kama hazina majibu ya hayo maswali yangu mawili hapo juu ambayo ni very basic katika sayansi ya madawa.
 
Mkuu nimeuliza maswali mawili ambayo ni very basic and fundamental katika sayansi ya madawa na hayajajibiwa hadi sasa hivi:

1.Hizi dawa zimejaribiwa wapi,lini na mafanikio yake yalikuwa ni asilimia ngapi?

2.Hizi dawa zina specific ingredients gani kwa ajili ya ku-attack antigens gani na katika level ipi?
 
Sawa wazo nzuri.maana Kama Ina madhara isiwadhuru wengine
 
Yale machupa ya maji yanayookotwa njiani ndiyo yanatumika kujaza huo urojo Mkuu
 
Kama ungekuwa umenunua hiyo dawa ungeona hizo specific agent zenye kupambana na hilo tatizo tena zimeandikwa kiswahili.pili unasema imefanyiwa majaribio wapi...haa haa hivi hizi chanjo zimefanyiwa majaribio wapi kabla ya kuanza kudungwa watu..walalamishi wa nchi hii wazuri kwenye kupinga vyao na wepesi kushadadia vya kigeni kwa hoja ile ile anayoipinga...
Soma hivyo viambata vilivyoandikwa kisha fanya reserch hata kwa google..kisha uje domo la kupinga sio kulalama tu
 
Safi kabisa maelezo yameshiba
 
Wengine wote hawa tuwaonee huruma kwa ufahamu wao. Tatizo ni hawa wa SUA na UD. Watu kama hawa ni pumbav kabisa! Elimu gani wanayotuonesha nchini kama wanatuletea mizizi na majani ya hovyo hovyo kiasi hiki?
Majani ya ovyo yametafitiwa zaidi ya miaka 12 ovyo ni majani au wewe kijana unayebalegh muda huu..balance shobo kidogo
 
Mkuu, sawa hizo sheria wengine hatuzijui. Ila kitendo cha kuruhusu hizo concoctions kutambulika kama sawa za Cov 19 ni kuwatapeli wananchi na ni criminals act.
 
We unatafuta sifa tu ya kutaja majina hayo. Una maana miezi mitatu ilitosha kufanya majaribio na kujua mumea huu na ule unaweza kupambana na COVID? Tusipende kuzubaisha watu kwa vijineno vya miaka mingi iliyopita kutetea uzembe. Waganga hujitetea kwamba wameoteshwa, hawa wa vyuo vikuu walioteshwa pia? Rubbish!
 
Majani ya ovyo yametafitiwa zaidi ya miaka 12 ovyo ni majani au wewe kijana unayebalegh muda huu..balance shobo kidogo
Rubbish! Miaka 12 corona ilikuwepo? Mbona unapayuka kuendelea kupotosha watu. Elimu gani hii?

Kama unayafahamu sana kuliko sisi, hebu tueleze hizo kachumbali kama kweli zinatibu corona kwa kiasi gani?
 
Ni

Ushamba wenu tu , kama dawa za kawaida tu zina reaction na wameeleza kabisa unaweza kutapika kuhalisha na mengineyo sasa iweje hizo zenu za kiswahili?
Kwa hiyo ukiharisha ndo dawa inakolea? Wewe umeharisha mara ngapi leo?
 
Kama ungekuwa umenunua hiyo dawa ungeona hizo specific agent zenye kupambana na hilo tatizo tena zimeandikwa kiswahili.
Dawa hizi hazina specific ingridients for the specific antigens.
Chanjo zote zimefanyiwa majaribio na kila moja inajulikana efficacy yake kama jedwali linavyoonyesha hapo chini.Ulivyocheka hapo juu ni kwamba umejicheka wewe mwenyewe kwa ujinga wako wa kutokufuatilia haya mambo.

Souces:Covid: What do we know about China's coronavirus vaccines?
 
Naona kila meseji unang'ang'ania mkemia mkuu. Umeona wapi kwamba aliruhusu? Umeona wapi kwamba TBS aliruhusu? Umeona wapi kwamba TMDA aliruhusu. Au hata hujui mamlaka husika? Rubbish!
Watu kama wewe ndo munalishwa haja kubwa na matapeli kama hawa.
 
Mkuu hii dawa ya SUA binafsi nimeishuudia imewasaidia wengi sana mimi mwenye ni kiwa na mafua au kikohozi nikitumia mafua yanakata fasta nadhani labda utakuwa na shida nyingine au uliifungua ukaiacha wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…