Hizi Honda mbona zina bei mkasi sana?

Hizi Honda mbona zina bei mkasi sana?

Nadhani ule msemo wa old is gold ndipo unapofanya kazi hapa. Hapo hununui tu usafiri bali unanunua kumbukumbu ya miaka 60 nyuma.

Kwa bei hiyo wanunuzi wanazinunua na kuziweka kwenye maonyesho zinarudisha pesa mara 100 zaidi.

Power of branding.
 
Wanajamvi nimeshangaa kusikia kumiliki kifaa kipya kama hiki ni almost 10millions. Kina maajabu gani zaidi?

View attachment 2756176
Haka kakitu kanafanya kazi nyingi sana, kanaweza lima ukikafungia jembe , unaweza ukakafanya lift ya kupandia ghorofani, unaweza ukakafungia tera la mizigo , hakana shida yani na sijawahi ona kamekufa, wanunuzi wanazeeka wanakufa wanakaacha kazima tu
 
Niliziona mwaka jana hizi Honda 110 na Kawasaki zilizotumika zinauzwa bei mkasi na Madalali wa H.J Pugh Auctioneers LTD Uingereza. Moja ilikuwa ni £ 1940.

Nilimuuliza mbongo mwenzangu akasema hizo pikipiki ukinunua kizazi chako cha pili wanazikuta yaani wajukuu😁

Note: Zilizotumika miaka hiyo zikakusanywa na madalali au wenye nazo wakaziuza kwa madalali ila bado bei mkasi.
 
Wajapan walituliza kichwa Honda 110 ni kama automatic ndio pikipiki za mwanzo ambazo unaondoka bila kutumia manual clutch.

Hiyo ni automatic unatumia mafuta na pedal ya brake mguuni na brake ya mkono.
 
Honda nawaangalia tu nasema hi!

Mchina anazidi kuteka soko la dunia kwa upumbavu kama huu. Mchina anatoa matoleo ya kisasa kwa bei chee huku makampuni ya zamani kama Honda wakibaki na zile fikra za miaka ya 90
Usifananishe uchafu wa kichina na Honda. Labda kama hujui Honda ni nini.
 
Niliziona mwaka jana hizi Honda 110 na Kawasaki zilizotumika zinauzwa bei mkasi na Madalali wa H.J Pugh Auctioneers LTD Uingereza. Moja ilikuwa ni £ 1940.

Nilimuuliza mbongo mwenzangu akasema hizo pikipiki ukinunua kizazi chako cha pili wanazikuta yaani wajukuu😁

Note: Zilizotumika miaka hiyo zikakusanywa na madalali au wenye nazo wakaziuza kwa madalali ila bado bei mkasi.
Collectors wanazikimbilia sana saivi. Sababu zinapanda thamani kila siku kama vile VW Beetle.
 
Back
Top Bottom