Nafikiri unajua utofauti wa Iran na Iraq. Toka lini ushawahi kusikia Iraq inatengeneza silaha zake yenyewe, za Iran ndo hizo zinazofanya maangamizi hata katika kambi za Marekani ambazo sio rahisi kuingilika wala kushambulika, Silaha za Iran ndo zilizobadilisha hali ya vita kule Ukraine hadi magharibi wakawa wanalaumu Iran kwa kumpatia silaha Mrusi ambazo zimesabisha madhara makubwa kwa majeshi ya Ukraine. Yani zimepenya hata pale ambapo hapakutarajiwa kupenywa.
Iraq hakuwa hata na kifaru cha maana achilia mbali ndege za kijeshi, Iran ina ndege hatari zisizokuwa na ruban ambazo zimekuwa msaada kwa vita vya Russia na Ukraine, vimekuwa msaada kwa serikali ya Syria ambayo mpaka leo ipo madarakani kutokana na msaada wa Iran pamoja na Russia. We haujiulizi ilikuwa Marekani akaivamia Iraq au Libya ambazo hakuwahi kurusha hata jiwe kwa Marekani, lakini wanashindwa kuthubutu kufanya hivyo kwa Iran ambayo imekuwa ikifanya mashambulizi ya wazi na ya mara kwa mara kwa jeshi na kambi za Marekani bila kuhofia chochote na mpaka leo hawana ujanja wa uwezo wa kuthubutu kuivamia kijeshi. So tumia akili kufikiri. Kwa sababu wanaijua uajemi kuwa ndio taifa lililokuwa na nguvu toka miaka zaidi ya 3000 iliyopita before Christ, hao hawakuanza leo.
Hizo hapo chini ni miongoni mwa empire kongwe duniani.
1. Persia (Iran) empire
2. Roma empire
3. Ottoman empire