Hizi ndio nchi ambazo Marekani na Israel hawawezi kuthubutu kuingiza pua zao kushambulia kijeshi

Hizi ndio nchi ambazo Marekani na Israel hawawezi kuthubutu kuingiza pua zao kushambulia kijeshi

Kuingia vita moja kwa moja hili bado wanalo waafrika tu
Kuna mataifa mengi wanaogopa na kuona madhara ya vita hasa ukizingatia Uchumi kuporomoka na hata soko kuwa baya kimaisha


Kuna watu wanajielewa na kauoga kamo, na kuwa muoga sio vibaya wakati mwingine kama unaangalia maslahi yako
Wanasema epuka Shari
Pakistan na India sio kama hawawezi kuzichapa ila wanajua athari za vita maana huwa haina mshindi bali hasara zinatofautiana tu

Mchina amejenga visiwa (artificial islands kibao na hakuna wa kumsemesha tena sio tu kaweka viwanda bali kapeleka na manowari za kijeshi na ndege yoyote ikipata juu inapewa warning moja tu kuwa iondoke eneo hilo au itunguliwe
Lakini hakuna taifa linathubutu kulianzisha hapo

Sisi kujenga bwawa tu mpaka vitisho halafu tunalazimisha muungano
Hebu kama ni kisiwa na sisi tutengeneze kimoja tujaze wanajeshi tu

Marekani hawezi kulianzisha na Iran wala kiduku moja kwa moja kwa sababu anajua hasara
Sio kuwa hana uwezo bali ni hasara na uchumi na watu pia kufa wengi
Umetishaa
 
Niaje waungwana

Hapo chini naorodhesha nchi ambazo si Marekani wala Israel itaweza kuthubutu kuingiza pua yake kuzivamia kijeshi kwa namna yoyote ile. Hii ni kutokana na uwezo mkubwa wa kijeshi, kiintelejensia, kiteknolojia ni kiuwezo zilizo nazo nchi hizo katika kulikalisha chini na kulihenyesha taifa lolote litakalothubutu kuvamia ardhi zao.

Hata Mmarekani anajua ndomaana akitaka ku deal nao kiaina huwa anatuma tu silaha huku yeye akiwa nje ya mapambano, au anaishia kushambulia vidagaa vilivyowekwa na hao wababe wasiopenda kuendeshwa kijinga jinga na nchi za magharibi. Kuna wazungu wa buhambwe walikuwa wanaota huku wanatembea kwamba eti Marekani itaivamia Iran kutokana na mashambulizi yaliofanywa na vijana kadhaa huko Iraq.

Wazungu hawa wa buhambwe wengi waliendeshwa na mihemko kuliko uhalisia kamili wa kile wanachokiota. Wenye akili tulipinga kwamba mbabe huyo wa mchongo hawezi kutia pua uajemi kufanya shambulizi, ila hawakutuelewa. Sasa leo wameona wenyewe jinsi mbabe wao alivyokwepa jukumu la kuthubutu kuivamia uajemi. Anachotaka kufanya ni kupambana tu na vijana waliowekwa na waajemi washughulike nae.

Nchi zenyewe ni...

1. Russia
2. Iran
3. China
4. North Korea.
Hoja yako ipo sahihi ila sio sahihi sana
 
Wewe ni mnafiki. Unasema hawakufanya retaliation zozote za maana, wakati shambulizi lilileta madhara makubwa katika kambi ya Marekani nchini Iraq!

Israel hiyo ndo inashambuliwa kila siku katika ardhi yake, so yenyewe ilibahatisha kuuwa afisa mmoja au wawili ni tofauti na yeye anaeshambuliwa kila siku katika ardhi yake na kusababisha maafa makubwa kama Oktoba 7.

China geographia yake inasababisha asikutane na changamoto hizi. Kama na yeye angeishi Mashariki ya kati kwenye misukosuko ya kila siku pengine na yeye angejaribiwa japo naamini na yeye angekuwa kama Iran asingesubiri kufanywa mnyonge.

Israel akikatiwa misaada na ufadhili wa kijeshi anaopewa na nchi za magharibi kila mwaka ni mwepesi mno. anaweza kuchakazwa hata na hezbulla kama walivyomchakaza mwaka 2006 pamoja na misaada yake ya kijeshi.
Unaongea kwa ushabiki sana, mimi sipo kwenye ligi ya kushabikia ubabe wa upande wowote
Nachukia uonevu unaofanywa na nchi nyingine kwa taifa lolote.... Na ukweli ni kuwa Israel na Marekani zimefanya uonevu mwingi sana ambao siushabikii, ila kama wewe unaamini wao ndio wahanga wanaoonewa basi ni sawa
 
Ona sasa ulivyo hujui taarifa.
Iran haikupeleka jeshi bali ilishambulia kwa makombora na ndege zisizo na rubani katika kambi za vikundi vya kigaidi.
Pakistan haikuridhishwa kwasababu Iran haikutoa taarifa kwa mamlaka.
Na hata aliposhambulia Pakistan ye mwenyewe amekiri kashambulia maeneo ya waasi hakupiga kambi wala kulenga wanajeshi wa Iran moja kwa moja.
Muwe munatizama habari.
Hivi nyie mazombi mnaisigi taarifa mnapata nyie tu. Iran katwangwa bada nae kumkorofisha pakista. Kajibiwa kawa mpole
 
Mtoe Iran, Iran ni mnyonge tu, aliuawa yule Jenerali wake Qassimm Suleiman kwa drone za Usa ila hawakufanya retaliation zozote za maana, Israel pia anaua na kushambulia maafisa wa juu wa Iran na wanasayansi wake, kitu ambacho hawawezi kufanya kwa nchi kama China
Siungi mkono wala sipendi uchokozi wa Marekani wala wa Israel, ila Iran hana ubabe wa kiasi hicho na anaweza kuvamiwa tu kama wakiona mazingira yanaruhusu
Hata marekani si wameshambuliwa kambi zao huko iraq juzi hapa wamepigwa kambi zao huko Jordan
Ni iran pekee anaeweza kufanya haya kuliko mwengine yeyote
 
Hivi nyie mazombi mnaisigi taarifa mnapata nyie tu. Iran katwangwa bada nae kumkorofisha pakista. Kajibiwa kawa mpole
Kama alivyokua mpole Americant baada ya magaidi wake kufyekwa kule Jordan wakiwa wanafanya ugaidi
 
Hivi nyie mazombi mnaisigi taarifa mnapata nyie tu. Iran katwangwa bada nae kumkorofisha pakista. Kajibiwa kawa mpole
Kaka kuwa mtu mzima kidogo.
Mwenzako kaleta habari pale uliisoma??
Acha ubishani wa kitoto.
Pakistan alidai kushambulia maficho ya washika silaha Boluchistan.
Mie huwa sipendi kubishana hupenda majadiliano.
 
Iran juzi amepigwa na Pakistani tena ndani ya ardhi yake, akakimbilia kuomba msamaha.
Mkuu Pakistan yenyewe imetoa kauli kuwa imepiga armed group site in Boluchistan.
Na Boluchistan inachangiwa na Iran na Pakistan.
Hivyo sio mpaka wa Iran pekee.
Pakistan hakutoa madai kuwa kalipiza kisasi kama mnavyodai .
Na aliyeitisha kikao cha usuluhishi ni Pakistan sio Iran.
 
Kushambulia ukiwa mbali hiyo hata Israel inafanyika kwa kushambuliwa na hezbullah, au Marekani kushambuliwa na vikundi vya itikadi kali.

Nazungumzia kuingia kabisa katika ardhi kijeshi kama ilivyofanyika Ukraine, Iraq, Libya nk.
Mkuu si Iran inataka kuifuta Israel kwenye Ramani ya dunia. Nini kimemshinda?
 
Unaongea kwa ushabiki sana, mimi sipo kwenye ligi ya kushabikia ubabe wa upande wowote
Nachukia uonevu unaofanywa na nchi nyingine kwa taifa lolote.... Na ukweli ni kuwa Israel na Marekani zimefanya uonevu mwingi sana ambao siushabikii, ila kama wewe unaamini wao ndio wahanga wanaoonewa basi ni sawa
Hakuna ushabiki hata chembe. Labda wewe ndo unaandika bila kuangalia uhalisia unaosababisha Israel ionekane ina kiburi cha kuchokoza wenzake.

Uchokozi wa Israel unatokana na kiburi cha misaada ya kijeshi inayopewa kutoka Marekani na baadhi ya nchi za magharibi.

Kama wangeiacha ijitegemee yenyewe kama Iran, North Korea au Venezuela basi leo hii Israel ingekuwa taifa la kinyonge na la kawaida tu kama Misri, Ugiriki na nchi nyingine ambazo hazitegemei badget ya kijeshi kila mwaka kutoka Marekani.

Ni kama Makonda miaka zaidi ya mitatu alikuwa mpole na mkimya kama mimi na wewe kwa sababu ya kukosa backup ya wakubwa nyuma yake. Lakini leo hii amepewa shavu na mkuu wa nchi, sasa hivi kageuka mbogo mpaka kwa wakuu wa mikoa, mawaziri fulani, na wabunge wa chama chake wanamgwaya.

So ukiwa na bacup hata ukiwa hauna nguvu watu watakuogopa tu kwa sababu ya kulindwa na mwenye nguvu. Hivyo ndo ilivyo kwa Israel ya leo, bila backup ya Mmarekani, UK na EU ni nyepesi sana kivita, kiuchumi na mambo mengine mengi tu. Tuache ushabiki maandazi hauna maana.
 
Asante Mkuu, ndio ukweli
Watu wanafikiri vita ni piga ua yameisha ila kuna athari kubwa sana
Hili hata mimi silipingi mkuu, japo kuna wale wenzangu na mimi walipoona kambi za Marekani zinashambuliwa kule Iraq na Syria wakaanza kufikiri kwamba jibu la Marekani itakuwa ni kuivamia Iran kijeshi kitu ambacho ni dhahiri kuwa wanaota mchana kweupe huku wanatembea.
 
Hata marekani si wameshambuliwa kambi zao huko iraq juzi hapa wamepigwa kambi zao huko Jordan
Ni iran pekee anaeweza kufanya haya kuliko mwengine yeyote
Ni Iran pekee pale Mashariki ya kati ndo vijana wake wana uwezo wa kushambulia kambi za jeshi za Marekani na wakati huo huo wakashambulia ardhi ya Israel. Nchi moja tu ambayo haina backup yoyote ya badget ya kijeshi kutoka popote ila inadhibiti ujinga wote unaoendelea pale Mashariki ya kati.
 
Back
Top Bottom