Israel tunaipa sifa kwa sababu ya biblia tu na dini. Lakini kiuhalisia tukiacha kuendekeza unafki na hisia za dini. Israel haina nguvu yoyote ya kuwa super power katika dunia hii ya leo. Kwa sababu inategemea kila kitu kutoka nje mpaka badget yake ya kijeshi inatoka Marekani, UK na Ulaya.
Hizo nchi zikijitoa kuisaidia au kuiwekea vikwazo kama Iran au North Korea kwa miaka mitano tu itakuwa nyang'a nyang'a kama chapati ya maji iliyowekwa maji mengi.
Tukiweka mihemko pembeni kusema ukweli wanaume ni Iran na North Korea maana pamoja na vikwazo vya nchi kubwa za magharibi kwa zaidi ya miaka 70 lakini bado zinatengeneza silaha zao zenyewe tena zile kubwa kubwa, hatari na za kisasa, nafikiri umeona ndege zisizo na ruban za Iran zilizobadilisha hali ya vita kule Ukraine hadi nchi za magharibi na Ukraine yenyewe zilikuwa zinalalamika kuwa vita imebadilika ghafla na kuwa ngumu kwa Ukraine baada ya Iran kumpa mrusi zile ndege zake, hapo sijazungumzia silah zingine ambazo anaziweka kwa ajili ya matumizi yake binafsi, hizo nchi hazitegemei msaada wa kifedha wala wa kijeshi kutoka kwa nchi nyingine yoyote, zina intelejensia yao, teknolojia zao, na juzi wao.
Iran juzi karusha satellite zake tatu. Jiulize kama hizo nchi zisingewekewa vikwazo kama Israel, Japan au Uk leo hii zingekuwa wapi kijeshi na kiuchumi. Israel haina vikwazo, inapewa misaada, na inafadhiliwa badget ya jeshi kila mwaka, lakini cha kushangaza juzi waliposhambuliwa na vijana elf 20 tu wanaotumia silaha duni, yeye kakimbilia kuomba msaada mungine wa kijeshi kutoka Marekani, kaita mpaka jeshi la akiba na wale wastafu ili kuja kupambana na vijana wanaotumia silaha za kienyeji, hawana jeshi wala uwezo wa kununua silaha. Alafu cha kushangaza zaidi na Marekani akamuongezea na ile meli yake ya kijeshi kupambana na wana mgambo elfu 20 ambao idadi yao haifiki hata ya raia wanaoishi kata ya manzese.
Alafu mtu useme eti nchi hiyo ikipigana dunia itatingishika. Ipigane mara ngapi na wakati leo ipo vitani kwa zaidi ya miezi minne kupambana na vijana duni elfu 20 bila kufikia malengo ya kuokoa mateka hata mmoja.
Huu ni unafiki wa hali ya juu ambao moyoni kwako mwenyewe unakataa [emoji23][emoji23][emoji23]
Ukiniambia Russia na Marekani, Japan na China au Iran na Uturuki hapo nitaelewa.