Hizi ndio nchi ambazo Marekani na Israel hawawezi kuthubutu kuingiza pua zao kushambulia kijeshi

Hizi ndio nchi ambazo Marekani na Israel hawawezi kuthubutu kuingiza pua zao kushambulia kijeshi

Juzi tu Pakistan nao wameshambulia katika ardhi yao, acheni kuwapaisha, ata Iraq walisema haitowezekana, akapigwa, na Iran atapigwa tu. Ni suala la muda.
Nafikiri unajua utofauti wa Iran na Iraq. Toka lini ushawahi kusikia Iraq inatengeneza silaha zake yenyewe, za Iran ndo hizo zinazofanya maangamizi hata katika kambi za Marekani ambazo sio rahisi kuingilika wala kushambulika, Silaha za Iran ndo zilizobadilisha hali ya vita kule Ukraine hadi magharibi wakawa wanalaumu Iran kwa kumpatia silaha Mrusi ambazo zimesabisha madhara makubwa kwa majeshi ya Ukraine. Yani zimepenya hata pale ambapo hapakutarajiwa kupenywa.

Iraq hakuwa hata na kifaru cha maana achilia mbali ndege za kijeshi, Iran ina ndege hatari zisizokuwa na ruban ambazo zimekuwa msaada kwa vita vya Russia na Ukraine, vimekuwa msaada kwa serikali ya Syria ambayo mpaka leo ipo madarakani kutokana na msaada wa Iran pamoja na Russia. We haujiulizi ilikuwa Marekani akaivamia Iraq au Libya ambazo hakuwahi kurusha hata jiwe kwa Marekani, lakini wanashindwa kuthubutu kufanya hivyo kwa Iran ambayo imekuwa ikifanya mashambulizi ya wazi na ya mara kwa mara kwa jeshi na kambi za Marekani bila kuhofia chochote na mpaka leo hawana ujanja wa uwezo wa kuthubutu kuivamia kijeshi. So tumia akili kufikiri. Kwa sababu wanaijua uajemi kuwa ndio taifa lililokuwa na nguvu toka miaka zaidi ya 3000 iliyopita before Christ, hao hawakuanza leo.

Hizo hapo chini ni miongoni mwa empire kongwe duniani.

1. Persia (Iran) empire
2. Roma empire
3. Ottoman empire
 
Iran haimo acha ushabiki
Iran haimo kivipi mbona haueleweki?

Kati ya hizo nchi nilizotaja, ni nani ana mdindia Mmarekani live live na kupiga mabomu kambi zake kila siku.

Unafikiri Iran ingekuwa Libya, Iraq au Venezuela ndo zinashambulia kambi hata moja au mbili tu za Marekani hali ingekuwaje
 
Niaje waungwana

Hapo chini naorodhesha nchi ambazo si Marekani wala Israel itaweza kuthubutu kuingiza pua yake kuzivamia kijeshi kwa namna yoyote ile. Hii ni kutokana na uwezo mkubwa wa kijeshi, kiintelejensia, kiteknolojia ni kiuwezo zilizo nazo nchi hizo katika kulikalisha chini na kulihenyesha taifa lolote litakalothubutu kuvamia ardhi zao.

Hata Mmarekani anajua ndomaana akitaka ku deal nao kiaina huwa anatuma tu silaha huku yeye akiwa nje ya mapambano, au anaishia kushambulia vidagaa vilivyowekwa na hao wababe wasiopenda kuendeshwa kijinga jinga na nchi za magharibi. Kuna wazungu wa buhambwe walikuwa wanaota huku wanatembea kwamba eti Marekani itaivamia Iran kutokana na mashambulizi yaliofanywa na vijana kadhaa huko Iraq.

Wazungu hawa wa buhambwe wengi waliendeshwa na mihemko kuliko uhalisia kamili wa kile wanachokiota. Wenye akili tulipinga kwamba mbabe huyo wa mchongo hawezi kutia pua uajemi kufanya shambulizi, ila hawakutuelewa. Sasa leo wameona wenyewe jinsi mbabe wao alivyokwepa jukumu la kuthubutu kuivamia uajemi. Anachotaka kufanya ni kupambana tu na vijana waliowekwa na waajemi washughulike nae.

Nchi zenyewe ni...

1. Russia
2. Iran
3. China
4. North Korea.
Ongeza Malawi 🇲🇼
 
Hata simba kuwinda nyati hujishauri lakini nyati huliwa
 
😂😂😂 tembo anaweza kuuwawa na simba, lakini sio kwa simba mmoja, na sio kwa tembo mkubwa.

Nafikiri umenielewa vizuri ndugu.
Haaaaa hii comment sikuiona.
Hao mamba wakimuona tembo mkubwa wanakimbia katika maji sembuse simba??
Huyu jamaa ana maskhara eti,tembo auliwe na simba!
Nachofaham tembo mtoto ndio anauliwa na simba tena wasiopungua 5 au sita.
 
Niaje waungwana

Hapo chini naorodhesha nchi ambazo si Marekani wala Israel itaweza kuthubutu kuingiza pua yake kuzivamia kijeshi kwa namna yoyote ile. Hii ni kutokana na uwezo mkubwa wa kijeshi, kiintelejensia, kiteknolojia ni kiuwezo zilizo nazo nchi hizo katika kulikalisha chini na kulihenyesha taifa lolote litakalothubutu kuvamia ardhi zao.

Hata Mmarekani anajua ndomaana akitaka ku deal nao kiaina huwa anatuma tu silaha huku yeye akiwa nje ya mapambano, au anaishia kushambulia vidagaa vilivyowekwa na hao wababe wasiopenda kuendeshwa kijinga jinga na nchi za magharibi. Kuna wazungu wa buhambwe walikuwa wanaota huku wanatembea kwamba eti Marekani itaivamia Iran kutokana na mashambulizi yaliofanywa na vijana kadhaa huko Iraq.

Wazungu hawa wa buhambwe wengi waliendeshwa na mihemko kuliko uhalisia kamili wa kile wanachokiota. Wenye akili tulipinga kwamba mbabe huyo wa mchongo hawezi kutia pua uajemi kufanya shambulizi, ila hawakutuelewa. Sasa leo wameona wenyewe jinsi mbabe wao alivyokwepa jukumu la kuthubutu kuivamia uajemi. Anachotaka kufanya ni kupambana tu na vijana waliowekwa na waajemi washughulike nae.

Nchi zenyewe ni...

1. Russia
2. Iran
3. China
4. North Korea.
Umesahau na sisi Tanzania.
Watupige kwa lipi kwa mfano..?
 
Haaaaa hii comment sikuiona.
Hao mamba wakimuona tembo mkubwa wanakimbia katika maji sembuse simba??
Huyu jamaa ana maskhara eti,tembo auliwe na simba!
Nachofaham tembo mtoto ndio anauliwa na simba tena wasiopungua 5 au sita.
Kuna video niliiona mamba aliona katembo katoto kanakuja kunywa maji. Mamba akasema hapa tayari nimepata kitoweo cha kutwa nzima ya leo.

Yule tembo mdogo akasogea akawa anakunywa maji mdogo mdogo, ghafla mamba huyo kakamata mkongoja wake. Basi purukushani mamba pamoja na ukubwa wake akaonekana kuzidiwa nguvu na kale katembo. Ghafla mama mtu akaona, basi alivyokuja pale majini hakuna mamba wala kiboko aliekaa, alitibua tibua maji yote dakika mbili yakageuka tope. Pale mtoni walibaki tembo tu na mtoto wake, mamba na viboko wote walitoka nduki kuwapisha tembo wakae.
 
Pia nchi hizo haziwezi kuivamia israel na marekani ujue. By the way wababe wa kivita duniani ni israel na marekani usiombe vita itokee kati ya nchi hizo dunia itatikisika na kuharibika pakubwa
 
Pia nchi hizo haziwezi kuivamia israel na marekani ujue. By the way wababe wa kivita duniani ni israel na marekani usiombe vita itokee kati ya nchi hizo dunia itatikisika na kuharibika pakubwa
Israel tunaipa sifa kwa sababu ya biblia tu na dini. Lakini kiuhalisia tukiacha kuendekeza unafki na hisia za dini. Israel haina nguvu yoyote ya kuwa super power katika dunia hii ya leo. Kwa sababu inategemea kila kitu kutoka nje mpaka badget yake ya kijeshi inatoka Marekani, UK na Ulaya.

Hizo nchi zikijitoa kuisaidia au kuiwekea vikwazo kama Iran au North Korea kwa miaka mitano tu itakuwa nyang'a nyang'a kama chapati ya maji iliyowekwa maji mengi.

Tukiweka mihemko pembeni kusema ukweli wanaume ni Iran na North Korea maana pamoja na vikwazo vya nchi kubwa za magharibi kwa zaidi ya miaka 70 lakini bado zinatengeneza silaha zao zenyewe tena zile kubwa kubwa, hatari na za kisasa, nafikiri umeona ndege zisizo na ruban za Iran zilizobadilisha hali ya vita kule Ukraine hadi nchi za magharibi na Ukraine yenyewe zilikuwa zinalalamika kuwa vita imebadilika ghafla na kuwa ngumu kwa Ukraine baada ya Iran kumpa mrusi zile ndege zake, hapo sijazungumzia silah zingine ambazo anaziweka kwa ajili ya matumizi yake binafsi, hizo nchi hazitegemei msaada wa kifedha wala wa kijeshi kutoka kwa nchi nyingine yoyote, zina intelejensia yao, teknolojia zao, na juzi wao.

Iran juzi karusha satellite zake tatu. Jiulize kama hizo nchi zisingewekewa vikwazo kama Israel, Japan au Uk leo hii zingekuwa wapi kijeshi na kiuchumi. Israel haina vikwazo, inapewa misaada, na inafadhiliwa badget ya jeshi kila mwaka, lakini cha kushangaza juzi waliposhambuliwa na vijana elf 20 tu wanaotumia silaha duni, yeye kakimbilia kuomba msaada mungine wa kijeshi kutoka Marekani, kaita mpaka jeshi la akiba na wale wastafu ili kuja kupambana na vijana wanaotumia silaha za kienyeji, hawana jeshi wala uwezo wa kununua silaha. Alafu cha kushangaza zaidi na Marekani akamuongezea na ile meli yake ya kijeshi kupambana na wana mgambo elfu 20 ambao idadi yao haifiki hata ya raia wanaoishi kata ya manzese.

Alafu mtu useme eti nchi hiyo ikipigana dunia itatingishika. Ipigane mara ngapi na wakati leo ipo vitani kwa zaidi ya miezi minne kupambana na vijana duni elfu 20 bila kufikia malengo ya kuokoa mateka hata mmoja.

Huu ni unafiki wa hali ya juu ambao moyoni kwako mwenyewe unakataa 😂😂😂

Ukiniambia Russia na Marekani, Japan na China au Iran na Uturuki hapo nitaelewa.
 
Kushambulia ukiwa mbali hiyo hata Israel inafanyika kwa kushambuliwa na hezbullah, au Marekani kushambuliwa na vikundi vya itikadi kali.

Nazungumzia kuingia kabisa katika ardhi kijeshi kama ilivyofanyika Ukraine, Iraq, Libya nk.
Mtoe Iran, Iran ni mnyonge tu, aliuawa yule Jenerali wake Qassimm Suleiman kwa drone za Usa ila hawakufanya retaliation zozote za maana, Israel pia anaua na kushambulia maafisa wa juu wa Iran na wanasayansi wake, kitu ambacho hawawezi kufanya kwa nchi kama China
Siungi mkono wala sipendi uchokozi wa Marekani wala wa Israel, ila Iran hana ubabe wa kiasi hicho na anaweza kuvamiwa tu kama wakiona mazingira yanaruhusu
 
Mtoe Iran, Iran ni mnyonge tu, aliuawa yule Jenerali wake Qassimm Suleiman kwa drone za Usa ila hawakufanya retaliation zozote za maana,
Wewe ni mnafiki. Unasema hawakufanya retaliation zozote za maana, wakati shambulizi lilileta madhara makubwa katika kambi ya Marekani nchini Iraq!
Israel pia anaua na kushambulia maafisa wa juu wa Iran na wanasayansi wake,
Israel hiyo ndo inashambuliwa kila siku katika ardhi yake, so yenyewe ilibahatisha kuuwa afisa mmoja au wawili ni tofauti na yeye anaeshambuliwa kila siku katika ardhi yake na kusababisha maafa makubwa kama Oktoba 7.
kitu ambacho hawawezi kufanya kwa nchi kama China
China geographia yake inasababisha asikutane na changamoto hizi. Kama na yeye angeishi Mashariki ya kati kwenye misukosuko ya kila siku pengine na yeye angejaribiwa japo naamini na yeye angekuwa kama Iran asingesubiri kufanywa mnyonge.
Siungi mkono wala sipendi uchokozi wa Marekani wala wa Israel, ila Iran hana ubabe wa kiasi hicho na anaweza kuvamiwa tu kama wakiona mazingira yanaruhusu
Israel akikatiwa misaada na ufadhili wa kijeshi anaopewa na nchi za magharibi kila mwaka ni mwepesi mno. anaweza kuchakazwa hata na hezbulla kama walivyomchakaza mwaka 2006 pamoja na misaada yake ya kijeshi.
 
Kwamba Marekani aliingia kijeshi kama ilivyofanyika Iraq na Libya, au kama Russia alivyofanya kwa Ukraine au shoo kivipi?

Cause Iran ishashambulia sana ndege zisizo na ruban za Marekani pamoja na zile meli zake zilizojaribu kukatiza katika mstari mwekundu wa taifa la Iran. Pia Iran kashambulia sana kambi za Marekani pale Iraq ila bado hakuna jeshi lolote la Marekani halijathubutu kwenda kuvamia ili lifanye kama lilivyofanya kwa nchi zingine dhaifu.
Kumbuka waling'oa Kidali cha brigadier suleiman........ambacho ni sawa na wanajeshi 1000
 
Back
Top Bottom