Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Toa Iran hapo, atapigwa kama ngoma muda sio mrefu.Niaje waungwana
Hapo chini naorodhesha nchi ambazo si Marekani wala Israel itaweza kuthubutu kuingiza pua yake kuzivamia kijeshi kwa namna yoyote ile. Hii ni kutokana na uwezo mkubwa wa kijeshi, kiintelejensia, kiteknolojia ni kiuwezo zilizo nazo nchi hizo katika kulikalisha chini na kulihenyesha taifa lolote litakalothubutu kuvamia ardhi zao.
Hata Mmarekani anajua ndomaana akitaka ku deal nao kiaina huwa anatuma tu silaha huku yeye akiwa nje ya mapambano, au anaishia kushambulia vidagaa vilivyowekwa na hao wababe wasiopenda kuendeshwa kijinga jinga na nchi za magharibi. Kuna wazungu wa buhambwe walikuwa wanaota huku wanatembea kwamba eti Marekani itaivamia Iran kutokana na mashambulizi yaliofanywa na vijana kadhaa huko Iraq.
Wazungu hawa wa buhambwe wengi waliendeshwa na mihemko kuliko uhalisia kamili wa kile wanachokiota. Wenye akili tulipinga kwamba mbabe huyo wa mchongo hawezi kutia pua uajemi kufanya shambulizi, ila hawakutuelewa. Sasa leo wameona wenyewe jinsi mbabe wao alivyokwepa jukumu la kuthubutu kuivamia uajemi. Anachotaka kufanya ni kupambana tu na vijana waliowekwa na waajemi washughulike nae.
Nchi zenyewe ni...
1. Russia
2. Iran
3. China
4. North Korea.
Wanainyong'onyeshaje Russia wakati nchi za magharibi ndo zinalalamika ugumu wa maisha baada ya Russia kupiga marufuku uuzaji wa gesi yake kwa nchi hizo?USA wanatumia AKILI kupigana vita mkuu
Vita huwa sio KUSHINDA tu
Sasa hivi Russia inapigana na USA indirectly
Wakati Russia anatumia resources zake zote kupigana na Ukraine, USA akitumia washirika wake wanachangia kidogo kidogo kumnyong’onyesha Russia kiuchumi na kijeshi...... Vita ni gharama kubwa mmno
Marekani kwa sasa haitoi tena msaada kwa Ukraine, huku Russia ikiendeleza kichapo kwa kibaraka huyo wa magharibi.Russia alijiapiza eti yeyote atakaye ingilia vita kati yake na Ukraine kwa kuipa chochote Ukraine atapata kichapo ambacho hatakuja kukisahau. Sasa najiuliza Je Marekani anaisaidia Ukraine silaha kwa kificho?
Sawa tu, ila Israel hamna kazi asee kanyanyasika sana na Hamas.Kwanini tusitoe Israel mkuu tuweke Tz?
Iran haikuanza kushambulia kambi za Marekani jana au juzi. Amekuwa akifanya hivyo miaka na miaka na hakuna anaeweza kuthubutu kumface moja kwa moja. Labda washambulie vijana wake ambao na wao watajibu tu baada ya muda.Toa Iran hapo, atapigwa kama ngoma muda sio mrefu.
USA wanatumia AKILI kupigana vita mkuu
Vita huwa sio KUSHINDA tu
Sasa hivi Russia inapigana na USA indirectly
Wakati Russia anatumia resources zake zote kupigana na Ukraine, USA akitumia washirika wake wanachangia kidogo kidogo kumnyong’onyesha Russia kiuchumi na kijeshi...... Vita ni gharama kubwa mmno
Ipo siku atapakatwa mpaka kubwaga Nyaa.Israel bila Marekani na UK ni sawa sawa na vifaranga vya kuku bila mama yao. Anakuwa mnyonge kweli kweli.
Hilo shambulio lilitumia mamluki na pia Israel hawakukiri wala kukataa mashtaka walikaa kimya.Mwaka 2021 Israel walishambulia kituo cha nuclear cha Iran cha Karaj kwa drones.
China na Marekani sio maadui kihivyo, juzi kati tu hapo Xi Jinping alikuwa California anagonga mvinyo na Biden.
Watu wengi hawaelewi na wala hawajui ulichoandika. Lakini wenye akili tunakubali kuwa umeandika ukweli mtupu.Kiboko ya Mmarekani ni Mrussia tu. Hapo USA hana jambo maana anajua kina chake si cha kitoto. Kuanzia tech kaachwa mbali sana.
Israel wenyewe haiwezi kukiri moja kwa moja sababu ya kuhofia kisasi cha Iran kitakuwa na madhara makubwa kwao. Nahisi Marekani aliwambia wasijitokeze kukubali kichwa kichwa inaweza ikala kwao.Hilo shambulio lilitumia mamluki na pia Israel hawakukiri wala kukataa mashtaka walikaa kimya.
Mkumbushe kuwa Iran anachapwa sana Syria na myahudi na amekunja mkiaHapo Iran Marekani kapiga shoo sana. Soma historia ya Taifa la Iran.
Unazungumzia Israel hii inayotumia jeshi lote la nchi nzima hadi askari wa akiba, midege ya kijeshi, meli na vifaru kupambana na vijana wasiozidi elf 20 tu ambao wanatumia silaha za kienyeji na bado wameshindwa kukomboa mateka wao?Mkumbushe kuwa Iran anachapwa sana Syria na myahudi na amekunja mkia
Usisahau kumkumbusha hata Mmarekani anachapwa iraq na juzi kachapwa Jordan na muajemi ila kakunja mkiaMkumbushe kuwa Iran anachapwa sana Syria na myahudi na amekunja mkia
Kwani marekani kwa urusi amechoka make ilikua siku3 saivi ni miaka mitatuTaiwan ipo katika mikono ya China, ikiamua kuangamizwa na China ni sekunde tu.
Ila inachokataa China ni kwa vile inaamini kuwa wataiwani ni ndugu zake, hivyo kuiangamiza Taiwan ni sawa na kuwangamiza raia wake wa kesho. Marekani pale ingeishia kutuma silaha tu kama inavyofanya kwa Ukraine hadi mwisho ingechoka na kuwaachia wataiwani zigo lao wanamalizane nalo wenyewe.