Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Kuna traffic huku chanika alifariki bhaana, ile kwenda kwake kabisa watu hawakuamini nyumba alokuwa akiishi. Pale kaweka kama 150,000,000 na unaambiwa ana nyumba 3.
 
Hizo Taasisi zilizotajwa ni salary hiyo bwashee, TRA unakuta Ni 2.7 M hiyo ni salary bado posho bado overtime ukijumlisha unajikuta ww unapokea posho mwenzio wa TRA anapokea mshahara

Wenzio hela za magumashi ndio zinawafanya wajenge magorofa
Hii nakubali kabisa yaani.
 
Unayoyasema ni kweli kabisa mkuu
 
Ninachojua mimi, wale makamishna bandarini, pesa zao za pembeni wanapiga saaana. Wale wana ela kuliko hata mabrigedia.
 
Wewe jamaa wa wapi unayejaribu kuestimate mishahara ya watu kutokana na maisha wanayoishi wakati hiko kitu tulishakiongelea sana kule juu! Mada inahusu taasisi zinazolipa vizuri na siyo taasisi zinazoongoza kwa pesa za magumashi au rushwa!
 
Hehe unasema hao watu hawajioneshi! Je una uhakika gani kuwa hata taasisi tena yenye usiri kama jeshi ndiyo inajionesha?
 
Kuna mjinga mmoja anasema koplo analipwa eti mpaka 2m, ni kichaa kabisa uyu mtu.

Hapa nina salary slip ya Koplo. Ameajiriwa 2008. Ukikusanya takataka zake zooote anagota 1.1m na ameoa.
Wabongo bhana! Iko hivi mishahara na posho ya baadhi ya makoplo na masajenti inacheza kwenye 1M-2M, kwahiyo wewe kumfahamu huyo koplo anayelipwa hiyo haimaanishi hakuna makoplo wanaolipwa hizo nilizokutajia, ukizingatia jeshi ni taasisi ambayo ulipaji wake unazingatia vitu vingi kama elimu nk!!
 
- Mkuu kwa heshima na taadhima, unaposema asilimia kubwa ya Bajeti maana yake wao ndiyo wenye bajeti kubwa kuliko wote, na nilishakwambia kuwa 14.4% ya Bajeti (ambayo ndiyo asilimia kubwa kuliko zote) inaenda Wizara ya Ujenzi,hivyo 14% ndiyo asilimia kubwa kuliko zote mkuu
  • Wizara ya Ulinzi ina mafungu matatu mosi Fungu la Wizara, Ngome na Jkt, hoja ya kutokuwa na Taasisi nyingi Haina nguvu unachotakiwa kujua Jeshi lina ukubwa gani (military personnel), gharama ya kuendesha Mafunzo ni kiasi gani? Zana za kivita (ambazo ni Siri) Ni zana kiasi gani?
  • umekubali kwamba duty free shops ni miongoni mwa privilege zinazopitishwa bungeni/ kujadiliwa bungeni, hoja ya kusema Mambo ya Siri inaenda Kwenye sehemu ya Bajeti tunaita jina la jumla ambalo ni zana za kivita na huwa zinawekewa Makadirio yake.
  • bajeti ya Ziada inachapishwa Kama bajeti nyingine kwa sababu inapelekwa bungeni kwenda kuombewa Fedha za Ziada hivyo inakuwa public document,
  • Mkuu umetoa hoja gani hapa ambazo Mimi sijazipinga kwa hoja mujarabu? Tafadhali naomba uorodheshe hizo hoja moja baada ya nyingine halafu tuone nani alikuwa anayumba / kutoa hoja za Uongo.

 

Kuna mtu alikua Bunge akasema mishahara yao ya kawaida tu sio mikubwa sasa sijui alikua anatuzuga ili wana wasipambane kuhamia sielewi.
 
Kwenye taarifa ya cag jwtz ipo? Naomba kuuliza cheif?
 
Kuna mjinga mmoja anasema koplo analipwa eti mpaka 2m, ni kichaa kabisa uyu mtu.

Hapa nina salary slip ya Koplo. Ameajiriwa 2008. Ukikusanya takataka zake zooote anagota 1.1m na ameoa.
Lation hapo bado mkuu
 
- Mkuu Mimi Kwanza sijakulazimisha ukubali hoja zangu, na kuhusu bajeti nilishakwambia kuwa zinakuwaje
- by the way hujajibu hoja yangu ya kwamba tuainishe hoja zetu zote tuone nani alikuwa anayumba/ anaandika Uongo, au unaogopa afande?
 
Kwenye taarifa ya cag jwtz ipo? Naomba kuuliza cheif?
- wapo ndiyo na wanakaguliwa na ripoti inatoka ikiwana opinion za CAG
- hata PPRA (mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma) huwa waakagua manunuzi ya Jeshi.
 
- Mkuu Mimi Kwanza sijakulazimisha ukubali hoja zangu, na kuhusu bajeti nilishakwambia kuwa zinakuwaje
- by the way hujajibu hoja yangu ya kwamba tuainishe hoja zetu zote tuone nani alikuwa anayumba/ anaandika Uongo, au unaogopa afande?
Unapata wapi nguvu za kubishana na mwanamke kiasi hiki?
 
-- ww umenielekeza Mimi? Hoja gani wakati nilikuwa nakuburuza ninavyotaka au umesahau unakumbuka nilikuwa nakupa hoja za mitego kupima uelewa wako Mfano. Meja vs Kamishna wa Forodha ukakubali ukaanza kuleta ulinganisho wa Kanali na Kamishna wa Forodha, nyingine unakumbuka ulisema kwamba asilimia kubwa ya bajeti inaenda Jeshini nikakwambia siyo kweli bajeti kubwa inaenda Wizara ya Ujenzi ambayo ni trilioni 4.3 huku Ulinzi ni Trilioni 2.3 umesahau hili?, Unakumbuka mwanzoni ulisema bajeti ya Jeshi haijadiliwi bungeni nikakuburuza ukakubali kuwa inajadiliwa ukaanza kusema haipingwi nikakuuliza swali kuwa tangu lini bunge letu hili limewahi kukataa bajeti?, Nyingine nilikwambia Kuna maluteni Wana elimu wa form6 ukabisha nikakuburuza hadi ukakubali
-kuhusu Luteni nilikwambia Ni 1.5 M na sijawahi kusema 2.3 M,
- kwa hiyo Kama wanasiasa Mambo Mengi wanayaficha ww ndiye mwenye taarifa sahihi,halisia na za kweli? hebu taja Sehemu hizo taarifa zilipo.
 
-meja ana mshahara mkubwa Kama ulisema hivyo mbona baadae ukaja ukabadili msimamo wako ukaanza kusema alinganishwe na Kanali au majenerali,? Kwa nini ubadili kauli yako ya awali? Maana yake huna taarifa za uhakika hivyo una badili badili kutokana na ukweli wa hoja,
  • Umesema kwamba mtu kuwa na cheo kikubwa kwenye Taasisi fulani siyo Kigezo cha kumzidi mtu mwingine mwenye cheo wa Taasisi nyingine, hivi unadhani tujadili Wakuu wa idara wa halmashauri? Hapa tujadili Wakuu wa idara wa TRA i.e Forodha na ushuru wa bidhaa, na ndiyo ujue kwamba Kamishna wa Forodha ana pesa nyingi kuliko meja, Meja level zake ni Mameneja wa TRA wilayani
  • hoja ya asilimia kubwa ya bajeti kwenda Jeshini ilishafeli bajeti yenu Ni 2.3 trilioni, Ujenzi ni Trilioni 4.3, hata Kama Kuna matumizi ya kificho (Kama manunuzi ya Zana)hayo unayosema yatakuwa ndani ya trilioni 2.3, fedha za umma hazitoki kizembe matumizi ya fedha za umma ni lazima yawe yameidhinishwa, kuhusu uwingi/ ukubwa wa Taasisi kwamba Bajeti ya 2.3 trilioni inatumika na Jeshi tu, nilikujibu kwamba matumizi hayo yanategemea ukubwa wa Jeshi, manunuzi ya Zana, Mafunzo kwa askari,
  • Kuhusu kupingwa kwa bajeti, nimekuuliza swali ww hapa Tanzania hili bunge letu ni lini umewahi kuona Bunge limekataa kuidhinisha bajeti ya Wizara yoyote? Kama umewahi kuona hebu itaje hiyo Wizara, tatizo kila hoja unakosea Mara haijadiliwi bungeni, Mara haipingwi? Inaonekana huna msimamo na hujui taratibu za fedha za umma
  • form six maluteni wako wengi tu Jeshini, ndani ya Jeshi Hilo Hilo ulilopo na Pengine na ww umo ndani ya hao form six (wasio na ujuzi wa chochote)
-luteni hapati 2.3 M ni uongo mshahara wake Ni 1.5 M nimepinga na huo ndio ukweli,usidanganye watu humu kutaka kujilinganisha na TRA
- Ona hata usivyojua kujenga hoja huyo TMO ni wa level gani II, I, senior II, Senior I, PRINCIPAL II, PRINCIPAL I umekuwa general be specific
-ukweli upi ulionipa? Wakati nilikuwa nakuyumbisha Hadi unabadili msimamo, hivi ungekuwa na kesi ya jinai c ungeenda jela? Kwa sabab ya retract na kubadili badili
- Umeamua kuyaacha wakati huyajui? Mara haijadiliwi, Mara haipingwi? Mara asilimia kubwa ya bajeti Ni Jeshi? Huo si uongo mtupu? Labda useme kitu gani unajua mkuu? Kulenga shabaha au
 
-kwani ukiwa mwanajeshi ni kwamba utaelewa kila kitu including public finance? ww hujui huko Jeshini wanaingia hadi form four wenye ufaulu wa chini/ form six wenye ufaulu wa chini? unatarajia hao wenye form4/6/ Degree (wenye uwezo mdogo) wataweza kupambanua Mambo ya kuhusu fedha za umma? Si wanachojua wao wapokee mishahara na posho tu,
-Kuwa tpdf haimaanishi kwamba unajua/ uelewa wa Mambo ya fedha, ndiyo maana ww ukaropoka kuwa Bajeti haijadiliwi bungeni, nikakurekebisha kwamba inajadiliwa, ukabadili ukaanza kusema haipingwi nikakuuliza swali kwamba lini kwenye Bunge letu limekataa kupitisha Bajeti? hili swali ulijibu? Halafu ndiyo maofisa nyie mna mawazo haya je wale mnaowaongoza watakuwaje?
- Kuhusu taarifa zinapatikana tu kirahisi Tena kutoka Primary source, ikiwa mishahara ya Kitengo (usalama) inajulikana sembuse ya Jeshi )
-maluteni wa form six wapo jeshini,
- kuhusu kurekebishwa kwa bajeti maana yake unarekebisha aidha numerical error za shilingi mfano unakuta wameandika bilioni 230 badala ya bilioni 23 hapo lazima Bunge litarekebisha hawawezi kupitisha kitu chenye kasoro, hivyo hivyo kwenye Bajeti ya Ulinzi ikitokea wameandika mfano trilioni 23 badala ya trilioni 2.3 patarekebishwa Bunge haliwezi kupitisha kitu chenye kasoro umenipata?
 
-ni kweli hujui mshahara wa Kamishna wa Forodha ndiyo maana ukasema anazidiwa, na Meja,
-Wapi Mimi nimesema kwamba form4 wanakuwa maofisa (onyesha) hoja ya form four failure imekuja baada ya kusema Askari wanajua vizur Mambo ya kijeshi yahusuyo Bajeti ndiyo nikakupinga hapo
  • umeona Sasa unavyojichanganya mwanzon ulisema Hakuna maofisa wa form six nikakwambia wapo, sasa umekubali kuwa wapo ila utaratibu wa Sasa ni Hadi uwe na degree/ diploma? Umekubali kwamba maofisa wa form six wapo, ndiyo maana Mimi nakwambia Nina kuburuza nnavyotaka na ukaburuzika Hadi unabadili kauli yako
  • Bajeti ya Jeshi inajadiliwa Bungeni,Kama Bajeti ya Tamisemi nothing special kwa Jeshi, Sasa hiyo Bajeti unayosema ya ziada itapitishwaje bungeni bila kuingia kwenye Hansard? Document yoyote ile ikishafika bungeni ni Public document, Sasa Bajeti itapitishwaje na bunge bila kujadiliwa? inaonekana hujui hata parliamentary business zinavyofanyika, bajeti inasomwa na waziri husika na Wabunge wanachangia hoja kuhusu hiyo bajeti, Sasa unaposema inapitishwa na haiwi published ni Uongo shughuli za bunge zote zinaendeshwa kwa Uwazi na kwa njia ya mijadala, na document yoyote ikishaingia bungeni ni public document, Sasa itapitishwaje bungeni bila kuingizwa kwenye Hansard? Unajua maana ya Hansard na Kazi ya Hansard?
  • Kuhusu suala la Zana za kivita ni wapi nimesema haiko kwenye Bajeti kuu? Mimi nikichosema ni kwamba ikitokea bajeti ya Jeshi haitoshi waziri anapeleka 'Bajeti ya ziada' bungeni kwa ajili ya Hilo Jambo na Kama ni Mambo ya Siri Kama silaha waziri hatataja hizo silaha atajaja tu 'zana za kivita'
  • Kwa hiyo watu wengi wakiunga mkono Jambo fulani inamaanisha Hilo Jambo ni la kweli? hao wengi unawajua personally uelewa wao? Mshahara ni 1.5 M huo ndiyo ukweli na sijawahi kubadilisha
  • Kuhusu kuleta salary scales za TRA, huyo aliyeleta hizo scale una uhakika naye? Na unaamini alichokisema ni kweli?
  • unataka kujilinganisha Na TRA ? Hivi Ugumu wa interview za TRA unazilinganisha na za huko kwenu?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…