Hakuna hiko kitu mzee, Ninawajua MAKANALI wa JWTZ kibao maisha yao hayaakisi mzigo wa MIL 10 per month.Kwa kigezo kipi alipwe 10M hivi unajua interval ya mishahara ya vyeo vyao? By the way anaweza kuwa analipwa pungufu ya hiyo ila ukijumlisha na posho na matakataka mengine yote wanayopata wanaweza kuzidi hata hiyo 10M nje ya mishahara!
Hakuna hiko kitu tuishie hapa.Mkuu na wewe uko kwenye lile kundi la wale wanaokadiria mishahara ya watu kutokana na namna wanavyoishi? Wakati tulishasema mtu anaweza kuwa na mshahara mkubwa na bado akawa na njaa na mwingine anaweza kuwa na mshahara mdogo na bado akawa na maisha mazuri tu!
By the way sijasema kuwa 10M ni mshahara wa Kanali ukinisoma vizuri hata mimi nimempinga jamaa kwamba hawezi kulipwa hivyo! Nikasema kwamba ila ukijumlisha na posho na matakataka mengine yote anayopata yeye na familia yake unaweza kuta gharama ikazidi hata hiyo 10M nje ya mshahara!
Matumizi yanatofautiana bro kuna mtu unaweza muona ana njaa ukadhani ana mshahara mdogo kumbe ana mshahara mzuri ila majukumu mengi anahudumia karibu ukoo mzima na mwingine inaweza kuwa ni mpenda anasa tu hivyo pesa zake hazikai! Binafsi nawafahamu makanali wanaokula maisha!
Nimeipenda comment yako....!! Tuko pamoja...ni kazi sana...tunabaki kushangaa tu du...hakuna namna.
Ni tag akikupa jibuYou are very right boss.
According to your level, can you mention at least 2. I am interested to know
Msaada tafadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app
-hivi hata Kama kweli uko jeshini(japo hainisaidii) huwezi ukadanganya watu? ,Kinachonifanya niamini uko jeshini ni uelewa wako ndiyo maana Kuna mahali nilikwambia pengine ni Form six, hivi ofisa gani wa TRA hajui Mambo madogo madogo Kama ya public finance? okay sawa Kama uko TRA uko kitengo gani, na umeajiriwa Kama nani?Umesema sijui mshahara wa kamishna hivyo siko TRA vile vile umesema sijui mshahara wa luteni ila bado umekomaa kuwa mimi niko jeshini we jamaa mbona una porojo nyingi hivi? Kinachokufanya ulazimishe kuwa mimi niko jeshini ila siko TRA ni kipi hasa mbona unazunguka sana au ndiyo unataka kudanganya watu kuwa TRA tuna uspecial sana?
Hapo kwenye kuwepo maluteni wa form six jeshini pia nimekuburuza kwa sababu mwanzo kabisa nilisema "MIAKA HII hakuna luteni wa form six jeshini ni lazima wakasome kwanza degree ndiyo waje kuvalishwa nyota" ukitaka rudi hata kwenye ile comment ukasome tena! Sasa hivi umekubali kuwa kumbe ni lazima wakasome kwanza ndiyo wapewe nyota!
Kuhusu bajeti ya jeshi nimegundua umegoma kuamini kwa sababu hutaki kukubali kwamba hii nchi jeshi ni tofauti kuliko taasisi nyingine za nchi maana nilishakufafanulia namna bajeti ya ziada inavyotolewa ila wewe umekazana kwamba bajeti kuu ndiyo bajeti pekee na kwamba eti matumizi yote ya jeshi yanawekwa kwenye bajeti kuu! Baki na imani yako!
Nilishakuambia fanya utafiti kutoka kwa watu wanaojua hayo mambo kiundani zaidi tena upate wale ambao watakuwa tayari kukufanulia maana wengine hawawezi kukuambia kitu watakuambia tu hayo hayo unayoyajua wewe na unayotaka kuyasikia! Halafu ulivyo wa ajabu unaona ugumu wa interview za TRA ila huoni ugumu wa mafunzo ya TPDF kazi kweli kweli!
Mkuu takwimu za hii nchi hasa zinazowekwa na serikali au wanasiasa siyo za kuziamini sana ndiyo maana nakuambia fanya utafiti wako utagundua zaidi ya hayo unayoyajua wewe! Nchi hii hii ambayo serikali inakuambia eti mapato ya utalii ni 2B kwa mwaka wakati ukiwauliza tour guides wa TANAPA wanakuambia mapato halisi ni 6B halafu mtu unasema unaiamini serikali?
Kumbe ni demu?Unapata wapi nguvu za kubishana na mwanamke kiasi hiki?
-- Mbona hujajibu maswali yangu? Swali la kwanza nimekuuliza majibu yako yanayohusu fedha unayatolea wapi? (Mimi yangu nayapatia kwenye Katiba)Sasa kwa kigezo kipi unaweza sema kwamba kinachofanya uamini kuwa mimi ni mwanajeshi ni uelewa wangu? Hilo swala la kusema eti ofisa gani wa jeshi sijui mambo madogo madogo inabidi nikuulize wewe sasa uliyesema kuwa mimi ni mwanajeshi tena unakazana eti ni ofisa niliyeishia form six!
Kuhusu kuwepo na maofisa walioishia form six jeshini nimeshakuambia nenda karejee ile comment tena! Narudia tena nilisema "MIAKA HII hakuna mtu anayevalishwa nyota akiwa na elimu ya form six" na nikakufafanulia kuwa ni lazima wakasome kwanza wawe na profession ndiyo wapewe nyota!
Kuhu_-su bajeti mkuu naona umeamua kujitoa ufahamu kabisa na kujifanya huelewi pamoja na kwamba nimeshakufafanulia! Hizo taarifa zote unazozisema kuhusu bajeti zinajulikana hata google ukitaka unazipata ila kiuhalisia bajeti ya jeshi siyo 2.3T mzee jeshi lina bajeti ya ziada ambayo haiwekwi wazi popote!
Unavyosema jeshi siyo tofauti ila usalama wa taifa ni tofauti unashindwa kujua kuwa usalama wa taifa kuwa tofauti haizuii jeshi nalo kuwa tofauti! Na kwa sababu hapa tunalinganisha jeshi na taasisi kama TRA hivyo point yangu ni jeshi ni tofauti kulinganisha na taasisi za kiraia na siyo taasisi za kiusalama!
Kuhusu ugumu wa TRA na jeshi ni nani amekudanganya kuwa mafunzo ya jeshi ni ya kutumia nguvu tu wakati hata jeshini kuna mitihani na watu wengi hufeli mitihani kuliko mazoezi! Na kuhusu mapato ya utalii nilimaanisha in USD na siyo TZS sababu hata takwimu zao mara nyingi huwa wanaziweka katika USD!
Hivi huu ubishi utaisha kweli?Kwanza kabisa kuhusu mimi kuwa TRA kitengo gani na nina cheo gani hilo siwezi kukujibu wala kukupa uthibitisho wowote siwezi kukuonesha salary slip wala job description ili uamini! Na nilishakuambia tangu mwanzo sikukuambia ili wewe uamini bali nilikuwa nakupa taarifa tu sasa kama unafikiri nisipokujibu ndiyo itabadili ukweli kuwa niko TRA basi sawa!
Pili kuhusu sheria ya jeshi kupewa bajeti ya ziada ambayo haichapishwi hiyo sheria haipo kwenye katiba wala wapi na haitakaa iandikwe popote pale ndiyo maana nikakuambia fanya utafiti kwa wahusika! Hata hiyo bajeti unayosema jeshi litaongezea tena nayo ni bajeti kuu na siyo hiyo bajeti ya ziada ninayokuambia ambayo inakaguliwa vizuri tu ila HAICHAPISHWI!
Hii nchi usifikiri kila kitu kinawekwa kwenye katiba yaani unafikiri wewe unaijua katiba kuliko wenyewe walioitunga na hata hawaifuati kila siku wanavunja sheria ndiyo watashindwa kuvunja sheria kwa kuliongezea jeshi bajeti ya siri! Ndiyo maana nikakuambia hii serikali siyo ya kuiamini nikakutolea mfano wa namna tunavyofichwa hata kwenye mapato ya utalii!
Kuhusu ugumu wa interviews za TRA na mitihani ya jeshi huna hoja mzee mitihani ya jeshi ni migumu na hata hao wanaochukuliwa na division 1 na 2 za form six waliosoma PCB na PCM nao wapo wanaofeli! Kuhusu kina 'baba kanituma' kwani unafikiri huku TRA hawapo au kwa vile mmedanganywa kuwa ajira zikipitia PSRS ndiyo hakuna kina 'kamlete?
Kuhusu takwimu za utalii hujaniburuza mkuu bali ni kwamba inaonesha hujui mapato ya utalii ya nchi hii huwa yanaandikwa kwa currency ipi kwenye takwimu za benki kuu! Wala sijakosea na nilimaanisha nilichokiandika kwamba serikali inasema mapato ni 2B ila tour guides wanasema mapato halisi ni 6B mengine tunafichwa na wala sikusema ni TZS ulikurupuka!
Kuhusu kuwepo na maluteni walioishia form six jeshini nimekuwekea screenshot ya comment yangu ya kwanza kabisa kuhusu huo mjadala hiyo hapo uone nilivyokuburuza! Tena nimeweka uliyoniquote ili usije ukasema labda niliedit so tangu mwanzo nilishasema "miaka hii" na nilikuwa na uhakika na nilichokisema sababu najua zamani walikuwepo tena wengi tu!View attachment 2118983
- Umekubali kuwa ww Ni Muoga? Umeshindwa hata kusema wewe ni Customs Officer II?, Umeogopa kusema kwa sababu ningekuuuliza maswali hadi ungeikimbia hii thread by the way hata kubuni tu kuwa ww Ni ofisa Forodha ii? hoja number moja umeshindwa/ Umeogopa kutaja kuwa uko TRA kwa sababu Umeogopa maswaliKwanza kabisa kuhusu mimi kuwa TRA kitengo gani na nina cheo gani hilo siwezi kukujibu wala kukupa uthibitisho wowote siwezi kukuonesha salary slip wala job description ili uamini! Na nilishakuambia tangu mwanzo sikukuambia ili wewe uamini bali nilikuwa nakupa taarifa tu sasa kama unafikiri nisipokujibu ndiyo itabadili ukweli kuwa niko TRA basi sawa!
Pili kuhusu sheria ya jeshi kupewa bajeti ya ziada ambayo haichapishwi hiyo sheria haipo kwenye katiba wala wapi na haitakaa iandikwe popote pale ndiyo maana nikakuambia fanya utafiti kwa wahusika! Hata hiyo bajeti unayosema jeshi litaongezea tena nayo ni bajeti kuu na siyo hiyo bajeti ya ziada ninayokuambia ambayo inakaguliwa vizuri tu ila HAICHAPISHWI!
Hii nchi usifikiri kila kitu kinawekwa kwenye katiba yaani unafikiri wewe unaijua katiba kuliko wenyewe walioitunga na hata hawaifuati kila siku wanavunja sheria ndiyo watashindwa kuvunja sheria kwa kuliongezea jeshi bajeti ya siri! Ndiyo maana nikakuambia hii serikali siyo ya kuiamini nikakutolea mfano wa namna tunavyofichwa hata kwenye mapato ya utalii!
Kuhusu ugumu wa interviews za TRA na mitihani ya jeshi huna hoja mzee mitihani ya jeshi ni migumu na hata hao wanaochukuliwa na division 1 na 2 za form six waliosoma PCB na PCM nao wapo wanaofeli! Kuhusu kina 'baba kanituma' kwani unafikiri huku TRA hawapo au kwa vile mmedanganywa kuwa ajira zikipitia PSRS ndiyo hakuna kina 'kamlete?
Kuhusu takwimu za utalii hujaniburuza mkuu bali ni kwamba inaonesha hujui mapato ya utalii ya nchi hii huwa yanaandikwa kwa currency ipi kwenye takwimu za benki kuu! Wala sijakosea na nilimaanisha nilichokiandika kwamba serikali inasema mapato ni 2B ila maafisa wa TANAPA wanasema mapato halisi ni 6B mengine tunafichwa na wala sikusema ni TZS ulikurupuka!
Kuhusu kuwepo na maluteni walioishia form six jeshini nimekuwekea screenshot ya comment yangu ya kwanza kabisa kuhusu huo mjadala hiyo hapo uone nilivyokuburuza! Tena nimeweka uliyoniquote ili usije ukasema labda niliedit so tangu mwanzo nilishasema "miaka hii" na nilikuwa na uhakika na nilichokisema sababu najua zamani walikuwepo tena wengi tu!View attachment 2118983
- Kwani kuna tatizo gani kutaja Cheo chako mahali ulipo? Mimi nimekwambia utaje Cheo, usitaje uko TRA ya mkoa gani mbona simple ungesema tu ww ni Customs Officer II, tungeendelea na Kukuuliza maswali ili kupima uelewa wako, Kama issue ni ku- Google mbona umeshindwa kujua Sheria zinazoongoza bajeti ya Tanzania? Kama ku- Google ni rahisi kwa kila mtu (na kuchambua taarifa), Sasa Kama ulikuwa na uwezo wa kuuliza hayo maswali kwa huyo mtu mwenye hicho Cheo unachokisemea kwa nini hukuuliza? ningekuuliza maswali ya Taxation na Customs usingejibu labda uwapelekee wataalam wa kodi wa Taasisi ya Kodi (ITA) ambao baadhi yao wasingepata majibuNimekataa kutaja kwa sababu sina haja ya kujiexpose position niliyonayo na salary ninayopata kisa haya mabishano ili tu nikuaminishe wewe, na nisingeshindwa kukudanganya ningeweza kukutajia hata cheo kikubwa zaidi ila nidanganye ili iweje? Maswali gani hayo ambayo ningekimbia wakati hata nisingekuwa TRA bado ningekuwa na uwezo wa kupata hizo taarifa google kama wewe, au kwa mtu ninayemfahamu mwenye hicho cheo kisha nikaja kukujibu na bado ungeamini!
Umeishiwa hoja sasa umeamua kujificha kwenye mwamvuli wa sheria eti sheria gani inayogovern ugawaji wa nyota, mwanzo uling'ang'ania kwamba maluteni walioishia form six wapo nikakuambia miaka hii hawapo walikuwepo zamani! Sababu zamani wasomi wengi walikuwa hawajiungi na jeshi hivyo mtu aliyeishia form six alionekana dili sana jeshini, hata kina Mabeyo na wenzie wengi nao wenyewe tunajua walivishwa nyota wakiwa na elimu ya form six kisha wakaja kujiendeleza hapo baadaye!
Ila miaka hii wasomi wengi wanajiunga na jeshi hivyo kuwa na elimu ya form six jeshini siyo dili tena wakiwarecruit lazima wakasome kwanza wawe na professions kisha ndiyo wanakuja kupewa mafunzo ya uafisa, na huo ndiyo utaratibu wa sasa hivyo hakuna tena anayepewa nyota akiwa na elimu ya form six! Kuhusu connection hakuna taasisi ya serikali isiyo na kina baba kanituma, TRA wapo na Jeshini wapo na hata wasio na connection wapo pia na wanapita vizuri tu mradi wana sifa!
Hilo la kusema eti kusoma PCB na PCM siyo justification inabidi mimi ndiyo nikushangae wewe ambaye mwanzo ulisema wanaofeli mitihani itakuwa ni wale wanaochukuliwa wakiwa form four failures, ndiyo maana nikakuambia kama unaona kigezo ni hicho wapo hata form six waliopata division 1 na 2 PCB na PCM na wanafeli mitihani ya jeshi! Mkuu wala hakuna haja ya kuzuga kwenye kiswahili nilichokitumia, narudia tena MIAKA HII HAKUNA ofisa aliyeishia form six jeshini hasa kuanzia 2010s!
Kuhusu bajeti nimeshakuambia na narudia tena kusema bajeti halisi ya jeshi siyo 2.3T ni zaidi ya hiyo ila hiyo ya ziada hakuna sheria sehemu yoyote ile inayoijadili hiyo bajeti kwa sababu ya usiri wa taasisi, kama ambavyo hakuna sheria inayoruhusu magari ya jeshi kupita upande wowote wa barabara! Kuhusu takwimu za utalii nimeshakuambia hujui huwa zinaandikwa kwa currency gani, ungekuwa unajua usingekurupuka kudhani ni TZS eti kisa tu mimi wakati naelezea sikufafanua kama ni USD au la!
Wakuu huu ndo mtiririko wa taasisi za serikali zinazolipa unono na zenye maslahi makubwa kwa watumishi wake
1. TPDC
2. TCRA
4. Ngorongoro
3. Ewura
4. WCF
5. TBS
5. TANAPA
5. Tume ya madini
6. Mamlaka ya chakula na dawa
7. SSRA
8. NSSF/PSSSF
9. BOT
9. Bunge
9. Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali
10. TASAC
10. TRA
11. MSD
11. TAKUKURU
11. EGA
12. NHIF
13. TPA
13. TIC
14. KADCO
15. TANESCO
16. TANROAD
17. TAA
- Mkuu vipi mbona unalia ? Unasema umefafanua, lakini kimsingi hujafafanua hata kidogo, but rather umeshindwa kutoa majibu ya hoja, mfano Ulikimbia hoja ya kamisheni kuwa zinatolewa kwa sheria gani? au ulitaja?Mkuu mbona maelezo mengi halafu unarudia maswali yale yale ambayo nimeshakufafanulia tofauti ni kwamba tu unabadilibadili maneno ili ionekane unaongea kitu tofauti wakati kila nikisoma naona ni yale yale uliyoyaandika kwenye comments zilizopita ambazo nilishajibu? How many times do you want me to repeat the same things over and over again?
Kuhusu position yangu TRA nimeshakueleza SIWEZI KUTAJA no matter what you conclude haibadili ukweli kuwa niko TRA sina haja ya kujifanya niko TRA eti kisa unaona huku kuna mishahara mizuri! Kwanini nisingejifanya niko TCRA au eGA ambako huko ndiyo kuna mishahara mizuri sasa nijifanye niko TRA ili inisaidie nini kwa kitu gani kizuri tunachopata huku?
Kuhusu bajeti ya jeshi nilishakueleza hiyo bajeti ya ziada siyo kwamba jeshi linakwapua hiyo nayo INAKAGULIWA kote kuanzia Bungeni hadi kwa CAG ila tu HAICHAPISHWI! Mbona unajua kuwa bajeti ya usalama wa taifa INAKAGULIWA ila HAICHAPISHWI sasa nani kakuambia kuwa kwa jeshi hilo haliwezekani kama ni usiri mbona hata jeshi nalo lina usiri?
Ofcourse ukilinganisha usalama wa taifa na jeshi kwenye usiri usalama wa taifa ndiyo ina usiri zaidi kuliko jeshi ndiyo maana nikakuambia usalama wa taifa kuwa na usiri haizuii jeshi nalo kuwa na usiri ni kwamba tu moja imezidi nyenzie! Tofauti ya bajeti zao ni kwamba ya usalama wa taifa YOTE haichapishwi ila ya jeshi NUSU inachapishwa NUSU haichapishwi that's it!
Hiyo ambayo haichapishwi ni ile ya ziada ambayo matumizi yake yoyote hayawekwi hadharani achana na hiyo bajeti kuu ambayo matumizi yake yote yanawekwa hadharani so bajeti kamili ya jeshi kiuhalisia siyo 2.3T ni zaidi ya hiyo na serikali inajua na imaruhusu pamoja na kwamba hawajaiwekea sheria!
Wewe huwezi kuwabishia maafisa waandamizi wa jeshi mkuu!
Kuhusu magari ya jeshi kupita upande wowote wa barabara wewe ulisema kwamba hii nchi kila kitu kiko kwenye katiba na sheria zote zimeandikwa sasa ndiyo nikakupa huo mfano ili kuonesha kwamba privileges za jeshi siyo zote ziko kwenye katiba! Kuhusu hatari unafikiri serikali haiioni hiyo hatari mbona matraffic wenyewe hawawaulizi chochote wakiwaona!
Halafu sasa hivi ndiyo unabadilisha unasema eti usifananishe road act na financial laws wakati mwanzo ulisema hii nchi hakuna sheria ambayo haijaandikwa mkuu usifikiri hii nchi pesa za umma zinaheshimiwa kiasi hicho hao unaodhani wanaheshimu pesa za umma ndiyo wanaoongoza kuzichezea! Waliotunga hizo sheria ndiyo hao wanaoongoza kuzivunja!
Kuhusu kuwepo na maluteni walioishia form six jeshini nimekuambia utaratibu unabadilika kulingana na uhitaji wao! Kuhusu wao kuamua kwamba miaka hii wasiwavalishe nyota watu wenye elimu ya form six wanajua wao kwanini wamebadilisha maana wenyewe wana msemo wao kuwa "JESHI HALIKARIRIKI" haswa kwenye masuala ya recruitment!
Kuhusu baba kanituma mkuu narudia hakuna taasisi hii nchi isiyo na baba kanituma hata zile ambazo ajira zinapitia PSRS kama TRA nako wapo na jeshini pia wapo baba kanituma na wasio baba kanituma! Kuhusu takwimu za utalii bado huna hoja umebaki kushikilia hapo kwamba kwanini sikuandika currency wakati currency inayotumika wewe ulitakiwa uijue!
Kuhusu taarifa za google kwani unafikiri mengi uliyoyaandika hapa google hayapo mfano hiyo bajeti ya wizara ya ulinzi kwa mwaka 2021/22 kwamba ni 2.3T unafikiri google haipo au unataka nikuletee huo mchanganuo! Hayo uliyoyaandika mengi yanajulikana mkuu mimi ninakuambia yale ambayo yamefichwa kwetu sisi raia wengi ila utayapata kwa wahusika wakuu tu!
Mkuu vipi? Kuna afisa was tra anaogopa kutaja yuko kitengo gani, nahisi anaogopa maswali ya taxation na customs, na I'm sure ningemuuliza maswali ambayo yange m-discredit
aseeee....Hii mbungi inapigwa hapa na AFISA WA TRA (KARMA) sambamba na MGAMBO wa jiji (SAVEYA) sio ya nchi hii.
- Afisa wa TRA vipi ? wewe si afisa wa tra bwana mbona Muoga? Kwa hiyo ushakubali kwamba maswali huyawezi, by the way unadhani ningekuuuliza maswali mangapi? Kwani nimekwambia lazima upate 100%? hata ungepata 60% ingetosha hivyo basi kwa kuwa umeogopa maswali kwa kitendo chako cha kukataa kujibu maswali, tunahitimisha kwamba wewe ni muoga, na nahitimisha kwamba umeshindwa hii hoja ya KwanzaHaha mkuu unahisi ukisema naogopa au nakimbia maswali ndiyo utanitisha ili nitaje position yangu au? Halafu maswali yenyewe ni yepi ndiyo yale uliyosema kwamba ungeniuliza nisingekuwa na majibu hadi niwapelekee wataalam wa ITA ambao nao baadhi wasingekuwa na majibu kwahiyo unaona sasa kumbe kutokuwa na majibu ya baadhi ya maswali bado isingekuwa sababu ya kunidiscredit kuwa siko TRA bali ni suala la utaalam tu!
Kuhusu kamisheni ya jeshi nimeshakujibu kule juu kuhusu utaratibu wao labda uniambie hiyo sheria unataka kuihusianisha vipi na suala la kwamba hakuna maluteni walioishia form six jeshini naomba unijibu hili! Kwa sababu jibu la kwamba hawapo nilikupa na ulishalikubali hivyo nijibu hiyo sheria ya ugawaji wa kamisheni inahusiana vipi na utaratibu wa sasa ambao hauruhusu mtu aliyeishia form six kuwa ofisa tofauti na zamani!
Kuhusu bajeti mkuu naona unarudi kule kule hivi mtu akikuambia hiyo sheria haipo huelewi au ndiyo unataka kulazimisha kwamba jeshi halina uspecial wala utofauti wowote! Bajeti ya jeshi siyo yote inayochapishwa nyingine inafichwa na wala hakuna sheria inayoruhusu huo ni upendeleo ambao jeshi limepewa na serikali hata kama wanafanya makosa ila wao ndiyo wameshaamua hivyo kwa sababu jeshi lina usiri hata kwenye baadhi ya matumizi!
Ni wapi nimesema taarifa za jeshi nimegoogle hebu nioneshe na kuhusu kukutajia exactly mwaka ambao huo utaratibu ulianza naomba unijibu inahusiana nini na kutokuwepo maluteni walioishia form six jeshini au ndiyo ukiishiwa hoja unaamua kuzalisha maswali mapya hata ambayo hayahusiani ili tu usikubali kuwa jibu ulilopewa ni la kweli! Kuhusu taarifa za jeshi sigoogle nimeambiwa na baadhi ya maofisa ninaowafahamu!
Unasema wanajeshi waliwahi kukemewa kwahiyo kwa akili yako unadhani kuwakemea tu inatosha nimekuuliza mbona matraffic wenyewe wakiwaona barabarani hawawasimamishi wala kuwauliza chochote je ni sheria gani kwenye road act inayoruhusu wao kufanya hivyo? By the way nikikuuliza privileges zote za maofisa wa jeshi hasa wale general officers zilizoandikwa kwenye sheria unaweza kunitajia zote mkuu?
Kuhusu takwimu za mapato ni wapi niliposema kwamba benki kuu wao hawakuandika currency wakati ni mimi ndiyo ambaye sikuandika currency niliandika tu amount na kwa vile wewe una 'uelewa mkubwa' nilitegemea ungeelewa nilichomaanisha au siyo brother? Kuhusu uwazi nimekuambia kote PSRS na jeshini kuna kina baba kanituma na kuna wale wa individual efforts so kama ni uwazi hata jeshi lina uwazi maana siyo wote ni baba kanituma!
Mimi sigoogle kwa sababu siiamini google kwa asilimia zote ndiyo maana nikakuambia ningetaka kupata hizo taarifa unazonipa ningeamua tu kugoogle ila ni kwa sababu najua google siyo the most reliable source of information! And ofcourse kuna baadhi ya taarifa kuhusu jeshi nazipata kwa wahusika wakuu tu ambako kwingine kote sizipati wala sijawahi kuzisoma kwenye sheria yoyote ile ya nchi hii sababu hazipo!