Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Klabu ya Azam Fc imetoa gharama kwa timu zenye kutaka kukodi na kuutumia uwanja wake wa Azam Complex pale kwenye maskani yao Chamazi.
Mazoezi kwa timu inayotaka kutumia uwanja huo kwa siku moja ni Shilingi laki sita ( 600,000 ) bila taa.
Ukitaka kufanya mazoezi na taa (usiku) basi utalazimika kulipa Shilingi Milioni Moja na Laki Tano kwa siku moja tu.
Ukitaka kucheza mechi pale kama anavyofanya Yanga, basi utalazimika kulipa Shilingi Milioni Tano na Laki Tisa tu. (5,900,000 ) na haijalishi mechi iwe mchana au usiku gharama ni hiyo.
Kwa timu za nje ya Tanzania gharama ya mazoezi ni Dola Elfu Moja ambazo ni sawa na karibu Milioni Mbili na Laki Tano.
Huku timu ya nje ikitaka kucheza hapo Azam Complex watalazimika kulipa Dola Elfu Tano sawa na Tshs Milioni 12 na Laki Tano.
Safi sana Azam Fc endeleeni kufanya maokoto maana timu hamna walau maokoto yapunguze gharama za uendeshaji wa timu.