Hizi ndizo sababu za kutopokea simu za baba yangu mzazi

Hauko pekee yako maelfu ya vijana wa kitanzania wanapitia hali kama yako including me.
Bado hapo hujaanza kutafutwa na wadogo zako shida zao zote watazielekeza kwako.
Kama una roho ndogo utajikuta na line ya simu unatupa. Nyerere alizingua sana kutuletea ujamaa haya mambo ya mtu kuishi kutegemea kwamba kaka yangu au dada yangu au mtoto Wangu yupo mahali fulani atakuja kunikomboa au kunitumia pesa ndio yanazidisha kizazi masikini.
Shida yako nyingine naona nikama umeruhusu mambo yakiimani yakutawale dunia ya sasa inahitaji Ubunifu na ufanyaji kazi hayo mambo sijui laana ,baraka yaweke kwanza pembeni yatakuchelewesha.
Kuhusu betting ni bora ungetulia kwanza ukipata ajira au biashara ya kueleweka utarudi kuendelea maana muda ambao unatakiwa kuwaza kazi za maana utajikuta unapoteza kwenye kufuma mikeka.
 
This piece of advice is second to none.Very superb indeed!
 
Pole mkuu kwa unayoyapitia, nimeifeel na kuiona imani yako kwangu uliyonayo kwenye swala la Code ninazoziweka,

Nitaongeza Umakini, NAOMBA WEKA CODE ITAKAKAYOKUWA NA HEADING "KIMKAKATI "

Code nyingi ninazotupia humu huwa ni "Kuza Cashout code"

Hizo kuza Cashout naziweka nyingi sana humu... so don't take them seriously... ili usipoteze pesa! Maana huwa natenga 10-15k kwa hizo kuza cashout code

almost kila baada ya siku moja ama2 kutegemeana na ushindi wa code za KIMKAKATI, by then hizi wiki 2 ama moja na nusu nimepoteza sana pia, UPEPO ZIWANI SIO MZURI!.
 
Mkuu kusema kurudi mbeya uwongo..
Ila upande wa mama nipo nae vizuri sana kabisa huyu mama kila siku naongea nae..

Nilichogundua pia kutengana kwa wazazi inaweza kuwa ni chanzo cha mtoto ku base upande mmoja
1. Ufunguo wa mafanikio yako umeushikilia mwenyewe

2. Ufunguo wa mateso na shida zako unao mikononi mwako

3. Ufunguo wa kwenda kuzimu bila kuacha historia nyuma unao wewe

4. Ufunguo wa kupata baraka na amani na historia njema unao wewe

UFUNGUO HUO NI BABA YAKO MZAZI NA MAMA YAKO MZAZI
-UTACHAGUA MATUMIZI YA HUO UFUNGUO MWENYEWE (KWA WEMA NA AMANI AU KWA KUKUMBUKA MABAYA NA KULAANI NA KUZIRA)

HUWEZI KUMZIRIA MZAZI UKATOBOA, LABDA HUKO MBEYA.

USHAURI: ukihisi kuwa utatofautiana na mzazi wako jifunze kunyamaza kuliko kumziria.
 
Pole mkuu...
Me nmeingia mbeya leo kama bado upo southern,njoo pm nikupe contact tuonane kesho pengine tutapata pa kuanzia kwa pamoja
Daaah mkuu asante sana kwa ukarimu wako..
Mzee ndio yupo mbeya ila mimi nipo dar es salaam
 
Daaah mkuu acha kabisa ni kweli hapo wadogo zako bado hawajakutafuta wanasema ishu za madaftari.

Ukitupa line ukawa upo off mana yake utampa presha zaidi an mkuu huwa nabadilisha line kila leo ila wapi sio solution..

Nipo hapa natulia nijue na solve vipi hii ishu
 
Ila jitu bandia bana daaah yaani kwenye mambo ya betting lazima uwe seriously ume bold kabisa hapo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Nina imani na wewe mkuu huwa nikija kule nachukua code za kukuza cash out hvo hvo tunasogeza siku.

Japo wanasema huku kunapoteza pesa ila kiukweli pesa nayompa muhindi hata nikisema niwekeze leo mpaka nipate milion basi nitatumia miaka 20
 
less is more, jitahidi uwe unatuma home hata 50k tu kwa mwezi consistently jimotivate
Kuna kipindi nilikua nafanya hvo mkuu Niliweza manage hiyo ila.kwa sasa just imagine kama hiko chumba nachokaa kwa mwezi haifiki 50k...

An mambo ni complex mkuu
 
Asante mkuu kwa maneno yako ya busara kwangu na naamini tachukua haya kama funzo kwangu..

Na nitayakumbuka daima

HUWEZI KUMZIRIA MZAZI UKATOBOA,

USHAURI: ukihisi kuwa utatofautiana na mzazi wako jifunze kunyamaza kuliko kumziria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…