Ngoja nieke kitu sawa, Anga la israel linalindwa na safu tatu, Arrow systems(1,2,3), David's sling na ya mwisho ndio hio "iron dome". Makombora ya masafa marefu yanayopita umbali wa juu sana yanazuiwa na arrow system, ya saizi ya kati na David's sling, na makombora madogo short range yanazuiwa na iron dome. Iron dome haiwezi kuzuia ballistics missile hivo yanazuiwa na arrow system. Makombora yaliorushwa na iran yalikuwa ni hypersonic ballistic missiles kwahiyo mengi yalizuiwa na arrow system na sio iron dome, teknolojia ya arrow system itaruhusu bomu lipite kama litaenda kutua sehemu ambayo haina shida, bomu kama linaenda kutua katikati ya jangwa haina haja ya kulizuia. Mabomu mengi ya iran yalitua jangwani, mengine kwenye open space tu, yaliolenga kwenye makazi yalizuiwa