Hizi ndizo Shahada za Heshima na Tuzo alizotunukiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Lakini akaiacha Nchi kwenye umaskini mkubwa
Ya nchi ilibaki kwenye umaskini mkubwa,lakini aliituachia gesi,madini,mafuta,
Zama zake zilikuwa za ukombozi wa Afrika,sasa nyie ambao hamna hata vita ya kupigsna ukiacha matumbo,
Marumbo yenu,Wakati wa Nyerere kulikuwa na wahandisi,ma injinia hata 20 hawafiki,sasa hv,tekinolojia ipo,rasilimali zipo,wasomi kibao,lakini hawana tofauti na chifu mangungo wa msovelo!!kizazi baada ya 1999 mmefsnya nini?
 


Nani alikuambia Nyerere alipigania uhuru wa nchi hii??--- na Jomokenyatta alifanya nini??, Samora, Mandela, Mugabe nk hao walifanya nini??.

Nyerere alipewa nchi na Waingereza, just simple.
 
Nani alikuambia Nyerere alipigania uhuru wa nchi hii??--- na Jomokenyatta alifanya nini??, Samora, Mandela, Mugabe nk hao walifanya nini??.

Nyerere alipewa nchi na Waingereza, just simple.
Wewe hata historia ya nchi yako huijui ila lwa vile unaweza kushika keyboard na kutype basi umdona na wewe uandike.
 
Wewe hata historia ya nchi yako huijui ila lwa vile unaweza kushika keyboard na kutype basi umdona na wewe uandike.


The cooked history!!---Koloni la Tanganyika baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia lilikabidhiwa kwa Waingereza kutoka kwa Wajerumani ni likaitwa the British protectorate ili baadaye tujekupewa uhuru wetu hii ni tofauti na Kenya na uganda ambao Wao walikuwa ni British colonies, Nyerere aka take advantage hiyo na mchakato ukafanyika wa kwenda UNO nk, na akapewa nchi kiulaini tofauti na wenzetu Kenya nk, waliomwaga damu kupigania uhuru wao, sasa Utasemaje Nyerere alipigania Uhuru, kupigana unakujua??!🤣
 
Hovyo kabisa huyo banana yenu


Alichojua ni kunyang'anya watu majumba yao na mashamba yao bila fidia na kuzifanya mali za taifa (utaifishaji/Azimio la Arusha), hapo ndipo laana ilipoanza., Baadaye wakaja watu wenye akili wakaliua hilo Azimio na sasa hatumo tena kwenye misingi ya katili ya kijamaa.
 
Ujamaa haukumuangusha bali kilichomuangusha ni kujitolea sana kuzisaidia nchi zingine zijitawale na baadaye ile vita na Iddi Amin ikahitimisha!
Mwalimu alianza vizuri sana, and I'll always respect him for that lakini ni yeye mwenyewe ndie alikuja kuyavuruga yale ambayo alikuwa ameyaanzisha!!

Hakika, sumu kubwa ya uongozi ni kubaki madarakani muda mrefu!

Lau kama Mwalimu angeanzisha mfumo wa kisiasa ambao, let's say angetoa miaka 5 ya mpito, na bada ya hapo ikaanza 5 to 10 years terms, basi angetoka madarakani akiwa ameacha heshima kubwa sana kiuchumi!

Na kwa upande mwingine, Ujamaa ulimwangusha kwa sababu Ujamaa unahitaji ubabe kwa wanaochezea mali za umma wakati Mwalimu ubabe wake aliufanya kwa wale waliomchezea kisiasa!

Haya mambo ya anayeharibu hapa anahamishiwa kule yalianza tangu enzi za Mwalimu, matokeo yake, hadi anatoka madarakani mashirika yote aliyokuwa ameanzisha yalishakuwa ICU!
Matatizo yakaanzia hapo baada ya wakubwa huko Duniani kumlazimisha Mwalimu ashushe thamani ya pesa ya Tanzania ndio wakubali Nchi ikopeshwe na IMF na World Bank hapo Mwalimu akakataa
Alikataa bila kuwa na sababu za kiuchumi kwa sababu ni kweli shilingi yetu ilikuwa overvalued!

Nchi haikuwa na uwezo hata wa kuwa na viberiti, inaanzaje kuwa na currency yenye thamani kubwa kama ile?! Tulikuwa tuna-export nini cha ku-influence stability ya sarafu yetu?
ndipo matatizo yaongezeka!!
Matatizo yalishaanza kitambo na ndo maana Bretton Woods wakataka kutunasua kwa mikopo!
Lakini kabla ya hapo maisha yalikuwa mazuri na rahisi sana !!
Unazungumzia wakati gani?!

Kwanza, moja ya sababu ambazo zilianza kuvuruga kabisa uchumi wetu ni Vita vya Kagera! Ukiifuatilia vizuri Vita vya Kagera utaona wazi kama Mwalimu asingekuwa na mahaba ya wazi kwa Obotte basi ile vita wala isingetokea!

Lakini kwavile alimuona Amin ni muhuni asiyefaa kuongoza nchi, na kwahiyo Obotte alistahili kurudishwa madarakani, hapo ndipo Mwalimu "akanunua" ugomvi ambao wala haukutuhusu!
Sisi tulikuwepo lakini ninyi wengi mnahadithiwa tu !!
Ina maana huwezi kuuelezea Mkutano wa Berlin kwa usahihi kwa sababu tu wakati huo hukuwepo?!
 
Lakini akaiacha Nchi kwenye umaskini mkubwa
Nyerere hakuiacha nchi kwenye umaskini mkubwa kuliko huu ulioko sasa. Wacha wanachanganya kwani wakati ule mambo kwa nchi zote yalikuwa ni tofauti na sasa. Wakati wa Nyerere watu walikuwa wanasoma bure, wanatibiwa bure na kulikuwa na nyumba za National housing kwa wafanyakazi. Wanafunzi walikuwa wanasafiri bure kwa kutumia ''warrant''. Tulikuwa na mashirika ya umma mengi. Watoto wa maskini walikuwa wanasoma bure na kugombea nafasi za kiasiasa hakuhitaji uwe na fedha. Kiwango cha elimu kilikuwa juu ukilinganisha na sasa.
 
Nilibahatika kutembea nchi za Scandinavia hususani Finland na Norway. Nilichogundua ni kuwa mfumo wao wa maisha hauna tofauti kubwa sana na ule ambao Nyerere alikuwa ameujenga. Kwa mfano nchi kuwa na mashirika na viwanda vya umma, kuhakikisha wananchi hawapishani sana kwa vipato hivyo nchi kutokuwa na matabaka ya matajiri sana na mafukara sana. Tangu kipindi hicho nimekuwa najiuliza: yale mashirika ya umma na viwanda vyote alivyoanzisha Mwalim mbona vilikufa lakini huku vina maendeleo mazuri? Inawezekana tatizo likawa ni watu na siyo mfumo? Kwamba sisi waafrika, hususan watanzania, hatuna uwezo wa kujitawala hivyo chochote tunachaanzisha hakidumu? Mbona basi nchi za Scandinavia wamefanikiwa? Je, ni sahihi kumlamu aliyeanzisha wakati sisi ndiyo tuliharibu?
 
Mwalimu Nyerere kaiachia Tanzania utajiri na heshima kubwa.
Unaposhindwa kujua hilo ilaumu akili yako iliyolala.
Mkuu asante sana. Watu wenye uelewa mpana kama wewe wanahitajika sana kwenye kufundisha hiki kizazi cha sasa kinachopenda ''short cut'' kuwa Nyerere alifanya makubwa ila sasa watawala wanashindana kuiuza nchi. Hivi wanadhani kama angekuwa ni mfano Kikwete au Samia aliyetuongoza kipindi chote cha Nyerere tungekuwa kwenye hali gani sasa hivi? Kuna fukara ambaye angekuwa na uwezo wa kumilika hata ekari mbili?
 
Hata Mkapa hakujiita Dr Mkapa! JPM alikuwa na PHD ya darasani, Mwinyi hakujiita Dr Mwinyi! Ila JK na Mama Samia hiyo title inakoma [emoji2]

Mwl Nyerere alibakia na title ya Mwl na ni mwanazuoni first class.
Siku zote debe tupu haliishi kuvuma. Nchi yetu ngumu sana. Mimi wakati mwingine naona aibu mwenyewe jinsi viongozi wanavyo-force kuitwa hizi tittle za u-dr.
 
Unapoteza muda wako bure kujadiliana na hiki kizazi ambacho hata mambo yaliyotokea mwaka jana wameshasahau. Tatizo kubwa ni elimu yetu. Watu wanakariri kujibu maswali na siyo kuwa wadadisi. Katika nchi ambazo raia yake wengi hawajui historia ya nchi yao ni Tanzania. Mtu hata jambo lililotokea wakati wa Nyerere atakuambia hajui eti kwa sababu hakuwepo wakati wenye akili wanajua mambo yaliyotokea miaka bilioni iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…