Mwanaume uliambiwa utakula kwa jasho lako ila mwanamke hakuambiwa hivyo kumhudumia mwanamke ni jukumu lako na ndo maana akaambiwa akutii na akuheshimu
Usidhani aliambiwa akutii na akuheshimu hivi hivi tu wakati haujamuumba wala haujamzaa aliambiwa akutii na akuheshimu kutokana na wewe kumhudumia kifedha kama ambavyo unahudumia watoto wako
Majukumu ya mwanamke yanajulikana ni kufanya kazi za nyumbani na kukulea wewe pamoja na watoto wenu na majukumu yako yanajulikana ni kutafuta pesa na kumhudumia mke wako na watoto wenu
Ndo maana mwanamke anaambiwa katika swala la malezi mtoto wake wa kwanza ni mume wake vivyo hivyo hata katika swala la huduma mtoto wako wa kwanza ni mke wako sasa ukitaka mkeo akusaidie kutafuta pesa ina maana na wewe utakuwa unamsaidia kufanya kazi za nyumbani si ndiyo?
Mithali 31:10-31 SRUV
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.
Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.