Hizi ni bidhaa za Kenya zilizoweza kuteka soko Tz kwa muda mrefu, ongeza nyingine

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
BLUE BAND - watanzania wengi hawalijui neno la siagi, msamiati wa siagi umekuwa blueband kwasababu ni bidhaa iliyoweza kupata umaarufu kwa muda mrefu sana, hii kitu ikipakwa kweye mkate ushushie na chai ni ladha amazing sana.


KIWI - vile vile nayo imekuwa msamiati rasmi wa rangi ya kungarisha viatu, ni kwa muda mrefu sana wamekamata soko na sisi wateja tumeridhika, kwenye maandalizi ya kufungua shule hii bidhaa haikwepeki


KASUKU KIBERITI - Unapozungumzia kuwasha moto watanzania wengi tumezoea kiberiti na kiberiti maarufu ni Kasuku, Matumizi yake ni mengi sana kuanzia kuwasha jiko, kuchoma taka, kuvuta sigara, kuwasha mishumaa, n.k.



GOOD MORNING (dawa ya kikohozi) - hii dawa ipo mpaka leo kwenye maduka lakini ipo tangu muda mrefu, dozi yake ni kimfuniko chake mara 3 kwa siku ila uwe makini uweke mbali na watoto maana ni tamu wanaweza kunywa yote kwa mpigo.


VASELINE (Mafuta ya mwili) - losheni na mgando mafuta ya ngozi, watoto, nywele, n.k. ubora wake umeweza kujijengea jina na kuwa chaguo la watu wengi kwa muda mrefu.


OMO (kabla yake kulikuwa na aerial) - ni sabuni iliyoweza kuteka soko kwa muda mrefu, ni gharama kuzidi sabuni nyingi zenye ujazo mkubwa kwa bei chee, soko lake ni kwa wateja wanaojali zaidi ubora kuzidi ujazo,


PIPI, Big G na pipi kali, - Msamiati mwengine tunaotumia kwajili ya bidhaa maarufu za Kenya ni big g, Kwenye pipi kuna kifua na machungwa, kuna PK maarufu kama pipi kali. kuna watu wana survive kwa kuuza hizi bidhaa pekee wameziweka kwenye ungo maeneo ya stendi, watoto wanazipenda, zinatumika kukata harufu, n.k.
 
Nchi inapata faida kubwa sana kwenye viwanda hata kama wamiliki ni kampuni ya nje.
  • Kenya inapata kodi zaidi kuanzia kodi za vat ya soko la ndani, kodi za kuuza bidhaa nje ya Kenya, kodi za viwanda, kodi za waajiriwa, n.k.
  • Kenya inatangazwa kupitia bidhaa
  • uchumi wa Kenya unazidi kuongezeka, wanavyotuuzia sisi (exports) vinazidi tunavyowauzia (imports).
  • Wakenya wengi wamepata ajira kuanzia mameneja, wahasibu. it, madereva, n.k. mfano Kampuni kama unilever ni ya ulaya ina viwanda Kenya na hata kwetu ipo Mufindi wana kiwanda vya chai, wananchi wengi wameajiriwa na kulipwa kizungu.
  • Jamii za karibu na viwanda zinanufaika kwa misaada kama kujengewa shule, kliniki, mikopo, n.k. (corporate social responsibility)
  • Kenya inanufaika na soko la rasilimali walizonazo zinazohitajika kutengeneza bidhaa viwandani, mfano mchanga, pamba, maji, n.k.
  • wawekezaji wanazidi kujaa Kenya, Kijana Bilionea wa kitanzania Fernandes mmiliki wa Nala kahamishia shughuli zake Kenya kavutiwa na mazingira ya uwekezaji, mambo ni chap chap
 
Japo radha ya blue band ya zamani ilikuwa nzuri zaidi na Lung tonic tulikuwa tunakunywa na kupona sijui kwa sasa
 
Mchina ndio kalikamata Soko kwasasa
 
Hizo bidhaa zote za kampuni za wazungu Kenya waingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…