Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Kuna kona moja matata kutoka Mbeya kuelekea Malawi imepewa jina Uwanja wa ndege ni balaa,R.I.P nyingi zilipatikana pale hasa kwa wageni enzi hizo hadi kuna kibao cha onyokali,punguza mwendo,tembea taratibu[emoji591][emoji591][emoji591][emoji591]
Mbona ni pa kawaida sana pale...Ni Tukuyu ile ukiwa waitafuta Kiwira kama unatoka Mbeya
 
1. Kona za Iyovu - ukitoka tu mikumi kuelekea iringa utaziona Kona hizi, ni Tamu Sana

Hizi nazo hazina shida yoyote, ukiwa mzoefu unatembea hata zaidi ya 110kph na ni usiku bila hata kuogopa vicheche...(angalizo maeneo yoyote yenye kona kali usijaribu kwenda kasi kama hujui barabara)
 
Hiyo barabara(uyole-Tukuyu- kyela). Nimeipita, ila huwa sioni Kona za kuogopesha au kwasabb huwa niko na uchovu.
 
Mi nashangaa watu wanafananisha eti na mburu kusiko hata na maporomoko,

Watu wengi wanaoenda Mbulu hua wanapitia Karatu ambapo njia hiyo japo ni rough road ila haina shida. Barabara tunayoizungumzia hapa ni shortcut kutoka Mbulu, kupitia Magara kuja kutokezea sehemu inaitwa Mbuyu wa Mjerumani ambapo unakutana na main road ya kutoka Arusha kwenda Babati. Hii barabara niseme kwa Tanzania, Afrika mashariki na nchi za SADEC jumlisha na maziwa makuu kusini mwa jangwa la Sahara ndio inaheshimika kwa kona kali sana kupita maelezo!!! Mbaya zaidi barabara inapita juu ya mlima ambapo PANDE ZOTE ZA BARABARA NI MAPOROMOKO MAKALI!! Kama unaendesha gari, yaani hata ukiwa spidi 10 bado utajiona uko spidi kali sana, na hakuna kabisa uwezekano wa magari mawili kupishana..!!!! Hii ndio barabara pekee ambayo madereva hua wanapaki magari katikati ya barabara ili wapumzike na kufuta jasho kwenye mikono, miguu hadi kwenye meno.







 
Mombo-Soni-Lushoto,
Mara ya kwanza waweza useme huku sirudi tena.View attachment 1764642
Hizi kona nilipita na shambalai bus 2009 sio mchezo kabisa na madereva vichaa wanalaza gari kana kwamba hajali kuwa lolote linaweza kutokea, Na mambo yaende Sawa angalau usichungulie upande wa bonde .
risk kubwa ipo wakati wa kuteremka mlima
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Hizi breki za miguu kumbe tupo wengi [emoji1787][emoji1787]
 
Kona za kutoka Njombe - Madaba - Songea
 
Zile Kona za mtera ni kufuru[emoji23]
Halafu haziishi haraka tofauti na kitonga dk chache tu pameisha.
Zile nusu saa inaisha bado hazijaisha na hapo gari ipo speed Sana.

Zile Kona ilifika mahala nikazizoea,,Kama hujakaa siti ya dirishani unaweza kudondoka aisee[emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Nazo ziko kama kitonga,pembeni korongo.
 
Kona za Lushoto Mombo
Miaka hiyoooo kabla ya barabara kuchongwa ilikuwa balaaa Tumelala sana kwenye hii njia. Maporomoko ya mawe mvua zikinyesha balaa. Ukifika Soni unapumua kidogo kuanzia pale kuitafuta Mombo mmh ni Mungu tu. Tulikuwa tunawacheka sana wasambaa eti miguu imekomaa sababu ya milima. Kwenda Gare usipime lakini all in all kuna ardhi yenye rutuba sana.
 
Nyang'oro( Iringa- dodoma ) , ni shida, kile kipande kina kilometers kaa 28 toka unapozianza zile kona hadi unapozimaliza , na inasemekana zile kona zipo kaa 300. Nanikona za bampa to bampa kweli .

Basi kuna jamaa anaitwa ustadhi ( dereva fuso tandam ) huyu mjomba huwa inazila zile kona speed ikisoma 60 km / h kwenye dash board mi hupaki tu nimeshikilia roho yangu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…