Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hiyo sehemu ni hatari mno, ukimaliza Kona unasali na kushukuru Mungu
 
Unakutana na Chakito Longway au Shambalai Apache zinashuka speed ziwahi abiria Mombo. Hiyo Chakito ni Fuso body za kuchonga anavyoshuka unajiuliza mwamba anajihamini nini?
 
Aisee sijapita hii njia na wala siwish kuipita😀 mambo ya kuminya breki kama mimi ndiye dereva sitaki😀
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Hizi breki za miguu kumbe tupo wengi [emoji1787][emoji1787]
Hatari sana na kujishikilia kwenye kiti kwa nguvu huku ukiminya breki😀😀😀 maisha ni matamu haya jamani ijapokua tunalalamika hamna pesa maisha magumu ila when it comes to uhai mmh full mabreki kama dereva😀🙌
 
Morogoro kuna Njia ya kutoka Mlali kwenda Mgeta Kibaoni kuna mlima hatari kuna Kona kali na miinuko mikali pia wameweka kalavati za kupitisha maji kwa juu na njia ni nyembamba. Kama dereva mgeni akipita na gari manual atapata tabu Sana.Ukienda mbele zaidi utakutana na vilima huko Nyandira.
 
Kuna milima na kona za hatari huku goba...
Jamaa yangu alikuwa hajawahi kupita Goba road. Siku katoka na Washkaji wakapita njia hii pale kwenye kilima Cha Mount Kibo Primary mpaka Kayuni gari yake Nissan March ilikosa nguvu akapanda kibishi.

Sasa akawa anasimulia amekutana na kilima Kikali Sana Dar, watu wakawa wanamcheka Sana wanamwambia kapanda Kitonga ya Dar na yeye ni Mwanadarisalama hajawahi kwenda Mkoa maisha yake yote.
 
Sababu ile ni njia ya pembezoni hivyo magari ni machache tofauti na Kitonga ambayo nikm geti la kuingilia nyanda za juu kusini na nchi jirani

Unaweza toka Mombo hadi Lishoto usipishana na lori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…