Hizi ni sababu zangu kuu tano za kwa nini sitampigia kura Samia Suluhu Hassan kama atasimamishwa na chama chake

Msitari wa pambizo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
3,098
Reaction score
5,451
Niende moja kwa moja. Ikiwa CCM watamsimamisha Samia kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu 2025 sitampigia kura yangu kwa sababu zifuatazo.

1. Matukio ya utekaji yanaongezeka siku hadi siku. Sijui anajisikiaje kuachanisha familia za watu, kuwaacha watoto bila wazazi kwa kuteka na kupoteza watu. Ni kawaida kwa nchi sasa mtu kupotea na kupoteza maisha kabisa alaf polisi wakasema hawana taarifa naye. Ni kawaida mtu kurepotiwa kwamba ametekwa na polisi hawana taarifa baadaye utasikia alikua mikononi mwa polisi. Huu ni ukatili wa Samia

2. Kuongezeka kwa tozo. Katika kipindi chake tozo katika miamala ya simu imekua kero, mbaya zaidi hatuoni ni wapi fedha hzo zinaenda. Nachelea kusema kuna genge linatafuna fedha hizo.

3. Kubinafsisha bandari kama si kuuza kabisa ni jambo ambalo linakera sana. Kwa sababu pamoja na bandari kuchukuliwa na DP world bado hakuna ahueni yoyote. Kama ume import gari kipindi cha karibuni utakubaliana na mimi kwamba charges zimeongezeka sana.

4. Mfumuko wa bei wa bidhaa mbali mbali hasa zile bidhaa muhimu. Katika nchi hii bei ya sukari iko juu pengine kuliko nchi yoyote jirani inayotuzunguka. Ameshindwa ku conroll hilo. Ajabu na kweli ni pale ambapo bei ya mafuta nchini kwetu ukilinganisha na nchi jirani ambazo zina import mafuta kupitia bandari ya DSM ni ndogo kuliko sisi

5. Wizi serikali na nidhamu ya hovyo imezidi mara dufu. Report ya CAG kila ikitoka lazima ije na report za ufujaji wa fedha uliokithiri. Kwa miaka hii imekua kawaida sana na huoni hatua zikichukuliwa. Zile kauli za 'utanijua mimi ni nani' zimerudi kwa kasi, yani unaweza kudhulumiwa haki yako na hakuna kitu utafanya.

Sitampigia kura Samia 2025. Kama una ungana nami ongeza mengine. Na kama huungani nami prove me wrong.
 
Umenena vema.

Ongezea na:

Kupora mbuga mbalimbali za wanyama na hifadhi za misitu, na kuwagawia waarabu, kwa maslahi ya kundi la uporaji.

Unamgawia mtu mbuga ya wanyama, eti ni mwekezaji! Anawekeza kitu gani? Anaenda kuwazalisha simva? Unamgawia mwarabu wa jangwani hifadhi ya msitu, anaenda kuwekeza nini!! Anaenda kutengeneza mininga na mitundu?

Kama unaipenda Tanzania, Tanganyika na watu wake, hakika huwezi kuwapigia kura hawa watu wa CCM ambao wamegeuka kuwa madalali wa kuuza nchi kwa waarabu. Unapopora rasilimali za nchi na kuzigawa kwa wageni kwa maslahi ya yako na watu wako, huko ni kuwatia utumwani wananchi wako. Maana ukweli ni kuwa mtu dhaifu kiuchumi hawezi kuukataa utumwa.
 
Hata usipompigia bado atashinda tu uraisi. Hapa umejichosa bure kuja kuandika mambo ambayo hayatokuwa na tija yoyote katika uchaguzi.

Enzi za chama kimoja, kuna watu ambao hawakuwa wanapiga kura, lakini raisi alipita kupitia wale wale wachache waliompigia kura.

Enzi za vyama vingi kuna watu hawakumpigia kura Mkapa, lakini alipita na kuongoza nchi kwa miaka 10.
Enzi za Kikwete ilikuwa ni mshike mshike kweli kweli, lakini mwisho wa siku Kikwete kashinda chaguzi zote na kukaa madarakani miaka 10.

Wakati wa uchaguzi wa 2015, kulikuwa na amsha amsha pamoja na propaganda zaidi ya hizi ulizoandika hapa, vyama viliungana, wapinzani wenye mvuto mkubwa pia waliungana hadi kupelekea wapinzani hao kuanza kupanga kabisa baraza lao la mawaziri kabla ya uchaguzi.

Mgombea wao akawambia mabisa kuwa wasiposhinda uraisi hiyo 2015, ndo basi tena hawatokuja kushinda mpaka miaka 50 mingine ipite. Lakini mwisho wa siku CCM ikashinda na Magufuli akawa raisi kwa muhula wa kwanza na wa pili ambao ulileta matokeo yaliowaacha watu wengi midomo wazi kutokana na shutuma nyingi alizopewa kabla ya uchaguzi kupitia ndani ya chama chake, na upinzani.

Hivyo hata hiyo 2025 bado Samia ataendelea kupeta tu kama kawa. Angalau kidogo 2030, kwa vile atakuwa sio yeye raisi ndo mgombea wa kiti. Hivyo mgombea mpya ataweza kukumbana na challenge za hapa na pale.
 
Umenena vema.

Ongezea na:

Kupora mbuga mbalimbali za wanyama na hifadhi za misitu, na kuwagawia waarabu, kwa maslahi ya kundi la uporaji.

Unamgawia mtu mbuga ya wanyama, eti ni mwekezaji! Anawekeza kitu gani? Anaenda kuwazalisha simva? Unamgawia mwarabu wa jangwani hifadhi ya msitu, anaenda kuwekeza nini!! Anaenda kutengeneza mininga na mitundu?

Kama unaipenda Tanzania, Tanganyika na watu wake, hakika huwezi kuwapigia kura hawa watu wa CCM ambao wamegeuka kuwa madalali wa kuuza nchi kwa waarabu. Unapopora rasilimali za nchi na kuzigawa kwa wageni kwa maslahi ya yako na watu wako, huko ni kuwatia utumwani wananchi wako. Maana ukweli ni kuwa mtu dhaifu kiuchumi hawezi kuukataa utumwa.
Wewe zero brain unaongea kwa mihemuko hujui kitu rudi shuleni.
 
Hata usipompigia bado atashinda tu uraisi. Hapa umejichosa bure kuja kuandika mambo ambayo hayatokuwa na tija yoyote katika uchaguzi.

Enzi za chama kimoja, kuna watu ambao hawakuwa wanapiga kura, lakini raisi alipita kupitia wale wale wachache waliompigia kura.

Enzi za vyama vingi kuna watu hawakumpigia kura Mkapa, lakini alipita na kuongoza nchi kwa miaka 10.
Enzi za Kikwete ilikuwa ni mshike mshike kweli kweli, lakini mwisho wa siku Kikwete kashinda chaguzi zote na kukaa madarakani miaka 10.

Wakati wa uchaguzi wa 2015, kulikuwa na amsha amsha pamoja na propaganda zaidi ya hizi ulizoandika hapa, hadi kupelekea wapinzania kuanza kupanga kabisa baraza lao la mawaziri kabla ya uchaguzi. Lakini mwisho wa siku CCM ikashinda na Magufuli akawa raisi kwa muhula wa kwanza na wa pili ambao ulileta matokeo yaliowaacha watu wengi midomo wazi kutokana na shutuma nyingi alizopewa kabla ya uchaguzi kupitia ndani ya chama chake, na upinzani.

Hivyo hata hiyo 2025 bado Samia ataendelea kupeta tu kama kawa. Angalau kidogo 2030, kwa vile atakuwa sio yeye raisi ndo mgombea wa kiti. Hivyo mgombea mpya ataweza kukumbana na challenge za hapa na pale.
Hawashindi bali wanatangazwa.
 
Hawashindi bali wanatangazwa.
Ni kawaida ya kila anaeshindwa kujificha katika kimvuli cha kuibiwa au kuonewa kwenye uchaguzi. Hivyo sishangazwi na jibu lako maana hata Trump pia alilalamika kuibiwa baada ya kushindwa.
 
Wewe zero brain unaongea kwa mihemuko hujui kitu rudi shuleni.
Wewe kwenye namna unavyoandika tu, huna sifa hata ya kuwa mwanafunzi wa darasa la mwalimu wa sekondari, achilia darasa la jwangu mimi.

The forum was intended for only high brains but unexpetedly has been corrupted by you such creatures with crippled minds.
 
Niende moja kwa moja. Ikiwa CCM watamsimamisha Samia kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu 2025 sitampigia kura yangu kwa sababu zifuatazo.

1. Matukio ya utekaji yanaongezeka siku hadi siku. Sijui anajisikiaje kuachanisha familia za watu, kuwaacha watoto bila wazazi kwa kuteka na kupoteza watu. Ni kawaida kwa nchi sasa mtu kupotea na kupoteza maisha kabisa alaf polisi wakasema hawana taarifa naye. Ni kawaida mtu kurepotiwa kwamba ametekwa na polisi hawana taarifa baadaye utasikia alikua mikononi mwa polisi. Huu ni ukatili wa Samia

2. Kuongezeka kwa tozo. Katika kipindi chake tozo katika miamala ya simu imekua kero, mbaya zaidi hatuoni ni wapi fedha hzo zinaenda. Nachelea kusema kuna genge linatafuna fedha hizo.

3. Kubinafsisha bandari kama si kuuza kabisa ni jambo ambalo linakera sana. Kwa sababu pamoja na bandari kuchukuliwa na DP world bado hakuna ahueni yoyote. Kama ume import gari kipindi cha karibuni utakubaliana na mimi kwamba charges zimeongezeka sana.

4. Mfumuko wa bei wa bidhaa mbali mbali hasa zile bidhaa muhimu. Katika nchi hii bei ya sukari iko juu pengine kuliko nchi yoyote jirani inayotuzunguka. Ameshindwa ku conroll hilo. Ajabu na kweli ni pale ambapo bei ya mafuta nchini kwetu ukilinganisha na nchi jirani ambazo zina import mafuta kupitia bandari ya DSM ni ndogo kuliko sisi

5. Wizi serikali na nidhamu ya hovyo imezidi mara dufu. Report ya CAG kila ikitoka lazima ije na report za ufujaji wa fedha uliokithiri. Kwa miaka hii imekua kawaida sana na huoni hatua zikichukuliwa. Zile kauli za 'utanijua mimi ni nani' zimerudi kwa kasi, yani unaweza kudhulumiwa haki yako na hakuna kitu utafanya.

Sitampigia kura Samia 2025. Kama una ungana nami ongeza mengine. Na kama huungani nami prove me wrong.
Ingekuwa kura zinaheshimiwa hapo sawa.
 
Ni kawaida ya kila anaeshindwa kujificha katika kimvuli cha kuibiwa au kuonewa kwenye uchaguzi. Hivyo sishangazwi na jibu lako maana hata Trump pia alilalamika kuibiwa baada ya kushindwa.
Usilinganishe US na huu uchafu wetu hapa. US mgombea akitaka anaoneshwa vielelezo vyote. US kura zinapigwa kwa uwazi, zinahesabiwa na kuoneshwa kwa wapiga kura wote wanaotaka, siyo ile taka taka ya hapa kwetu kuwa mtu akipiga kura anafukuzwa asishuhudue uhesabuji wa kura ili wafanye ushetani wao ule alioueleza Nape. US wana tume huru ya uchaguzi siyo hii takataka ya hapa kwetu ambayo ni kamati ya Rais ya kusimamia uchaguzi.

Wewe unaweza kueleza kwa nini Rais na CCM yake hawataki Tume Huru ya Uchaguzi? Kama unatenda haki, unaona shida gani kuwa na chombo huru cha kusimmaia uchaguzi?
 
Wewe kwenye namna unavyoandika tu, huna sifa hata ya kuwa mwanafunzi wa darasa la mwalimu wa sekondari, achilia darasa la jwangu mimi.

The forum was intended for only high brains but unexpetedly has been corrupted by you such creatures with crippled minds.
Kama high brain ni wewe basi kama taifa tumekula hasara, wewe na akili zote umeshindwa kuelewa tu biashara zinafanyika vipi unapigania watu ambao productivity zero bado wanaleta ndugu za wa masai wa Kenya kuchunga mifugo yao ndani sehemu ambayo inaingiza pesa nyingi katika utalii, Kuna uhaba mkubwa wa mahotel ndio maana bei ziko juu sana. Nini kimefanya idadi ya wa Masai kuongezeka kwa kiasi kikubwa pale kwenye hifadhi. Wa Masai wote wahamiaji waondoke wabaki wale waliokuwa makazi yao original sio vinginevyo.
 
mimi zangu 5 ni hizi

1. Ameshindwa sector ya Afya kwa 86%

2.Ameshindwa kwenye sector ya uchumi wa nchi na kuongeza mianya ya matumizi mabaya ya fedha za serikali na kodi zisizoelewaka na kufanya uchumi wa wananchi kutoeleweka.

3. Amefail kabisa kwenye uongozi wa kimadarakaa kwa wateuzi wake kwa kuwa na washauri wabovu sana haijawahi tokea, na ndio wamemuangusha, hakutumia akili wakati wa kuchagua cabinet ya washauri wake since mwanzo, so ameharibu a lot of secters cas of that thing, hivo ni big no.

4.Sijui ni tamaa ya kupenda easy things, au kukosa akili ya uongozi au ndo washauri wapuuzi, but ameharibu sana kutobalance issue ya mikopo na malipo ya serikali na kupelekea upuuzi wa kodi zisizoleta uafadhari, miradi iso na maana yakipigaji, yani full stupidness kwenye mzunguko wa fedha,so ni big no

5. Suala la uuzwaji na ugawaji ovyo raslimali za nchi bila kujali umuhimu kwa nchi na,wananchi, hana mpango endelevu wowote wa maana kwa nchi, ujinga ujinga tu badala ya kufocus na vitu muhimu, yani ana upuuzi mwingi sana.

sio kwa ubaya au chuki,but kwa issue ya maswala ya kuongoza nchi kwangu ni big no😪
 
Usilinganishe US na huu uchafu wetu hapa. US mgombea akitaka anaoneshwa vielelezo vyote. US kura zinapigwa kwa uwazi, zinahesabiwa na kuoneshwa kwa wapiga kura wote wanaotaka, siyo ile taka taka ya hapa kwetu kuwa mtu akipiga kura anafukuzwa asishuhudue uhesabuji wa kura ili wafanye ushetani wao ule alioueleza Nape. US wana tume huru ya uchaguzi siyo hii takataka ya hapa kwetu ambayo ni kamati ya Rais ya kusimamia uchaguzi.

Wewe unaweza kueleza kwa nini Rais na CCM yake hawataki Tume Huru ya Uchaguzi? Kama unatenda haki, unaona shida gani kuwa na chombo huru cha kusimmaia uchaguzi?
Pale mmatumbi anapojifanya anau elewa mkubwa wa chaguzi za Marekani kuliko Trump ambae ndio anaifahamu Marekani na uchaguzi wa Marekani kuliko mmatumbi yoyote hapa duniani.

Halafu ni kawaida wapinzani kulalamika lalamika miaka yote wanaposhindwa. Hata utapoweka hiyo wanayodai kuwa ni tume huru, wakishindwa watakuja kudai kuwa wasimamizi wao walihongwa na mtoto wa mama Abdul. Kama uchaguzi wao wenyewe wa ndani wanadai kuwa kuna hela za mama Abdul ambazo kiongozi mkuu wa chama cha upinzani amepewa ili kuwadhoofisha wale wenye nguvu wasipite.

Hapa inaleta picha uchaguzi mkuu wakishindwa hata kama tume ni ile wanayoitaka wao bado watakuja kudai kuwa kuna hela za Abdul walipewa wasimamizi wao ili kuhakikisha wanashindwa uchaguzi huo nk.
 
Back
Top Bottom