Msitari wa pambizo
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 3,098
- 5,451
Niende moja kwa moja. Ikiwa CCM watamsimamisha Samia kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu 2025 sitampigia kura yangu kwa sababu zifuatazo.
1. Matukio ya utekaji yanaongezeka siku hadi siku. Sijui anajisikiaje kuachanisha familia za watu, kuwaacha watoto bila wazazi kwa kuteka na kupoteza watu. Ni kawaida kwa nchi sasa mtu kupotea na kupoteza maisha kabisa alaf polisi wakasema hawana taarifa naye. Ni kawaida mtu kurepotiwa kwamba ametekwa na polisi hawana taarifa baadaye utasikia alikua mikononi mwa polisi. Huu ni ukatili wa Samia
2. Kuongezeka kwa tozo. Katika kipindi chake tozo katika miamala ya simu imekua kero, mbaya zaidi hatuoni ni wapi fedha hzo zinaenda. Nachelea kusema kuna genge linatafuna fedha hizo.
3. Kubinafsisha bandari kama si kuuza kabisa ni jambo ambalo linakera sana. Kwa sababu pamoja na bandari kuchukuliwa na DP world bado hakuna ahueni yoyote. Kama ume import gari kipindi cha karibuni utakubaliana na mimi kwamba charges zimeongezeka sana.
4. Mfumuko wa bei wa bidhaa mbali mbali hasa zile bidhaa muhimu. Katika nchi hii bei ya sukari iko juu pengine kuliko nchi yoyote jirani inayotuzunguka. Ameshindwa ku conroll hilo. Ajabu na kweli ni pale ambapo bei ya mafuta nchini kwetu ukilinganisha na nchi jirani ambazo zina import mafuta kupitia bandari ya DSM ni ndogo kuliko sisi
5. Wizi serikali na nidhamu ya hovyo imezidi mara dufu. Report ya CAG kila ikitoka lazima ije na report za ufujaji wa fedha uliokithiri. Kwa miaka hii imekua kawaida sana na huoni hatua zikichukuliwa. Zile kauli za 'utanijua mimi ni nani' zimerudi kwa kasi, yani unaweza kudhulumiwa haki yako na hakuna kitu utafanya.
Sitampigia kura Samia 2025. Kama una ungana nami ongeza mengine. Na kama huungani nami prove me wrong.