MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mimi ni mkristo na ninaamini Mungu yupo na anatenda. Ila kuna mambo ukisoma kwenye biblia lazima ujiulize maswali mengi sana yanayokosa majibu. Leo nitashea nanyi mambo ambayo naona kama yana ukakasi;
1. Kwenye Mwanzo 1:26 imeandikwa kuwa Mungu alisema tuumbe mtu kwa mfano wetu. Nimejiuliza ina maana uumbaji ulifanywa nae kwa kushirikiana na wengine? Hakuwa peke yake? Hao wengine kina nani?
2. Mwanzo 6 - 10 kuna stori maarufu ya Nuhu. Hii ni stori ina ukakasi zaidi. Nikiandika maswali yote niliyojiuliza uzi utakuwa mrefu. Ninashauri mkaisome ili tuifungulie uzi wake.
3. Kutoka 11:5-6 kuna maandiko yanayosema kuwa wazaliwa wa kwanza wote wa wamisri kwa upande wa binadamu hadi wanyama watauwawa na Mungu mwenyewe ili waisraeli wapewe ruhusa ya kwenda nchi ya ahadi. Kiukweli haya yalikuwa ni mauaji ya halaiki kwa wasio na hatia. Unaambiwa hadi mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, kuku, ng'ombe, mbwa na farasi waliuwawa. Kwanini isingetumika njia nyingine hao waisraeli wakaondoka?
4. Kitabu kizima cha Joshua kimejaa stori za mauaji matupu. Ikumbukwe Joshua alichukua nafasi ya Musa kwenye kuwaingiza waisraeli nchi ya ahadi baada ya kifo cha Musa. Nchi waliyoahidiwa ilikuwa tayari ina wakazi wake ambao ilibidi wauwawe wote ili kuwapisha waisraeli. Hivi ilishindikana vipi kufanya kama alivyofanya Mama Samia kuwatoa wamasai Ngorongoro na kuwapeleka Msomera kwa amani kabisa bila kumwaga damu? Kama leo 2024 bado kuna maeneo duniani hayajakaliwa na binadamu ilikuwaje enzi za Joshua? Ukisoma kitabu cha Joshua utaona kila sehemu waliyopita walikuwa wakiua wenyeji watakaowakuta. Kulikuwa na sababu zipi za msingi za mauaji haya yote?
5. Ayubu 1:6-12 utaona stori ya shetani alipojiunga na wana wa Mungu kupita mbele ya Mungu kumwabudu hadi Mungu akashangaa imekuwaje shetani akawa eneo lile? Baada ya hapo Mungu na Shetani wakakubaliana kwenda kumjaribu Ayubu kwa sharti la kutogusa mwili wa ajabu (kumuua). Katika yale majaribu watoto wa Ayubu waliuwawa na shetani. Naweza kusema ni mauaji yaliyokuwa na approval toka juu. Ilikuwa kazi maalum. Je, sio kwamba wawili hawa hukutana na kukubaliana baadhi ya mambo? Sio kwamba kuna kazi za shetani zina kibali maalum?