Hizi ni stori za kwenye Biblia ambazo zimeniacha na maswali sana

Hizi ni stori za kwenye Biblia ambazo zimeniacha na maswali sana

Mimi ni mkristo na ninaamini Mungu yupo na anatenda. Ila kuna mambo ukisoma kwenye biblia lazima ujiulize maswali mengi sana yanayokosa majibu. Leo nitashea nanyi mambo ambayo naona kama yana ukakasi;

1. Kwenye Mwanzo 1:26 imeandikwa kuwa Mungu alisema tuumbe mtu kwa mfano wetu. Nimejiuliza ina maana uumbaji ulifanywa nae kwa kushirikiana na wengine? Hakuwa peke yake? Hao wengine kina nani?

2. Mwanzo 6 - 10 kuna stori maarufu ya Nuhu. Hii ni stori ina ukakasi zaidi. Nikiandika maswali yote niliyojiuliza uzi utakuwa mrefu. Ninashauri mkaisome ili tuifungulie uzi wake.

3. Kutoka 11:5-6 kuna maandiko yanayosema kuwa wazaliwa wa kwanza wote wa wamisri kwa upande wa binadamu hadi wanyama watauwawa na Mungu mwenyewe ili waisraeli wapewe ruhusa ya kwenda nchi ya ahadi. Kiukweli haya yalikuwa ni mauaji ya halaiki kwa wasio na hatia. Unaambiwa hadi mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, kuku, ng'ombe, mbwa na farasi waliuwawa. Kwanini isingetumika njia nyingine hao waisraeli wakaondoka?

4. Kitabu kizima cha Joshua kimejaa stori za mauaji matupu. Ikumbukwe Joshua alichukua nafasi ya Musa kwenye kuwaingiza waisraeli nchi ya ahadi baada ya kifo cha Musa. Nchi waliyoahidiwa ilikuwa tayari ina wakazi wake ambao ilibidi wauwawe wote ili kuwapisha waisraeli. Hivi ilishindikana vipi kufanya kama alivyofanya Mama Samia kuwatoa wamasai Ngorongoro na kuwapeleka Msomera kwa amani kabisa bila kumwaga damu? Kama leo 2024 bado kuna maeneo duniani hayajakaliwa na binadamu ilikuwaje enzi za Joshua? Ukisoma kitabu cha Joshua utaona kila sehemu waliyopita walikuwa wakiua wenyeji watakaowakuta. Kulikuwa na sababu zipi za msingi za mauaji haya yote?

5. Ayubu 1:6-12 utaona stori ya shetani alipojiunga na wana wa Mungu kupita mbele ya Mungu kumwabudu hadi Mungu akashangaa imekuwaje shetani akawa eneo lile? Baada ya hapo Mungu na Shetani wakakubaliana kwenda kumjaribu Ayubu kwa sharti la kutogusa mwili wa ajabu (kumuua). Katika yale majaribu watoto wa Ayubu waliuwawa na shetani. Naweza kusema ni mauaji yaliyokuwa na approval toka juu. Ilikuwa kazi maalum. Je, sio kwamba wawili hawa hukutana na kukubaliana baadhi ya mambo? Sio kwamba kuna kazi za shetani zina kibali maalum?
Ngoja waje wakujibu uenda bado wamelala.
 
rejea Yohana 1:1,
"Hapo mwanzo kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa kwa Mungu, na Neno alikuwa Mungu." (Yohana 1:1,
TAFSIRI YAKE...
  1. Neno ni sehemu ya asili ya Mungu.
  2. uhusiano wa karibu kati ya Mungu Baba na "Neno" (Yesu), akisema kuwa "Neno" lilikuwa kwa Mungu tangu mwanzo wa kila kitu
  3. Wakristo wanaamini kwamba "Neno" lilijificha katika mwili wa Yesu Kristu (Yohana 1:14). Yesu, akiwa Neno la Mungu, alikubaliana kuwa binadamu ili kuleta wokovu kwa wanadamu.
Wewe ni mjinga wa wajinga, kwa nini wenzio hawakujibu hoja zangu, kwasabu nimepiga kwenye mshono hapo hapo , soma maandiko yangu vizuri nimetoa ktk bibilia yenu

Rejea SIfa za Mungu ktk bibilia
Mungu habadiliki
Sauti ya Mungu haijapata kusikika
Mungu halali usingizi nk

hizo ni baadhi ya sifa za Mungu ktk bibilia , na hayo ni maneno yake mwenyewe ,
Sasa wewe unataka watu wa si iamini bibilia,
Huyo YESU wako alikuwa hana hizo sifa, Mungu habadiliki bibilia ina sema alafu wewe Eti ooh neno ooh akawa yesu , porojo tupu
 
BIBLIA NI NGUMU ,NMEPITIA HAPA
Zaburi 90:10:
-"Miaka ya umri wetu ni sabini, au, ikiwa ni nguvu, thelathini na tano; lakini mrefu wake ni uchungu na huzuni, maana huisha kwa haraka, nasi twapita." (Zaburi 90:10)
Muongo , bibilia uongo mwingi ndio umejaa na visa vya kutungwa na kubuni ndio vimejaa
 
  1. Yesu ni Mungu katika Umbo la Kibinadamu (Ukristo), Ingawa Yesu alijitambulisha kama "Mwana wa Mungu", imani ya Kikristo inafundisha kwamba alikubali kuwa binadamu ili kumkomboa mwanadamu, lakini haimaanishi kuwa alikosa uungu wake. Hivyo, Yesu alichukua hali mbili: ya kibinadamu na ya uungu.
  2. Mungu hawezi Kubadilika (Uislamu): Hii inatokana na imani ya Tawhid ambapo Allah ni mmoja, hawezi kushirikishwa na yeyote, na hivyo Yesu hawezi kuwa Mungu kwa sababu Allah hawezi kubadilika na kujificha katika umbo la kibinadamu.
  3. Yesu kama Mwana wa Mungu ni tafsiri ya kiroho katika Ukristo na si kwa maana ya kibiolojia. Hii ni tofauti na Uislamu ambapo Yesu ni nabii, na Allah pekee ni Mola. Tafsiri hizi zinatofautiana kwa msingi wa mafundisho ya kila dini.
I think. Hii ni last comment yangu kwako, wewe hamnazo nimetoa andiko ktk bibilia yako baada ya kuona bibilia. Imekusaliti una tapatapa , huna hoja wana Jamii forum wameona jinsi ulivyo empty ki misingi
Hakuna anayeweza itetea bibilia
Mungu habadiliki 1:17 yakobo
 
"Ah, kumbe unaishi katika ulimwengu wa akili zako tu, ambapo ukweli unaendeshwa na maoni yako binafsi! Lakini, kama vile Aristotle alivyosema, 'Ukweli haupo katika mawazo yetu, bali katika maumbile.' Labda tunahitaji kumrudisha mtaalamu wa falsafa ili kuelewa kwamba Mungu hakubadiliki hata kama mawazo yetu yanabadilika kila siku."
 
Muongo , bibilia uongo mwingi ndio umejaa na visa vya kutungwa na kubuni ndio vimejaa
je haya ni ya kweli ?
Hadithi inayosema kuwa shahidi atapata mabikra 70 peponi ni sehemu ya mafundisho ya kiroho?,endelea kukanusha mawazo ya wengine kwa kejeli
 
BIBLIA NI NGUMU ,NMEPITIA HAPA
Zaburi 90:10:
-"Miaka ya umri wetu ni sabini, au, ikiwa ni nguvu, thelathini na tano; lakini mrefu wake ni uchungu na huzuni, maana huisha kwa haraka, nasi twapita." (Zaburi 90:10)
Haya ni maneno ya daudi nadhani na ni kweli watu wengi tunakufa tukiwa kati ya miaka 35 -70. Na ni kweli

Ila kwa rekodi za haraka watu wengi hawavuki miaka 120. Kwa muda mrefu sasa.

Kama yupo sidhani labda kama hajahesabiwa vizuri umri. Kuna makosa..
Na hilo Mungu alisema kwenye kitabu cha mwanzo maana binadamu walikuwa wanaishi miaka 300+ hadi 900+
Ila wakawa wanamuumiza kichwa sana maana wengine madhambi yalikuwa mengi. So akashusha umri wa kuishi.

Sasa pata picha hadi sasa watu tungekuwa tunaishi miaka mingi hivyo kwa vichwa vibovu vilivyowahi kuwepo hapa duniani ingekuwaje.

Mwanzo 6:3 SRUV

BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.
 
Haya ni maneno ya daudi nadhani na ni kweli watu wengi tunakufa tukiwa kati ya miaka 35 -70. Na ni kweli

Ila kwa rekodi za haraka watu wengi hawavuki miaka 120. Kwa muda mrefu sasa.

Kama yupo sidhani labda kama hajahesabiwa vizuri umri. Kuna makosa..
Na hilo Mungu alisema kwenye kitabu cha mwanzo maana binadamu walikuwa wanaishi miaka 300+ hadi 900+
Ila wakawa wanamuumiza kichwa sana maana wengine madhambi yalikuwa mengi. So akashusha umri wa kuishi.

Sasa pata picha hadi sasa watu tungekuwa tunaishi miaka mingi hivyo kwa vichwa vibovu vilivyowahi kuwepo hapa duniani ingekuwaje.
dhambi nyingi,kunyanyasana, ufuska ungekuwa mwingi
 
Back
Top Bottom