Biblia ipo kiroho zaidi. Huwezi elewa baadhi ya maandiko mpaka umaanishe kumfuata Kristo.
“ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.
”
— Marko 4:12
Kwa kukusaidia machache:
1. Tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu: kumbe yupo Mungu Baba, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu
3. Hapo kwa wazaliwa wa kwanza, kibinadamu ni wazaliwa wa kwanza ndiyo, lakini Mungu alikuwa anashughulikia miungu ya Wamisri inayompa kiburi farao. Hapo ilikuwa vita ya Mungu na miungu. Kumbuka Waisraeli walikuwa ni wazaliwa wa kwanza kwa Mungu kabla ya mataifa mengine yote.
4. Hapo kwa Joshua, kumbuka huko nyuma aliangamiza wanadamu wote na kubaki Nuhu tu sababu ya maovu mengi ya wanadamu. Kumbuka Sodoma na Gomora. Kumbuka Ninawi. Toka Adam atende dhambi, ndiyo mwanzo wa mauaji, mwanzo wa kuondoka amani duniani. Biblia inasema hakuna amani kwa wabaya. Na Yesu hakuja kuleta amani duniani bali upanga ili mtu achukiane na ndugu yake. Halafu akaleta amani yake ya kipekee tofauti na hizi amani za kidunia. Joshua aliwaua wote waliokataa kufanya shirika na Israel, na waisrael walikatazwa kuoana na watu wa maraifa mengine kwani wangewafanya Israel waabudu miungu mingine. Hata sasa tunaishi duniani Mungu akiwa na huruma lakini huruma ya Mungu haipo kwa wafu. Aliyekufa katika dhambi hakuna msamaha tena, ukomo wa huruma ya Mungu.
5. Kuhusu Ayubu. Kwani kwanin Mungu kamwacha shetani kwa muda. Hapo mwanzo Shetani alitaka kuabudiwa kwa kushawishi malaika wenzake kuwa Mungu ni dikteta. Mungu akamwacha ili kudhihirisha je, madai ya Shetani ni kweli au uongo. Akamwacha kila malaika na kila mwanadamu afanye machaguzi aidha ya kusimama na Mungu au kumwamini Shetani. Leo watu wote tunaoana Shetani ni mwongo. Tafuta kitabu cha Yashari (the book of jashar) na kitabu cha henoko (The book of enock). Utaona mengi humo