Hizi ni tabia za kukosa ustaarabu na kishenzi (uncultured) kwa sisi madereva tukiwa barabarani, tubadilike

Aisee;..

1. Kuhusu kuingia barabarani: Siyo jukumu la dereva wa barabara kubwa kusimama, isipokuwa ni wajibu wa dereva wa barabara ndogo kuhakikisha kwamba kwenye barabara kubwa hakuna gari iliyokaribu na ama ni salama kuingia bila kusababisha usumbufu ama ajali.

2. Kuhusu kutoa shukrani; siyo lazima na haswa ikiwa kufanya hivyo si salama. Mfano unakuta gari ina mzigo mkubwa na barabara imekaa vibaya kiasi kwamba dereva anayeingia anapaswa kuzidisha umakini kuliko kuanza kuchanganyw mambo kwa kutoa shukrani wakati namba moja (1) hapo juu inajulikana kwamba kuingia barabarani ni wajibu wa anayeingia kulinda usalama.

3. Ni wajibu kwa anaye-overtake kuhakikisha kwamba ni salama kufanya hivyo, ikiwemo kutoa taarifa kwa madereva wengine kwamba anataka kufanya hivyo. Siyo kuvizia vizia na kuchomoka. Dereva wa mbele hana wajibu wa kupunguza ili upite isipokuwa wewe unayetaka kumpita ndiye unatakiwa ujipime iwapo unaweza kumpita salama.

4. Namba nne inajibiwa na namba 3. Kwamba wajibu wa anaye-overtake kuchukua tahadhari na siyo kuruka ruka na kukurupuka.

5. Ni wajibu wa mtembea kwa miguu kuhakikisha kwamba gari zimesimama, ndiyo avuke kwenye zebra. Wajibu wa dereva ni kupunguza mwendo ili kuhakikisha kwamba hakuna mvukaji. Hivyo, kwenye kuvuka, ni wajibu wa mvukaji kuzingatia usalama na siyo dereva. Hii haihusishi zebra àmbazo zimewekwa alama ya STOP ambapo no sharti dereva kusimama kwa muda halafu ndiyo apite.


...............,............

Fungo Augustus ▶ ‎RSA TANZANIA(Road Safety Ambassadors)

JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA?
Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.

Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.

Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.

Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja
Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari.

[Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa].
Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.

KWA MINAJILI YA REJEA KIFUNGU CHENYEWE CHA 65(10) Kinasema hivi katika lugha yake asili "(10) Where a pedestrian is using or is about to use a pedestrian crossing, a driver of a vehicle shall stop before a pedestrian crossing on a carriageway which is not regulated by traffic lights, traffic signals or by a police officer."

HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari.

Kwa hiyo, dereva asimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.


Ni matumaini yangu tumeelewana. Mwelimishe na mwenzio.


ZINGATIA: Maelezo haya hayahusishi zile ZEBRA crossings ambazo kabla yake kunakuwa na mchoro chini au alama ya amri iliyoandikwa kabisaaa STOP. Hapa utatakiwa kusimama hata kama hakuna anayevuka.
 
Siku hizi reckless driving kumezidii sana kupita kiasi mabarabarani, hakuna ushirikiano wa kuhakikisha mabarabara zetu zinakuwa salama, kuanzia bajaji, bodaboda, magari madogo kwa makubwa, ila magari makubwa wengine wana ustaarabu sana unaona kabisa kabisa anavyoendesha ukiwa nyuma yake utafurahi mwenyewe anavyokuongoza!
 
kwanza elewa kwamba “mshenzi” ni muislamu mweusi, ndiyo maana na asili ya neno mshenzi, ni derogatory term for a black muslim, mwarabu aliita muislamu mweusi “mshenzi”, kwa hiyo mwenye “tabia za kishenzi” anaweza tu kuwa muislamu mweusi kwa maana halisi ya neno mshenzi …
 
Hiyo namba 3 madereva daladala na kaka zao wa mabasi ya masafa hawaji kuacha kamwe.
 
Kuovertake Halafu ghafla na kupinda kushoto au kulima bila kuonyesha ishara ya mwelekeo(indicator).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…