Hizi ni tabia za kukosa ustaarabu na kishenzi (uncultured) kwa sisi madereva tukiwa barabarani, tubadilike

Huo ushenzi namba 3 unanihusu 100%...😜😜
 
Madereva wa gari ndogo ndo huwa wanakaza kindezi tu.
Wengi hawana zile fair play za road, wao ni kukaza tu. Akiwa mdada ndo kabisaaa ila wao wanataka kuonewa huruma.
Na wewe kwa nini ulazimishe. Ni ushenzi na ujuha.
 
Kwakweli halafu unakuta mtu mwingine ame overtake vibaya ghafla anakutana na jam anarudi lane yake ghafla ww unatoka barabarani, ni ushenzi!
 
Hiyo namba 3 madereva daladala na kaka zao wa mabasi ya masafa hawaji kuacha kamwe.
Madaladala ya Papafololo ya Mburahati Posta na daladala za Nangaboy Segerea Mnazi mmoja.
Nadhani hizi ni za vigogo fulani.
Mungu yupo
 
Mkimalizana na madereva wa magari tuhamie kwenye kikao cha kuwajadili untouchable group on the road a.k.a BODA BODA,wananikera sana na masauti yao ya piki piki (noise pollution) imekuwa kama fashen sasa hivi yaani mtu Yuko umbali wa kama kilometa 4 ila unaanza kusikia sauti kali ya piki piki na hapo hajafika ulipo.Hawa watu wadhibitiwe aisee maana imekuwa kero japo wao wanaona ndio ujanja na sifa
 
Hapa hatuongelei sheria, tunaongelea ustaarabu, sasa kama wewe unafanya ushenzi na kukosa ustaarabu kwa sababu hakuna sheria inakutaka ufanye tofauti basi una tatizo.

Hakuna sheria inasema unapokuwa na watu mnakula chakula pamoja acha kuongea ukiwa unatafuna chakula mdomoni - lakini ukiwa na tabia ya kufanya hivyo wewe ni mshenzi na huna ustaarabu.

Kuna mtu alitoa post humu kuhusu watu kula ugali pamoja huku kila mara wanajiramba vidole na kuendelea kula - huo ni ushenzi na kukosa ustaarabu, lakini hakuna sheria juu ya hilo.

Sasa wewe unaona wazi magari yako main road bumper to bumper hakuna nafasi ya mtu kuingia na humwachii mtu anaetaka kuingia kwa sababu sheria inasema asubiri kuwe hakuna gari - huo ni ushenzi na kukosa ustaarabu!
 
Ukipita Old Bagamoyo road huko Daslama kwenu ndo hizi tabia ulizosema mleta sledi
 

Hili povu jingi sana. Pole!
 
No. 3. Mara kadhaa nimekutana na situation ya gari mbele yangu likienda taratibu muda mrefu. Fursa ikitokea ukawasha kiashirio cha kulia na kuanza kupita (overtake) ndio kama umemuamsha mtu anaanza kuongeza mwendo mpaka unashangaa.

Kizuri huwa na naangalia magari ya kuendelea ku-overtake na ya kuachia ikitokea hali kama hiyo. Huwa sipendi kukanyaga sana - hadi nilazimike. I have my ideal speed.

Lakini kama alivyosema mleta mada si ustaarabu kabisa. Ukiamua kwenda mwendo mdogo na nyuma yako kuna magari yanakusanyika acha yapite. Vinginevyo, ukiona yanakaribia na wewe hutaki kupitwa basi ongeza mwendo kabla yasifikirie kikupita. Lazima uwe consistent barabarani. ‘usiendeshwe’ na watu wengine wakati kila mtu ana safari yake.

Kero nyingine uko kwenye barabara kuu, mbele jirani gari tokea njia ya pembeni linakuja na kuingia mbele yako kwa kasi hadi unalazimika kukanyaga breki za ghafla. Halafu sasa linaendelea na kasi ndogo tofauti na liliyoingia. Ukilipita unakuta dereva anaongea na simu ame-relax kabisa kama yuko kibarazani kwake!

Haya mambo hapa kwetu hayana sheria lakini ustaarabu barabarani ni kitu muhimu sana. Siku hizi gari ni kitu cha kawaida sana; halitakiwi “kumpanda mtu kichwani”.
 
Ukipita Old Bagamoyo road huko Daslama kwenu ndo hizi tabia ulizosema mleta sledi
Yaani Old Bagamoyo ndio hakufai kabisa! Kule kila mtu ni kingunge, mtoto wa kingunge au usalama wa taifa - anataka aachiwe barabara!
 
Well said Mkuu!
 
Hili povu jingi sana. Pole!
Ujumbe umefika lakini? Badilika bwana. Tunataka tuendeshe IST zetu na kufurahi kuwa nazo barabarani, sio kupata ugonjwa wa pressure kwa hofu za kila wakati au hasira kunakosababishwa na madereva wengine washenzi na wasio wastaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…