Hizi roho za watu wasio na hatia waliouawa siku ya mapinduzi ya Zanzibar January 12, 1964 zinahitaji kutendewa haki

Hizi roho za watu wasio na hatia waliouawa siku ya mapinduzi ya Zanzibar January 12, 1964 zinahitaji kutendewa haki

Baada ya mapinduzi ndio ukaja muungano.?? Hapo uki unganisha dots utagundua mapinduzi ya zanzibar ilitakiwa iitwe mauwaji ya zanzibar

Na hapo lazima kulikuwa na mkono wa ticha

Kiukweli waisilamu waliuawa sana kwa mlengo wa mapinduzi
 
Na Kina Mbowe tulioambiwa ni gaidi na yule aliyepigwa risasi kwenye viwanja vya Bunge na wale waliookotwa coco beach, Chama chao ni dini gani na kiongozi wao ni mtume gani?
watu wa siasa dini yao ni utawala mungu wao ni pesa,hata wakauana sawa tu lakini muisilamu akifia kwenye ujinga huo anakufa akiwa kafiri anaenda motoni tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya mapinduzi ndio ukaja muungano.?? Hapo uki unganisha dots utagundua mapinduzi ya zanzibar ilitakiwa iitwe mauwaji ya zanzibar

Na hapo lazima kulikuwa na mkono wa ticha

Kiukweli waisilamu waliuawa sana kwa mlengo wa mapinduzi

Hata mimi hili limenifikirisha sana.

Ile haraka ya kupindua serikali iliyochaguliwa na wananchi huko Zanzibar ambayo ilikuwa na umri wa mwezi mmoja tu, na haraka ya kufanya muungano baada ya mapinduzi inaonyesha dhahiri waliokimbilia kufanya muungano ni wahusika wakuu wa ile chinjachinja inayoitwa mapinduzi matukufu.

Damu za watu wale wasio na hatia hazitowaacha salama, zitadai haki mbele ya Muumba!
 
Walioorganise na kuratibu yale mapinduzi baadhi yao wamepata adhabu hapahapa duniani
Kassim Hanga alipotezwa, hjulikani alipo mpaka leo
Karume aliuawa kwa shaba
Profesa Babu(japo alikana kuhusika lakini alihusuika) aliishi jela na uhamishoni kama digidigi
Kambona (miongoni mwa waratibu wakuu wa upatikanaji silaha) aliishia kuishia ukimbizini kama digidigi
Mzee Jumbe, aliishia kuwekwa kifungo cha ndani
John Okello, aliondolewa Zanzibar na Tanganyika kwa aibu
Nassoro Moyo alikuja baadae kufedheheshwa kwa kutimuliwa CCM uzeeni
 
Kuna propaganda kubwa sana za kuwaita Wahanga wa Yale Mapinduzi kuwa ni waarabu na kwa hiyo eti hakuna haja ya kujali. Hii inasikitisha sana. Hata wangekuwa waarabu tupu waliuawa, still ni unyama!

Hata hivyo, Wazanzibar wamechanganya damu sana. Yaani kama jinsi unavyowaona Wazanzibar wa leo, muonekano wao wa leo etc. ndivyo hivyohivyo walivyokuwa wakionekana hata mwaka 1964.

Hata miongoni mwa Wafalme wa Zanzibar, miongoni mwa Wafalme walikuwa na damu iliyochanganyika. Unamkuta mfalme ana damu ya Watu weusi na waarabu, kama ambavyo Wazanzibar wa kawaida nao walimix.

Hebu Angalia Huyu Sultani Wa Zanzibar , anaitwa Ali bin Hamud alipokuwa mdogo. Hii picha ilipigwa mwaka 1890.

20230116_130625.jpg

Miaka 12 baadae (mwaka 1902)akawa sultan. Anaonekana hivi.
Zanz-Ali_II.jpg
 
Bahari imetulia inasubiri uchafuzi uitwao uchaguzi, mauwaji na mateso yaendelee. Tunawasubiri mje na majeshi ya wahutu wa Burundi Kama mwaka juzi muendeleze mauwaji

Endapo mkileta chokochoko hamtavumiliwa
 
Hata mimi hili limenifikirisha sana.

Ile haraka ya kupindua serikali iliyochaguliwa na wananchi huko Zanzibar ambayo ilikuwa na umri wa mwezi mmoja tu, na haraka ya kufanya muungano baada ya mapinduzi inaonyesha dhahiri waliokimbilia kufanya muungano ni wahusika wakuu wa ile chinjachinja inayoitwa mapinduzi matukufu.

Damu za watu wale wasio na hatia hazitowaacha salama, zitadai haki mbele ya Muumba!
Hivi nañi alimuua karume na ni Kwa nini?
 
Back
Top Bottom