Hofu hii inasababishwa na nini na kwanini haikuwapo wakati wa kupigania uhuru?

Hofu hii inasababishwa na nini na kwanini haikuwapo wakati wa kupigania uhuru?

Kuna mtu anaitwa juma na mwingine maulid lakin ni wakristo unavyosema huwez ni sheria ipi inazuia mtu kuitwa abdalah na hawez kuwa mkristo acha upotoshaji

..ukiona hivyo ujue mhusika anatokea ktk jamii ambayo ilifikiwa na dini ya Kiislamu kabla ya dini ya Kikristo.
 
Kuna mtu anaitwa juma na mwingine maulid lakin ni wakristo unavyosema huwez ni sheria ipi inazuia mtu kuitwa abdalah na hawez kuwa mkristo acha upotoshaji
Juma si neno tu la kiarabu, wapo pia watu wanaitwa jumanne waisilamu na Wakristo, kuna majina ya kiisilamu na Kiarabu Juma ni la kiarabu.

Mfano nakupa majina wa Waarabu Wakristo, Feirouz (feruzi), Salim, warda, walid etc haya ni majina ambayo kwetu mtu akiitwa Utasema ni muisilamu ila uhalisia ni majina ya kiarabu.

Ila Ukiona neno Abdul then linafuatiwa na jina La mwenyezi Mungu hilo ni jina la kiisilamu, hutakuta mkristo Muarabu anaitwa hivyo. Iwe Abdul Rahman, Abdullah, Abdul Malik, Abdul Salam, AbdulAziz etc.

SSababu kwenye uisilamu Tunaamini ukishakua muisilamu una Submit to Allah na neno Abd linamaanisha Mja hivyo tunaanza na hilo neno kisha tunaweka Moja wapo ya majina 99 ya mungu.

Kama vile ambavyo jina Baptista ama Bautista ni exclusive la kikristo, wapo waisilamu wanaitwa Daniel, Moses etc ila Baptista ni exclusive la Kikristo MAANA linaongelea dini ubatizaji.
 
Mohamed Said hua nasoma sana makala zako nikiri kwamba zimeongeza Jambo kwenye ubongo wangu hata nikipita baadhi ya sehemu hapa mjini hua navuta picha ya makala zako nikijurudisha enzi hizo. Nimefika Kalenga yule bwana mtoa historia ya Mtwa mkwawa mwenye jina refu kama treni alikuwepo. Mkwawa alikua ni Mwisilamu hilo sio hoja hata kidogo hata hiyo barua niliiona na tafsiri tulipewa. Na ni kweli Mkwawa alisilimishwa na Abushiri kama ulivosema hilo nakuunga mkono pasi na shaka wala hutakiwi kushupaza shingo kulitetea Mkwawa alikua ni mwisilamu na amefariki akiwa ndani ya uislamu. Pia hizi hoja ndogo ndogo ulitakiwa uzijibu bila kuzikwepa majina ni ya kiarabu na sio ya kiislamu ila dini ya kiislamu inatumia sana majina ya Kiarabu. Ukienda Iringa sio kila Issa unaekutana nae huko ni Mwislamu au sio kila Asha, Mudi, Said ni waislamu la hasha. Mimi ni mzaliwa wa Nyanda za juu kusini watu wanatoa tuu majina kwa sababu kalisikia yule anaitwa hivyo wala sio kwa sababu ni la kiislamu, labda siku hizi kidogo Uislamu umeingia sana kule. Na ni kweli asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa wa Iringa na Njombe ni wa kristo lakini Mkwawa ali silimu hata ukoo wake mpaka leo ni Waislamu labda Mjerumani angechelewa kuingia kulikua na uwezekano mkubwa sana Uislamu kuenea kule. Kule wilayani kwangu hakujawahi kua na msikiti mpaka mwaka 2004 ndo msikiti wa kwanza ulijengwa tena na wafanyakazi wa Serikali wenye Imani ya Kiislamu ndo walijenga na Uislamu ukaannza kujulikana kule. Ndio maana nimesema hoja ya jina ulipaswa kujibu tu ni majina ya kiarabu kwa sababu ukiwaona wakristo waliopo mataifa ya uarabuni wakisali unaweza sema ni waislamu kwa sababu ya Lugha inayotumika. Kuhusu kuandika historia sijui ni nchi gani inayo andika histirua hiyo kwamba Nyerere alipigania uhuru wa Tanzania na alikua mkristo, au Nkuruma alipigania uhuru wa ghana na alikua mkristo,. Pia akaburi mengi kama sio yote kwa Iringa yale ya zamani yapo kama hili la mkwawa hata yale ya Njiani yaliyo kua yanazuia umeme kupita yanafanana na ya Kiislamu hivyo watu wanaweza wasielewe hoja kwa sababu hiyo. Lakini itoshe kusema mkwa ali Silimu lakini Jeshi lak hali kusilimu kwa kiasi hicho inawezekana wap waliobadili dini kutoka zile za asili kuja za ya Kiaramu kwa sababu Ukristo ulikua bado haujafika umekuja baada ya Mkwawa kuuwawa ndipo wamisionary wa kijerumani walipo jichia na mimi nilipozaliwa nikajikuta nipo kwenye Ukristo.
Thanks for this useful post.
 
..ukiona hivyo ujue mhusika anatokea ktk jamii ambayo ilifikiwa na dini ya Kiislamu kabla ya dini ya Kikristo.
Si kweli, Musoma jamii za kiislamu au uislamu uliingia lini?

Nenda kule utakuta kina Juma wengi tu, Abdala, Musa wanaita Msa.

Kuna jamii ilipendaga tu majina kama kizazi chetu cha sasa kinavyopenda kuiga majina ya uzungu uzungu.

Siku hizi watoto wa kiislamu wengi tu wanapewa majina ya Dayana, Sasha, Natasha ili mradi kutaka uzungu uzungu tu na majina haya so ya kiislamu wala si ya kikristo, ila wenye hayo majina wana dini zao.

Mimi napenda Sana na najisikia fahari kumuita na kumtamka Sheikh Mazinge, Sheikh Ponda, Sheikh Mataka, Sheikh Gologosi, hivi hapo hao masheikh wetu kwa kuitwa hivyo kwa majina yao ya asili, je wamepotezs Usheikh wao na uislamu wao?

Lakini hali ni tofauti kwa Mzee wetu Mohamed Said hata majina yake ya asili hayataki ila majina yakiarabu yeye ndio yanampa fahari.

Licha ya heshima kubwa aliyonayo Mzee wetu haya nayo ni mapungufu yake makubwa na mbaya zaidi huwa hawezi kukuelewa kwa lolote juu ya kile anachokiamini lakini wakati huohuo akitaka wengine nao wasiamini wanachokiamini na ndio mwisho wa siku Mzee wetu huishia kwenye muslim movement Propagandist au kama Modern Mujahedeen fulani tu hivi mwenye cover ya mwanahistoria.
 
Matola,
Nazungumza kuhusu historia iliyopotoshwa na mimi nikaja kuiweka sawa.

Huu ndiyo mjadala wetu hapa.
Je nimesema kweli?
 
Back
Top Bottom