Hv kugombania dini ya mtu fulani itatusaidia ni i Waafrika. Au dini Inaumuhimu hmgani kwetu?
Ed ...
Tatizo lililopo Tanzania ni hofu iliyopo juu ya Uislam.
Mkwawa Museum ndiyo wanaeleza kuwa Mkwawa alikuwa Muislam.
Watu wanapinga.
Songea Mbano jina lake Abdulrauf Songea Mbano.
Inapingwa.
Mkomanile jina lake Khadija Mkomanile.
Inapingwa.
Africa Association iliasisiwa na watu tisa saba ni Waislam na sababu wamishionari wakiwakataza waumini wao kujiingiza katika siasa.
Hili halitakiwi lisemwe.
Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika alikuwa anauza kadi za TANU msikitini.
Baraza la Wazee wa TANU liliundwa na wajumbe 120 wote Waislam hili halitakiwi liwe katika historia ya TANU.
Halitakiwi hili lisemwe nk.nk. nk.
Mradi ni Uislam ni mwiko kuwa sehemu ya historia ya Tanganyika.
Matokeo yake Chuo Cha CCM Kivukoni ikaandika historia ya TANU ikimlenga Nyerere peke yake.
Lakini Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka wa 1952 harakati zimeanza 1929 kapokelewa na Abdul Sykes.
Abdul Sykes kadi yake ya TANU na 3 ya ndugu yake No. 2 ya Nyerere kama TAA Territorial President ni No. 1 na hizo kadi za TANU kazichapa Ally Sykes Printpak wachapaji wa gazeti la Tanganyika Standard.
Na hiyo kadi ya Nyerere, Mwalimu kaandikiwa na Ally Sykes.
Historia hii haitakiwi.
Tatizo liko hapo.
Huwezi kufuta historia za watu.
Huu ni muhali mkubwa.
Wenyewe hawatakubali.
Ndiyo leo mko hapa mnasoneshwa historia ambayo hamkupata kuijua, kuisoma wala kuisikia popote.
Mnaonyeshwa picha hamkupata kuziona hata siku moja.
Kujikinga na dhoruba hii mnakimbilia hoja ya "Udini."
Kuwa hii historia ilihujumiwa hili halipiti katika fikra zenu.
Laiti lingepita mngefahamu kuwa hawa waliokula njama kufuta historia ya kweli ya TANU walifanya hivyo katika kujaribu kuhami imani zao.